NILIISHI DUNIA YA PEKE YANGU - 13
ILIPOISHIA;
“Siyo kwamba nimechanganyikiwa bali siamini.”
“Basi amini mpenzi wangu.”
Baada ya kutulia alihesabu na kuzikuta zilezile milioni tatu na laki mbili.
“Zipo sawa.”

“Basi toa hizo tatu zingine utamalizia mambo mengine.”
Victor baada ya kutoa laki mbili, milioni tatu aliziweka kwenye mfuko kusubiri siku ya pili kwenda kununua gari letu. Maskini siku hiyo nilimuonea huruma Victor alikuwa na furaha ya ajabu alinikumbatia kwa furaha kwake ilikuwa kama muujiza fulani ambao hakuutegemea.
SASA ENDELEA...
Tulilala mpaka siku ya pili ambayo tulikutana na huyo Mwarabu Maheb.
Tulichanya mchakato wote wa mauziano uliokwenda vizuri na kukabidshiwa vitu vyote muhimu na kadi ya gari. Baada ya makabidhiano gari likawa letu rasimi. Japo ilikuwa na jila la mwenye gari lilikuwa langu lakini niliamini ile ni yetu. Victor alidizi kunishukuru kwa kumtoa kwenye kazi ya manyanyaso.
“Yaani siamini nashukuru sana mpenzi wangu kwa yote uliyonifanyia, sijakueleza ya moyoni lakini nilikuwa na mpango wa kuacha kazi kwani manyanyaso yalizidi. Leo hii na mimi naweza kusimama mbele za watu na kuonekana mtu. Nakuahidi kufanya kazi kwa nguvu zote ili isijutie uamuzi wako wa kununua gari.”
“Wala usifike huko mpenzi wangu, usitumie nguvu sana shida yangu si fedha bali uwe na uhuru na kazi yako, pia uifanye kazi bila wasiwasi.”
“Nimekuelewa, lakini chetu ndicho kinatakiwa tukihangaikie sana.”
“Nimekuelewa.”
Huo ndio ukawa mwanzo mpya wa maisha yaliyojaa furaha na faraja kwangu na Victor, nami biashara zangu zilitoka mtoto wa kike kwa muda mfupi nilinenepa na kupendeza machoni mwa watu. Mpenzi wangu naye alifanya kazi kwa bidii iliyoonesha matunda kila wiki tuliweka fedha zaidi ya ile aliyokuwa akipeleka kwa tajiri yake.
Ndani ya miezi sita toka tununue gari tuweza kununua kiwanja maeneo ya Tabata Segerea na kukusanya nguvu za ujenzi. Wakati huo niliona ule ndiyo ulikuwa muda mzuri wa mimi kutafuta mtoto baada ya kuridhika na muda nilioamua kupumzika.
Kwa vile hali yetu ya maisha ilikuwa imeimalika kwa kipato kuongezeka tulifunga ndoa na kuwa mke na mume, baada ya ndoa ilichukua miezi miwili kushika mimba. Ilikuwa kama inasubiri ndoa kwani nilikuwa nimekwisha kubali kubemba mimba hata bila ya ndoa.
Siku zilikatika mambo yenu nayo yalizidi kutunyookea nami nilizidi kumshukuru Mungu ujauzito wangu uliendelea vizuri. Muda ulipotimu nilijifungua salama mtoto wa kike ambaye nilimpa jina la mama yangu mzazi Fatuma kama kumbukumbu yake. Kila mmoja alishangaa mimi mkristo kumwita mwanangu jina la fatuma. Niliwaeleza jina si dini kila mmoja alinielewa.
Siku zilikatika maisha nayo yalitunyookea duka nalo lilizidi kupanuka na kuweza kuajili wasichana wawili ambao walifanya kazi vizuri ya kuuza duka kipindi chote nilipokuwa nikimlea mwanangu. Mume wangu baada ya kukusanya fedha ambayo nilichanganya na yangu kidogo kwa ajili ya kuanza ujenzi.
Fedha ilikuwa kama milioni nne na nusu ambazo tulipanga kuanzia kunyanyua nyumba, siku mbili kabla ya kuanza mchakato baada ya wapimaji kupima kiwanja na kutueleza mpaka nyumba kusimama ilitakiwa milioni kumi na tano. Kwa vile kwa mwezi tulikuwa na uhakika wa kuingiza zaidi ya laki nne mpaka tano tuliamini nyumba ingesimama taratibu.
Usiku wa kuamkia siku tuliyopanga kuanza ujenzi mume wangu alipigiwa simu kuwa kuna gari zuri linauzwa kwa bei ya kutupa ya milioni tatu na laki mbili. Taarifa zile kidogo zilimchanganya Tony na kumuona kuna kitu ninahitaji kumsaidia.
“Vipi mpenzi mbona kama habari hizi zimekushtua?” nilimuuliza kwa sauti ya upole.
“Ni kweli.”
“Kwa nini?”
“Isingekuwa tumekubaliana kujenga nyumba tungelinunua, nina imani tukiwa na gari mbili ndani ya miezi sita nyumba itanyanyuka bila kuchukua fedha za dukani.”
“Siku zote huwa sipendi kukuona ukiumia kwa jambo linalowezekana kutatulika.”
“Sawa, lakini sipendi kila jambo niamue mimi.”
“Ndiyo sababu ya kuwa baba wa familia, nina imani kila ukifanyacho kina faida yake.”
“Kama ni hivyo basi tulinunue hilo gari litatuongezea kipato.”
Siku ya pili tuliongeza teksi ya pili, mume wangu kama kawaida alimtafuta dereva mzuri tena mwenye bidii ya kazi. Miezi mitatu ya kwanza tulianza kujenzi wa nyumba yetu. Niliamini duniani hakuna mwembamba mume wangu alinenepa na kuwa na kitambi alionekana kweli mtu mwenye fedha.
Maisha yangu yalivyobadilika sikuamini na mimi nitakuwa mtu wa kufanyiwa kazi hata kuwalipa watu mshahara. Niliamini siri ya maisha aijuae Mungu peke yake, kutokana na mateso niliyopata mwanzo wa maisha yangu niliamini kabisa nilikuwa nikiishi dunia ya peke yangu lakini kumbe penye matatizo makubwa mbele kuna faraja kubwa.
Miezi sita toka tununue gari jingine ujenzi wa nyumba ya vyumba vya kulala sita, viwili vya watoto masta bed, jiko mabafu mawili ya ndani sehemu ya kulia pamoja na sebule kubwa ilikuwa imefikia kwenye madirisha na kujipanga kwa ajili ya lenta ambayo ilihitaji fedha nyingi kidogo.
Niliamini kutokana na biashara ya gari kwenda vizuri na kuengeza akiba yangu iliyokuwa kama milioni na nusu iliyobaki baada ya kununua vitu vyote muhimu vya dukani vilivyogharimu milioni zaidi ya tano. Mwanangu Fatuma naye aliendelea vizuri katika afya njema.
Siku moja nikiwa dukani nilipigiwa simu na dereva wetu aliyekuwa akiendesha teksi ya pili, baada ya kupokea simu upande wa pili
“Haloo shem.”
“Vipi Jimmy?”
“Umepata taarifa zozote za Tony?”
“Taarifa za nini?” Nilishtuka.
“Nimepigiwa simu kuwa Tony amechanganyikiwa.”
“Eti, amefanya nini?” Nilishtuka kusikia vile.
“Nasikia Tony amechanganyikiwa, kaliacha gari kwenye mataa na kusimama pembeni akihubiri dini.”
“Mbona sikuelewi, Tony anafanya nini?” habari zile zilinichanganya sana.
“Amekutwa anahubiri dini.”
“Jimmy acha utani,” nilijua Jimmy ananitania.”
“Kweli shem.”
“Wewe uko wapi?”
“Ndiyo nakaribia eneo la tukio.”
“Hebu kwanza muone, ameanza lini tena kuwa mlokole wa kutangaza dini!”
“Sawa shem, nitakujulisha.”
Kutokana na kuchanganyikiwa nilitoka dukani na kumsahau mwanangu, nilikodi teksi kwenda Ubungo ili nikamuone mume wangu ambaye nilielezwa kuwa amechanganyikiwa.
Nikiwa njiani nilimpigia simu Jimmy, baada ya kupokea nilimuuliza.
“Vipi Jimmy, Tony yupo kwenye hali gani?”
“Shem inaonekana kama malaria imempanda kichwani, sasa hivi tunamkimbiza Hospitali ya Amana.”
“Nami nipo njiani basi nakuja hukohuko,” nilimueleza dereva ageuze gari kuelekea Amana, bahati nzuri nilikuwa nimefika Buguruni Kwa Ali Hamza, tuligeuza gari.
Ilikuwa kama bahati baada ya teksi niliyoikodi kufika tu na gari alilokuwemo mume wangu nalo liliwasili hospitalini hapo.
Ajabu Tony hakuonesha kuchanganyikiwa, alikuwa katika hali ya kawaida lakini mkononi alikuwa na Biblia ambayo ilionekana kuwa mpya. Aliponiona alipaza sauti.”
“Ester mke wangu.”
“Abee, mume wangu.”
“Mke wangu dunia inaangamia, hasira za Mungu ni kubwa.”
“Kwa nini tena Mume wangu?”
“Mke wangu roho mtakatifu aliniagiza ninunue Biblia ili nihubiri Injili, baada ya kununua niliiweka ndani ya gari na kutembea nayo. Kumbe Mungu hakufurahishwa mimi kutembelea gari. Wakati naendesha kila kitu kilikuwa cha moto kasoro hii Biblia.
“Kama nisingetoka haraka ndani ya gari lingewaka moto.”
Maneno ya mume wangu yalinichanganya, kwani hata siku moja sikuwahi kumuona akijikita katika dini kiasi cha kusahau hata kanisa.
Siku ile nilimshangaa kusema maneno yale ambayo hata mlokole asingeyasema vile.
“Mume wangu upo sawa?” nilimuuliza nikiwa nimemkazia macho.
“Nipo sawa mke wangu, japokuwa wananilazimisha kwa kusema eti nimechanganyikiwa, mke wangu wote mnatakiwa kumrudia Mungu. Muda wowote anaweza kuiangamiza dunia.”
“Mume wangu mbona sikuelewi?’
“Huwezi...huwezi kunielewa mke wangu, shetani kakuzunguka mke wangu, hutaona milele bila ya kupokea wokovu,” mume wangu alisema huku akitiririkwa machozi.
Nilizidi kuchanganyikiwa, kwa kila aliyekuwa akimfahamu mume wangu aliamini kuwa amechanganyikiwa.
“Sasa shemeji mna mpango gani?” nilimuuliza Jimmy.
“Haya shemeji ni malaria tu, atatulia muda si mrefu akipata tiba,” Jimmy alimwambia shemeji yake.
“Jamani siumwi, nimewaeleza muda mrefu natakiwa kueneza Injili kwa mataifa.”
Wakati huo rafiki yake mmoja alikuwa ameshaandikisha cheti na tukaongozana naye hadi kwa daktari baada ya kupewa upendeleo maalum.
Baada ya kuingia kwa daktari tukiwa watu zaidi ya watano, daktari alituomba tubakie wachache. Kwa vile Jimmy ndiye aliyenipa taarifa nilibaki naye.
“Ndiyo jamani, mheshimiwa ana matatizo gani?” Daktari alituuliza.
“Sina tatizo lolote, Injili itamfikia kila mwenye sikio, hata wewe unatakiwa kuokoka, acheni kutoa mimba za wanawake, kumbukeni adhabu ya Mungu ni kali kwenu.”
“Mume wangu hebu nyamaza basi.”
“Ninyamaze kwani mimi ni mfu?”
“Hapana, msikilize daktari.”
“Haya namsikiliza,” mume wangu alisema huku akifumbata mikono juu ya mapaja yake.
“Mmh! Ipo shughuli,” daktari alisema huku akitikisa kichwa kisha aliuliza swali la awali.
“Nilipigiwa simu kuwa ndugu yangu amechanganyikiwa na ameliacha gari kwenye taa za kuongozea magari pale Ubungo. Nilipomkuta kwa kweli nilishtuka, amekuwa mlokole na Biblia mkononi.”
“Mnataka kuniambia hali hii ndiyo leo imemtokea?”
“Ndiyo,” nilijibu.
Nini kiliendelea? Je, Tony atakuwa chizi? Usikose kusoma katika Gazeti la Risasi Jumamosi.
Antony Joseph,” alijibu vizuri.
“Ushawahi kuumwa hivi karibuni?”
“Dokta nikueleze mara ngapi siumwi na sitaumwa milele, roho mtakatifu yumo ndani yangu.”
“Mpelekeni akapime maralia na majibu mniletee.”
Tuliondoka na mume wangu hadi maabara na kupima, baadaye tulirudisha majibu kwa daktari. Majibu yalinichanganya baada ya kuonekana kwamba mume wangu hana maralia. Nilijiuliza itakuwa nini, kwa vile alikuwa akiongea sana mambo ya kilokole doktari alimchoma sindano ya usingizi na kumpa mapumziko ya muda.
“Dokta itakuwa malaria imempanda kichwani tu,” Jimmy alichangia.
“Samahani ndugu yangu unaitwa nani?” daktari alimuuliza mume wangu.
“Victor Joseph,” alijibu vizuri.
“Ulishawahi kuumwa hivi karibuni?”
“Dokta nikueleze mara ngapi siumwi na sitaumwa milele, roho mtakatifu yumo ndani yangu.”
“Mpelekeni akapime malaria na majibu mniletee.”
Tuliondoka na mume wangu hadi maabara na kupima, baada ya kupima tulirudisha majibu. Majibu yalinichanganya baada ya mume wangu kukutwa hana malaria. Nilijiuliza ile itakuwa nini, kwa vile alikuwa akiongea sana mambo ya kilokole, dokta alimchoma sindano ya usingizi na kupewa mapumziko ya muda.
Saa moja usiku, mume wangu alipewa ruhusa, aliponiona alionesha kushtuka:
“Mke wangu!”
“Mume wangu.”
“Mbona hivi?”
“Kwani hujui kilichokuleta hapa?”
“Hata sijui.”
“Kweli?” nilimuuliza kwa kumshangaa.
“Kweli, kwani nilipatwa na nini?”
“Ulikutwa ukihubiri Injili maeneo ya Ubungo.”
“Mimi?” mume wangu alishtuka.
Kauli yake ilinishtua na kujiuliza kitu gani kilichomtokea mume wangu, kama angekutwa na malaria ningejua labda ilimpanda kichwani.
“Tena ulikuwa umejaza watu wakikushangaa ukitangaza Injili kwa uwezo mkubwa,” Jimmy alisema.
Tuliingia ndani ya gari ili turudi nyumbani ikionesha kabisa yaliyomtokea asubuhi ameyasahau. Mume wangu alikuwa tofauti na mchana, hata yale maneno yake ya kutangaza Injili hakuyasema. Kingine kilichonishangaza ni kusahau hata Biblia aliyokuja nayo. Tuliibeba na kurudi nayo nyumbani, tukiwa tunarudi mume wangu aliniuliza:
“Unasema nilikuwa nafanya nini Ubungo?” alionesha kushangaa.
“Unatangaza Injili, nashangaa hujauliza hata Biblia yako,” nilimjibu.
“Mmh!” Mume wangu aliguna na kutulia akivuta kumbukumbu kisha alisema:
“Kweli nimekumbuka.”
“Umekumbuka nini?” nilimuuliza.
“Tangu juzi kuna kitu sikielewi.”
“Kitu gani?”
“Kama kuna nguvu fulani ambazo sizielewi zinanituma nitangaze Injili, jana nilinunua Biblia na kuiweka kwenye gari. Leo nilipokaribia mataa ya Ubungo kuna sauti ilikuwa ikinifukuza kwenye gari eti niteremke nikatangaze Injili. Ndipo nilipoliona gari kama likitaka kuwaka moto, nilitoka na kuliacha, baada ya hapo sielewi mpaka nilipojikuta hapa.”
“Huna malaria?” Jimmy alimuuliza.
“Si umesikia sina ugonjwa wowote.”
“Sasa ni nini?” niliuliza.
“Hata sijui, yaani nashangaa.” Victor alijibu.
“Au watu wameanza?” Jimmy alisema.
“Waanze nini?” Victor aliuliza.
“Kutia mkono, si unajua kwenye neema hapakosi fitina?”
“Mmh! Jamani mawazo gani hayo, mimi nafikiri ni tatizo dogo, la muhimu tumrudie Mungu. Inaonesha jinsi gani tulivyomhasi Mungu, Victor una muda gani hujaingia kanisani au kushika Biblia?” nilimuuliza mume wangu.
“Mmh! Mwaka wa pili sasa.”
“Basi leo ulikuwa mchungaji ukihubiri neno la Mungu tena kwa ufasaha mkubwa,” Jimmy alisema.
“Sasa hiyo imaanisha nini?” Victor aliuliza.
“Haimaanishi kitu zaidi ya kumrejea Mungu na Jumapili lazima uende kanisani,” nilitoa mawazo, pamoja na kuwa na wasiwasi wa labda mume wangu alikuwa amechanganyikiwa, lakini maneno aliyosema kuhusu wanadamu kumrudia Mungu, niliamini kabisa ile haikuwa kuchanganyikiwa bali kukumbushwa kutokana na kumsahau.
Hata mimi uvivu wa Victor ulinifanya nilione kanisa kama kituo cha polisi na kibaka.
“Sawa nitaenda lakini mimi Roma na ulokole wapi na wapi?” Victor alihoji.
“Itabidi uokoke,” nilimwambia.
“Hata siku moja,” Victor alikataa, katika vitu ambavyo alikuwa hakubaliani navyo ni kusikia walokole wanaponya, siku zote aliwaona waongo na wazushi. Lakini jirani yangu mwanaye aliyekuwa na matatizo ya majini tangu alipokwenda kwenye moja ya makanisa ya maombi, hali yake ilitulia.
Lakini wengine walikwenda miaka nenda rudi na hawakupata nafuu yoyote na kuishia kubadili makanisa. Niliamini huenda ni imani yao kuwa ndogo iliyowafanya wasipokee uponyaji ambao uliegemea sana kwenye imani.
Mazungumzo yalitufanya tufike nyumbani bila kujua, tuliingia ndani, Victor alisema amechoka sana hivyo alikuwa akiomba kupumzika.
Siku ya pili mume wangu aliamka katika hali ya kawaida, hakuonesha kitu chochote zaidi ya uchovu wa mwili kama alikuwa na malaria. Kwa vile gari lilikuwa limechukuliwa na polisi wa usalama barabarani, tulimtuma Jimmy kulifuata polisi pamoja na faini ya kuliacha gari barabarani.
Alipofika alilikuta lipo kwenye hali nzuri hata simu na vitu vyake vilikuwa katika hali nzuri. Alilirudisha gari nyumbani na yeye kuendelea na kazi yake, siku ile nilishinda na mume wangu sikwenda kwenye biashara zangu mpaka usiku.
Nini kitaendelea? Kuyajua yote tukutane wiki ijayo jumatatu
Mtunzi: Ally Mbetu
Like: www.facebook.com/2jiachie
Web: www.2jiachie.com
Post a Comment