ad

ad

CAF YAMPELEKA ULAYA KIUNGO WA YANGA SIMON MSUVA

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva, amepanga kuitumia vyema michuano ya Kombe la Shirikisho inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (Caf) kwa ajili ya kujitangaza kimataifa ili kupata soko la kucheza soka la kulipwa hasa katika nchi za Ulaya.

Msuva, mwenye mabao saba katika Ligi Kuu Bara akichuana na mshambuliaji wa Azam FC raia wa Burundi, Didier Kavumbagu aliyefanikiwa kupachika mabao nane, ameonekana kuwa kwenye kasi ya hali ya juu msimu huu.

Kiungo huyo ambaye anaitumikia Yanga kwenye Kombe la Shirikisho Afrika (Caf) ambayo katika mchezo wa kwanza wa nyumbani ilifanikiwa kuwafunga wapinzani wao BDF XI FC ya Botswana mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, amaeonyesha kupania vilivyo.

Akizungumza na Championi Jumatano, Msuva alisema anaamini michuano hiyo ni mikubwa kwa Afrika ambayo inatoa nafasi kwa mawakala na viongozi wa klabu kubwa kuhudhuria mechi hizo kwa ajili ya kuwanunua na kuwauza wachezaji nje ya nchi itampaisha.


Msuva alisema malengo yake ni kucheza soka la kulipwa, hivyo atajibidiisha ndani ya uwanja kwa kutimiza majukumu yake yote ikiwemo kufunga na kutengeneza nafasi za mabao.Aliongeza kuwa, kama akipata nafasi ya kucheza soka la nje ya nchi, basi hatasita na badala yake ataondoka kwa makubaliano maalum kati yake na timu yake.

“Ujue michuano hii ya kimataifa tunayoshiriki ni mikubwa sana ambayo nimepanga kuitumia vyema kuhakikisha inanitangaza kimataifa kwa kupata klabu Ulaya.“Kiukweli malengo ni kucheza soka nje ya nchi, kama nilivyozitimiza ndoto zangu za kucheza klabu kubwa hapa nchini, ninaamini nitazifanikisha ndoto hizo kama ilivyokuwa kwa Samatta (Mbwana), Ulimwengu (Thomas) na Luizio (Juma).

“Nitaondoka kwa makubaliano maalum na endapo klabu itakayonihitaji itafikia makubaliano mazuri na klabu yangu ya Yanga, kikubwa sitaki kuondoka Yanga kwa ubaya.

“Kuhusiana na klabu za hapa nchini, itakayonihitaji nipo tayari kuichezea kwa makubaliano na klabu yangu, kikubwa mimi ninaangalia maslahi na siyo kitu kingine chochote, wachezaji wengi wamepita Yanga na mimi nitapita kama wao.”

No comments

Powered by Blogger.