ad

ad

SIMBA KUIVAA MTIBWA FAINALI MAPINDUZI CUP



KIKOSI CHA SIMBA KILICHOTINGA FAINALI YA KOMBE LA MAPINDUZI KWA KUIFUNGA POLISI ZANZIBAR KWA BAO 1-0 LEO NDIYO HIKI HAPA.

KINAONEKANA KUWA KIKOSI KINACHOJUMLISHA VIJANA WENGI ZAIDI NA SASA KITAPIGA FAINALI JUMATATU DHIDI YA MTIBWA SUGAR.




Vinara wa Ligi Kuu Bara, Mtibwa Sugar wameimeng’oa JKU na kutinga fainali ya Kombe la Mapinduzi.

Mtibwa imetinga fainali baada ya kulazimika kuingia kwenye changamoto ya mikwaju ya penalti baada ya kumaliza muda wa kawaida kwa sare ya bila kufungana.


Ushindi wa penalti 4-3 ndiyo ulioipeleka Mtibwa Sugar ambayo beki wake David Luhende pekee ndiye alipoteza mkwaju wake kwa kupiga nje.

Wachezaji wawili wa JKU nao walipaisha mikwaju yao na kumpa nafasi Vicent Barnabas kuwamaliza.
CREDIT:  SALEHJEMBE 

No comments

Powered by Blogger.