YANGA IMEONDOKA NA CHAKULA, MAJI HADI USAFIRI YAIFUATA BDF XI
TIMU ya Yanga imeondoka leo alfajiri kuelekea nchini Botswana kwa ajili ya mchezo wao wa marudiano dhidi ya BDF XI unaotarajiwa kupigwa keshokutwa Ijumaa katika Dimba la Roberte nchini humo.

Yanga wameondoka na msafara wa watu 31 wakiwemo wachezaji wanne, benchi la ufundi saba pamoja na viongozi wanne lakini kikubwa zaidi pia wameondoka na maji pamoja na chakula chao ambavyo watavitumia kipindi chote watakachokaa nchini humo.
Akizungumza Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro, alisema kuwa wameamua kufanya hivyo ili kuwaweka wachezaji wao kwenye hali nzuri ya kimchezo na kuwawezesha kuibuka na ushindi kwenye mechi hiyo.
Alisema kuwa kinachowatia hofu mpaka wakaamua kufanya hivyo ni kutokana na kutovifahamu vizuri vyakula wanavyovitumia watu wa Botswana, hivyo wanaogopa huenda wakavikuta vyakula ambavyo siyo sawa na vya huku na kusababisha wachezaji kuwa kwenye hali ngumu na kushindwa kucheza vizuri.
“Timu inaondoka kesho(leo) alfajiri na wachezaji 20, benchi la ufundi saba pamoja na viongozi wanne na tunatarajia kucheza mchezo wetu Februari 27 saa 19:30 GMT (sawa na saa 11:30 kwa saa za Afrika Mashariki) kwenye Uwanja wa Robate, ambao upo kilometa 70 kutoka Mji Mkuu wa Gaborone.
“Tunaondoka na chakula chetu na hatutarajii kutumia kitu chochote cha kwao, yaani kuanzia chakula, maji hadi usafiri, basi letu litakuwepo huko kwa kuwa litawaleta mashabiki wetu ambao watatupa sapoti kwenye mchezo huo,” alisema Muro.

Post a Comment