ad

ad

MJANE WA GURUMO AWASHUKURU NSSF


SIKU chache baada ya mjane wa marehemu, Muhidin Gurumo, Pili Nassoro, kukabidhiwa shilingi milioni mbili na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa ajili ya kununua bajaj, amelishukuru kwa kujitoa kwao.


Mjane wa marehemu, Muhidin Gurumo, Pili Nassoro.

Akizungumza na Amani, Pili alilisifu shirika hilo kwa kuthamini michango ya wanamuziki.

“Nawashukuru NSSF kwa kunitoa kwenye mawazo kwani mchango wao ni mkubwa sana kwangu pia nawapongeza kwa kuutambua mchango wa wanamuziki,” alisema Pili.


Pili Nassoro akipokea hundi ya milioni mbili kutoka NSSF.

Jumanne ya wiki hii, mjane wa Gurumo alikabidhiwa shilingi milioni mbili na shirika hilo ambapo makabidhiano hayo yalifanyika katika Ukumbi wa NSSF, Jengo la Mkapa Tower.Marehemu Gurumo alifariki Aprili 13, mwaka jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na kuzikwa kijijini kwao Kisarawe mkoani Pwani.

No comments

Powered by Blogger.