NILIISHI DUNIA YA PEKE YANGU - 16

ILIPOISHIA;
Mwezi wa pili nao ulikatika bila mabadiliko yoyote, mume wangu alidhoofu na kuwa kama mgonjwa wa kifua kikuu kutokana na mawazo ya kila siku, tulipokuwa wawili aliniambia maneno ambayo kwa kweli yaliniumiza na kunifanya nilie kila mara, maneno ambayo hata hivyo sikukubaliana nayo, alinieleza:
“Mke wangu nina imani ugonjwa huu sitapona leo wala kesho, kwa nini usiniache nife kuliko kupoteza fedha za bure?”
“Maneno gani hayo mume wangu, fedha inatafutwa lakini si uhai wa mtu.”
“Hebu angalia kazi zote zimesimama kwa ajili yangu, utamaliza fedha na kupona nisipone kuna faida gani?”
“Wewe si Mungu wa kujua hatima yako, naomba uniachie sitachoka hata siku moja kukuuguza, naomba mume wangu usinivunje nguvu. Muamini Mungu kama aliweza kukuponya na kifo ugonjwa huu si kitu kikubwa kwake.”
“Ni kweli mke wangu hata hivyo huu ni mwezi wa sita unakatika hakuna mabadiliko yoyote, zaidi ya kila mganga kusema lake lakini hakuna lolote, kwa nini hizo fedha usizifanyie kazi nyingine kuliko kuzipoteza?”
“Mume wangu yote hayo ni kuhangaika, hatujui utaponea wapi?”
SASA ENDELEA...
“Kama ni hivyo heri nirudi nyumbani ili hata wewe uweze kuhangaika.”
Wazo la mume wangu japokuwa sikuliafiki moja kwa moja lakini kwa upande mwingine niliona linafaa kutokana muda mwingi kuupoteza nikiwa nimekaa tu bila ya kufanya kazi.
Lakini kama ningekuwa nyumbani ningeweza hata kwenda dukani na kuingiza fedha kidogo ya matumizi.
Nilimueleza mganga ambaye alikubali turudi nyumbani huku akitupa dawa za kutumia tukiwa nyumbani.
Tulirudi nyumbani kama tulivyoondoka hakukuwa na mabadiliko yoyote zaidi ya mgonjwa na muuguzaji kupungua kutokana na mawazo na mkono kuzidi kusinyaa kiasi cha bega nalo kuanza kukonda.
Kila nilipomuangalia mume wangu roho iliniuma sana, kuna kipindi nilikuwa nikijifungia ndani na kulia mpaka macho yakanivimba huku nikimuuliza Mungu kosa langu ni nini, kwani kila matatizo ni yangu. Nilimuomba Mwenyezi Mungu basi anitazame na mimi kwa jicho la huruma kwani hali kwa upande wangu ilikuwa mbaya sana iliyopoteza matumaini na kuhofia kufikia hatua ya kumkufuru.
Katika kuhangaika kuna dada mmoja alinieleza jambo, kuwa pengine kutopona kwa mume wangu huenda ni chukizo la Mungu kwa kuwa tumekuwa tukutumia nguvu za giza na kumsahau yeye aliyemuokoa mume wangu kwenye kinywa cha mauti.
Alinieleza miujiza ya maombi jinsi yanavyowaponya watu wengi, hivyo nilitakiwa kutubu na kumrudia Mungu.
Nilikubaliana moja kwa moja na wazo lake, kwanza alisema jioni ya siku ile angeniletea mchungaji wa kanisa analosali.
Japokuwa nilikuwa ni muumini wa dhehebu la Romani Katoliki, sikuweza kubisha kwani niliamini kinachoponya ni imani na kuyaamini maneno ya Mungu aliye hai wala si dhehebu.
Jioni alikuja mchungaji ambaye aliendesha ibada ya maombi.Kila alipokuwa akioomba mume wangu aligaagaa chini kama kuna kitu kinataka kutoka mwilini. Mchungaji kila alivyofanya ilikuwa kazi bure pamoja na kukemea pepo litoke mpaka shati lake likalowana na jasho kama mtu aliyenyeshewa na mvua, mume wangu aliendelea kugaagaa lakini pepo lilionekana kuwa na nguvu sana kiasi cha kugoma kutoka.
Mchungaji aliamini kila siku akilikemea pepo mwishowe lingetoka, baada ya jitihada zake kugonga ukuta, nilielekezwa niende katika moja ya makanisa makubwa ya maombezi yenye sifa ndani na nje ya nchi na lazima pepo lile kaidi lingetoka.
Nami nilifanya kama nilivyoshauriwa kwa kuzunguka na mume wangu kwenye makanisa nikiamini kuwa Mungu atatuona nasi kama alivyowaona wengine waliokuwa wakitoa ushuhuda wa kupona kwenye runinga.
Kwangu ilikuwa tofauti na wengine, wengi waliopanda mbele baada ya maombezi walitoa ushuhuda kwa midomo yao kuwa wamepona lakini kwangu ilikuwa tofauti mume wangu alikuwa vilevile.
Hata hivyo, sikuchoka kila kanisa kubwa unalolijua nilifika na mume wangu, lakini sikuona miujiza yoyote, nilijiuliza sisi na wengine tuna tofauti gani ya imani.
Iweje kila aliyepanda alitoa ushuhuda kuwa amepona lakini sisi hata robo ya mabadiliko hayakuwepo.
Nilipouliza mbona kwangu hakuna tofauti kila siku nilielezwa huenda mume wangu imani yake ilikuwa ni ndogo.
Niliamini matatizo humfanya mtu kumjua Mungu, mume wangu naye aliokoka akawa anatumia muda mwingi kusoma Biblia na kuhudhuria misa zote, ilibidi tuhame kutoka ukatoriki na kuhamia ulokole ili kuitafuta huruma ya Mungu.
Lakini mwaka ulikatika bila mabadiliko zaidi ya mume wangu kuzidi kupungua na kuonekana mzee wakati kijana mdogo kabisa. Kingine kilichonishangaza alianza na kutoka mvi kutokana na matatizo. Huwezi kuamini makanisa yote ya kilokole, nilifika kila kanisa, nilikaa zaidi ya miezi miwili hakukuwepo mabadiliko yoyote.
Kila mfuasi wa mchungaji fulani alinipa sifa ya kanisa lao, nami kiguu na njia nilikwenda lakini hakukuwa na mabadiliko. Hali ya mume wangu ilizidi kuwa mbaya hasa mkono kuwa kama wa mtoto mdogo, kweli wanadamu wana sumu kali kushinda ya nyoka.
Mwisho wa siku niliona kama kuna upendeleo kila kanisa nililokwenda watu wengi walitoa ushuhuda wa kupona lakini sisi tulitoka kavu. Japo tulielezwa si wote maombi yao upokelewa mapema, wengine tulitakiwa kuendelea kuomba kwa vile neema za Mungu hazina siku wala saa.
Kila kukicha ilikuwa afadhali ya jana, hatukuchoka kuhudhuria maombi labda kuna siku nasi tutasikilizwa kilio chetu. Lakini hali ya mume wangu ilizidi kuwa mbaya, kila kukicha alikuwa anaweza kutembea akawa hawezi tena wakati huo miguu nayo ilianza kuvimba.
Nilizidi kuchanganyikiwa mtoto wa kike na kushindwa nishike kitu gani ambacho kitakuwa nafuu kwa hali ya mume wangu. Nilijiuliza nimekosea wapi katika kumsaidia mume wangu waganga asilimia kubwa niliwamaliza na kupoteza fedha bila mafanikio. Niligeukia nguvu za Mungu kwa kukubali kuwa mlokole ili tu mume wangu apone lakini vilevile ilikuwa kazi bure.
Siku moja dada mmoja jirani yangu alinishauri nijaribu kutumia na dawa za kizungu. Mwanzo niliona kama kinyume kutokana na dawa za asili na maombi kugonga mwamba. Niliamini dawa za kizungu ndizo haziwezi kabisa.
Lakini aliendelea kunieleza:
“Sikiliza mdogo wangu, hao wanaoombea watu, ndugu zao wakiugua wanakwenda hospitali sembuse wewe usiyejua lolote unakwenda kanisani kwa kufuata mkumbo.”
“Hakuna kitu kama hicho, wao huwa hawaumwi,” nilipinga kwa kuamini wachungaji, maaskofu na familia zao huwa hawaumwi na wakiumwa basi maombi huwaponya haraka.
“Nani kakudanganya, kila mwanadamu anaumwa, ila wao hawajionesha kwa vile ndiyo wanaoongoza maombi kama wakifanya hivyo huenda msiende tena katika makanisa yao.”
“Dada huo ni uzushi mtupu, hata kama kweli wanaumwa lakini hupona kwa maombi.”
“Acha kuwa kipofu wa fikra, unataka kuniambia maombi yao ndiyo yanayoponyesha?”
“Ndiyo.”
“Kama kweli maombi yao ni kila kitu, mbona hawajaenda hospitalini kuombea wagonjwa zaidi ya kujitajirisha wao katika makanisa yao.”
“Hakuna hata mchungaji au askofu aliyewahi kuomba fedha kwa ajili maombi, hayo ni majungu tu,” nilipinga tuhuma zile kwa nguvu zangu zote.
“Mmh! Huwezi kujua, wana mbinu ambazo huwezi kuziona lakini mtaji mkubwa ni ninyi waumini. Kazi hawana, utajiri wa kutisha wanautoa wapi?”
“Wengine wameingia kwenye huduma za kiroho wakiwa wana fedha zao.”
“Esta, ninyi mnaoingia katika madhehebu kwa ajili ya kuamini miujiza na si ucha Mungu, siku zote huwa mnaamini kuliko hata huyo Mungu mwenyewe. Hujui mengi, mbona sisi tunajua mengi? Wapo walioingia huko na kutoka bila kuaga badala ya kupata waliingia kwenye madeni mpaka leo ukiwaeleza habari hizo mnagombana.
“Una habari kuna msaidizi wa mmoja wa viongozi wa kiroho amekwenda kutibiwa nje ya nchi baada ya kusumbuliwa na maumivu ya mguu, kwa nini hawakumuombea akapona, nao ni mabingwa zaidi ya Yesu?”
“Si kweli, kama alikwenda, alikwenda na yake na si kutibiwa kwa vile naamini maombi huponya.”
“Mumeo amepona?”
“Hapana.”
“Sasa hayo maombi gani unayoyajua wewe ambayo hayakuponyi, nasikia hata wachawi huacha uchawi na kuwa watu wema, mumeo karogwa, kwa nini asipone?” Mmh! Swali lile ilikuwa kama kunitoa kwenye kiza kizito.
“Hata mimi nashangaa.”
“Una muda gani?”
“Mrefu sana, kila kanisa nimefika.”
“Basi pata akili, kama wao wakiugua wanakwenda kutibiwa hospitali iweje wewe ung’ang’anie maombi tu, aliyeleta maombi ndiye aliyeleta akili ya kutengeneza dawa. Mbona hao wanaowakataza msitumie dawa zaidi ya maombi, kwa nini hawasafiri kwa maombi badala yake wanasafiri kwa magari ya wazungu?.
Maombi hayakatazwi, ni sehemu ya huduma, kama umeshindwa sehemu moja hamia nyingine, zote ni baraka za Mungu, kibaya kumshirikisha Mungu na kuabudu Miungu mingine lakini dawa za kawaida hazikatazwi.”
“Nimekuelewa shoga yangu, nitafanya hivyo, mpaka sasa sijui nifanye nini nimechanganyikiwa hata sijui nishike mti gani,” maneno ya shoga yangu yaliniingia na kunichanganya sana.
“Usichanganyikiwe, imani yako katika maombi ilikuwa kubwa ukasahau kwamba uweza wa Mungu ni mkubwa si katika maombi tu hata katika miti aliyotuletea kwa ajili ya chakula na dawa, hivi nikikuuliza wakati wa Yesu hapakuwepo maskini?”
“Nina imani hawakuwepo,” nilijibu kwa vile niliamini kama wachungaji wana uwezo kama ule Yesu alikuwa yupo vipi, na wote waliponya kwa jina lake.
“Nataka nikueleze mpaka Yesu anasalitiwa na Yuda pia kukanwa na Petro inaonesha bado walikuwepo wenye mioyo dhaifu pia maskini vipofu hata wagumba walikuwepo. Na kama maombi ni kila kitu hospitali zisingekuwepo kila atakayeombewa angepona bila kwenda hospitali. Lakini haohao wanaoombea watu wanatibiwa na dawa hizihizi kwa vile kumeza au kunywa dawa si dhambi.”
“Inaonekana unaijua dini vizuri?” Nilishangazwa na uwezo wa yule dada katika kuichambua dini.
“Si kwamba naijua dini sana, kuna mambo mengine wanadamu tunayakuza kwa faida zetu wenyewe.”
“Kwa hiyo maombi ni uongo?”
“La hasha maombi si uongo kila mwenye imani maombi yake hupokewa na vilevile hata yakichelewa huwa mvumilivu.”
“Kwa hiyo hata mimi sikutakiwa kukata tamaa.”
“Kama ingekuwa hakuna njia mbadala ulitakiwa uendelee na hayo maombi japokuwa si kwenda kwa mtu bali kujazwa imani na wewe kusimama popote kumlilia Mungu kilio cha kweli chenye kumtegemea yeye hakika Muumba wetu ni msikivu.”
“Kwa nini waumini tunadharauliana?”
“Wapo wanaodharau watu kwa kuamini wao ndiyo wapo sahihi, lakini Mungu ni mmoja na katufundisha tufanyeje tunapokuwa kwenye matatizo.”
“Unaweza kuchanganya maombi na dawa za hospitali?”
“Unaweza kwa vile yote ni kutafuta ufumbuzi, maombi si wakati wa kuumwa tu muda wote unatakiwa kuzungumza na Muumba wako. Ukimkumbuka Mungu kila wakati hata yeye atakukumbuka.”
“Nimekuelewa shoga yangu, leo umeniondoa ukungu kwenye akili yangu.”
“Si ukungu aliyekushawishi kuokoka alikushawishi vibaya na kujikuta kila kitu amehamishia huko na matokeo yake amekuacha ukipata maswali yasiyo na majibu kila siku.”
Baada ya kuachana na shoga yangu ambaye alikuwa Mkristo kama mimi, angekuwa Muislamu ningekuwa na uwalakini. Maneno yake niliyafanyia kazi na kufikiria jinsi nilivyohangaika na mume wangu bila mabadiliko yoyote japokuwa tulionekana hatuna imani. Nilijiuliza imani hiyo ni kwetu tu wakati kuna watu wengi walikuwa na mapungufu ya kibinadamu yaliyokuwa yakijulikana na wengine kukiri kuwa walikuwa wachawi na wazinzi waliokubuhu.
Kwa upande wangu niliingiwa na wasiwasi na uponyaji wa kwenye makanisa yote niliyokwenda kwa kuwa ulikuwa ukichagua baadhi ya watu. Niliamua kuachana na makanisa ya uponyaji na kurudi katika dhehebu langu la Kikatoliki na kumuachia Mungu aamue chochote juu ya hatima yetu. Niliamua kumpeleka hospitali mume wangu ingawaje familia yake bado ilikuwa ikitaka twende kwa waganga wa kienyeji.
“Wazazi wangu kwa nini turudi sehemu iliyoshindikana?”
“Kila mganga ana uwezo wake tujaribu na kwingine,” alisema mama mkwe.
“Jamani wazazi wangu kuna waganga kama tulipokwenda huko Tanga mlipokuwa mnapasifia, nimekaa zaidi ya miezi mitatu bila mafanikio mnfikiri kuna mganga gani zaidi?”
“Tumekueleza unaweza kutumia nguvu nyingi asifanikiwe, lakini ukatumia kidogo tu akafanikiwa.”
“Wazazi wangu nilikuwa naomba tumpeleke baba Fatu hospitali,” nilizidi kuwabembeleza.
“Kwa waganga kumeshindikana, kwenye maombi pamoja na kuokoka kwenu lakini imeshindikana. Mi nilijua huko ni utapeli mtupu ningewakatalia mngeniona mbaya nafikiri mmejionea wenyewe.

Post a Comment