WATANO WAUAWA KATIKA MAPIGANO NA POLISI NIGER KISA KIBONZO
Nchini Niger watu watano wameripotiwa kuuawa katika maandamano ya
kulaani kibonzo cha kumvunjia heshima Mtukufu Mtume Muhammad SAW kati ya
polisi na waandamanaji katika mji mkuu Niamey.
Hayo yamethibitishwa na Rais Mahamadou Issoufou wa nchi hiyo ambapo mbali na kukiri kutokea mauaji hayo, amewataka pia wananchi kuwa watulivu.
Kwa mujibu wa Rais Mahamadou miongoni mwa wahanga wa mauaji hayo, waliuawa katika vurugu zilizoibuka siku ya Ijumaa kati ya polisi na waandamanaji waliokuwa wakiandamana kulaani kitendo cha jarida la Ufaransa la Charlie Hebdo kuchapisha tena picha za vikatuni vinavyomvunjia heshima Mtume Mtukufu wa Uislamu SAW katika mji wa Zinder.
Inaarifiwa kuwa, polisi walitumia nguvu kupindukia dhidi ya waandamanaji hao ikiwemo kuwafyatulia gesi za kutoa machozi, hali iliyopelekea waandamanaji kupoteza fahamu na wengine kufariki dunia. Kufuatia hali hiyo, jana Jumamosi Waislamu wenye hasira kali walimiminika mabarabarani mjini Niamey, na kuchoma moto makanisa manane ya mji huo. Habari zinadokeza kuwa, awali maandamano hayo ya siku ya Ijumaa yalikuwa ya amani kabla ya polisi kuwashambulia waandamanaji.

Post a Comment