ad

ad

DIAMOND AGAWA FEDHA, ALIKIBA AFANYA VIOJA

USIKU wa kuamkia juzi tamasha la Kiboko Yao lililofanyika katika Viwanja vya Leaders Club na kuacha historia kwa mashabiki na wasanii wa muziki nchini.

Tamasha hilo liliandaliwa na Kampuni ya Mawasiliano ya Tigo Tanzania kwa kushirikiana na Deezer, ambayo ni huduma ya kimataifa inayorusha muziki, itakayowapa Watanzania muziki usiokuwa na kikomo.

Pia, itawapa nafasi wasanii wa hapa nchini kujiongezea kipato kutokana na nyimbo zao ambazo zitakuwa zimesikilizwa kupitia huduma hii.

Wasanii watapewa mafunzo ya jinsi ya kutumia na kunufaika na huduma hiyo.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Fenella Mukangala akihutubia maelfu ya mashabiki kabla ya kuanza kwa tamasha hilo, aliyasihi makampuni ya mawasiliano kuwatendea haki wasanii katika ushirikiano wa kikazi baina yao ikiwamo kuwalipa kiwango kinachostahili katika miito ya simu.

“Ni matumaini yangu uzinduzi huu utawanufaisha wasanii wetu, pamoja na kuiingizia serikali mapato yatakayotokana na biashara baina yenu na wasanii hawa. Mna kila sababu kuhakikisha kwamba huduma hii inawanufaisha wanamuziki wetu moja kwa moja,” alisema Mukangara wakati wa uzinduzi huo.

Awali wanamuziki wa Mashauzi Classic, Malaika Band na wengineo walilishambulia jukwaa, kabla ya kuwapisha viongozi mbalimbali kutoa nasaha zao na kuzindua rasmi promosheni hiyo.

Tamasha laanza rasmi

DJ Mafuvu ndiye aliyepanda jukwaani na kuanza kupasha kabla ya washereheshaji wawili Sam Misago na Dullah hawajapanda na nyimbo mbalimbali za wasanii wa zamani ambazo ziliwaamsha mashabiki. ‘Naja’ wimbo ulioimbwa na Juma Nature ndiyo uliozidi kuwavutia mashabiki na kuamsha shangwe na vifijo.

Ya Moto Band walipanda jukwaani na kuonyesha umahiri wao katika kuimba, huku wakitambulisha wimbo wao mpya ‘Nitakupwelepweta’ kabla ya kuwapisha wasanii wengine akiwamo Shaa, Linah, Ben Pol, Stamina, Young Killer, Fid Q, Profesa Jay, Vanessa Mdee, Mwana FA & AY, Barnabas, Shilole, Weusi na wengineo wengi.

Ben Pol ni kati ya wasanii waliofanya mabadiliko makubwa katika kuonyesha uwezo wake jukwaani, baada ya kupanda na madansa wawili ‘Wazungu’ ambao walicheza vilivyo wakati akitumbuiza wimbo wake mpya ‘Sophia’.

Kwa upande wa Vanessa Mdee, kama kawaida yake alifanya shoo ya aina yake, lakini alionekana kuzidiwa baada ya sauti yake kushindwa kutoka ipasavyo, baada ya kujituma kwa kucheza alipokuwa jukwaani.
Mpambano Mkali

Wasanii waliokuwa wakisubiriwa ni Diamond Platnumz na Ali Kiba ambao hata hivyo ratiba zao za kupanda jukwaani zilikuwa mwishoni.

Ali Kiba alianza kutumbuiza kupitia wimbo wake wa zamani uliomtambulisha katika muziki mwaka 2007, ‘Cinderela’ na baadaye aliachia nyimbo nyingi alizowahi kutamba nazo.

Wakati wote huo shangwe na vifijo vilisikika kutoka kwa mashabiki, ambao wengi wao walikuwa wamevalia fulana zenye jina la ‘Team Kiba’.

Wakati wote wa shoo yake, kulikuwa na utulivu ambapo mashabiki waliongozwa na msanii huyo kuimba nyimbo zake zilizowahi kutamba.

Diamond Platnumz alipokea jukwaa baada ya Ali Kiba kushuka, alifanya shoo nzuri zaidi na pindi alipoanza kuimba, kuna baadhi ya mashabiki walianza kutupa chupa jukwaani zilizoaminika kwamba zilikuwa na mikojo, sambamba na mawe.

Nyota huyo hakujali na aliendelea kushusha burudani hadi mashabiki hao walipotulia. Diamond aliona isiwe shida, akaamua kuanza kufungua maburungutu ya fedha na kuzirusha kwa mashabiki noti za Sh2,000 ambapo walizipokea kwa mikono miwili na kuanza kumshangilia na walisahau walichokifanya awali.

Baadhi ya mashabiki waliovalia fulana za ‘Team Kiba’ walionekana wakizigombea fedha hizo na baadaye waliendelea kumshangilia Diamond ambaye aliendelea kushambulia jukwaa.

Vimbwanga

Katika hali isiyo ya kawaida msanii Ali Kiba aliingia uwanjani kwa staili ya aina yake. Yeye aliamua kuruka ukuta badala ya kutumia mlango wa kawaida. Hiyo ilikuwa ni majira ya saa 05:37 usiku.

Licha ya kuwepo kwa milango miwili ya kuingilia upande wa VIP, watu waliokuwa nyuma ya jukwaa walishituka kuona Kiba akiingia kwa staili hiyo hali iliyowashangaza wasanii wenzake na watu waliokuwa wakifanya shughuli mbalimbali nyuma ya jukwaa hilo.

Kilichowashangaza wakongwe wa muziki ni Ali Kiba kuwapita bila kuwasalimia, ambapo wasanii kadhaa walilalamika kitendo cha yeye kushindwa kuwasalimia wenzake. Licha ya kufanya shoo nzuri, Ali Kiba bado amewaachia maswali mengi wasanii wenzake.

No comments

Powered by Blogger.