MKALI WA YouTube GLOZELL LYNETTE ALIVYOPAGAWA KUMFANYIA MAHOJIANO RAIS OBAMA!
GloZell Lynette Simon akiwa katika moja ya kazi zake zilizopo mtandaoni.
GloZell baada ya kupata taarifa za kumfanyia mahojiano Rais Obama.
MKALI wa You Tube na Mchekeshaji Maarufu (Comedian), GloZell Lynette Simon, hivi karibuni alipagawa baada ya kuambiwa kuwa atamfanyia mahojiano Rais wa Marekani, Barrack Obama.GloZell ambaye ni raia wa Marekani mwenye umri wa miaka 52, amejipatia umaarufu sana kupitia kazi zake za muziki, Vichekesho na video zake kwenye mtandao wa You Tube ambazo zinaangaliwa sana.
Agosti mwaka jana, chaneli hiyo ilikuwa tayari na wanachama zaidi ya milioni tatu na zaidi ya watazamaji milioni 500. Ndani ya mwezi huo, video zake sita kila moja ilikuwa imetazamwa zaidi ya mara milioni 10 kila moja. Mojawapo ya video hizo ni "My Push up Bra will help me get my man" (iliyokuwa na watazamaji milioni 23).
GloZell akimfanyia mahojiano Rais Obama.
Mwezi huu, GloZell amemfanyia mahojiano Rais Obama kupitia 'livestream' ya You Tube, mahojiano yaliyofanyika Ikulu ya White House, Marekani.
Post a Comment