ASHA BARAKA, ALI CHOKI SASA 'NO BEEF'
Choki na Asha wakiwa katika pozi na Mhariri Mtendaji wa Global Publishers Richard Manyota (wa pili kulia) aliyefanikisha kumalizika kwa bifu hilo. Kushoto ni Mhariri wa Gazeti la Ijumaa Wikienda Sifael Paul.
Ali Choki na Asha Baraka wakiwa ndani ya studio za Global TV Online leo wakati wa kumaliza bifu lao.
Choki na Asha wakiwa katika picha ya pamoja na Manyota (wa pili kulia). Kushoto ni Mhariri Kiongozi wa Magazeti ya Championi Saleh Ally.
Juhudi za kuwapatanisha wakongwe hao katika muziki wa dansi zimefanywa na baadhi ya viongozi wa Global Publishers ambap wanakiri kuwa halikuwa jambo rahisi kuwapatanisha viongozi hao.
Wakongwe hao katika muziki wa dansi wameamua kumaliza tofauti zao na kuwa kitu kimoja huku wakiahidi kushirikiana katika muziki na mambo mengine.
Mbali na mengi yaliyoongea pia wamekubaliana kufanya onyesho la pamoja huko mbeleni kuwadhihirishia mashabiki kuwa kwa sasa hawana bifu lolote na wamekuwa kama ilivyokuwa awali.
Mtandao huu unawapongeza na kuwatakia kila la kheri viongozi hao kwa uamuzi sahii waliouchukua ili kuzidi kusukuma gurudumu la muziki wa dansi.
(PICHA NA GPL)
Post a Comment