DIAMOND AKANUSHA KUPEWA MILIONI 500 NA LOWASSA ILI AMPIGIE KAMPENI
Meneja wa msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Nasib Abdul ‘Diamond’, Babu Tale, amesema hawajawahi kupewa kiasi cha fedha Sh mil 500 na Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, ili wampigie kampeni za urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza
na Mpekuzi, Babu Tale alisema watakuwa wehu kukataa fedha nyingi kiasi
hicho wakati wenyewe wanafanya muziki ili kupata fedha, lakini ukweli ni
kwamba hawajapewa kitu chochote.
Alisema hata hivyo Diamond yupo tayari kumfanyia kampeni mgombea yeyote atakayetangazwa kuiwakilisha CCM.
“Kama
kweli tungekataa fedha hizo hata Mwenyezi Mungu angetulaani, ila
naamini taarifa hizo zitakuwa zinasambazwa na wapinzani wa kisiasa wa
kiongozi huyo kwa lengo la kumchafua, hajawahi kutupa ofa hiyo,”alisema Babu Tale.
Meneja
huyo alitoa ufafanuzi huo baada ya hivi karibuni kuzagaa kwa taarifa
ambazo si za kweli, kwamba walipokea kiasi hicho ili kumpigia kampeni
Lowassa

Post a Comment