ad

ad

TAMBWE: NITAFUNGA ILI KUWAONYESHA SIMBA

 

Mshambuliaji mpya wa Yanga, Amissi Tambwe akisoma gazeti la Championi.

Na Mwandishi Wetu
MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga, Amissi Tambwe amesema atafanya juhudi afunge bao au mabao watakapokutana na Simba.Tambwe amejiunga na Yanga kwa mkataba wa mwaka mmoja ikiwa ni saa chache baada ya kutemwa na Simba.

Akizungumza na Championi Jumatano, Tambwe alisema atahakikisha anafunga ili kuwaonyesha Simba yuko kazini kweli.“Kweli watu wa Simba waliniunga mkono, lakini ninapokutana nao nitajitahidi kufunga ili kuondoa hisia zozote mbaya zilizopo. Yanga ndiyo sehemu yangu mpya ya kazi, lazima niipende na kuiheshimu,” alisema Tambwe ambaye ni mtaratibu.

Tambwe amekabidhiwa jezi namba 19 badala ya 17 aliyokuwa akiitumia Simba.
Hii ina maana kuwa mchezaji huyo amepewa jezi yenye namba sawa na idadi ya mabao yake aliyofunga msimu uliopita akiwa Simba na kuibuka mfungaji bora.

Tambwe amejiunga na Yanga kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea Simba ambayo ilitangaza kumuacha ili impe nafasi Simon Sserunkuma.Msimu uliopita, Tambwe alifunga mabao 19 na kuibuka mfungaji bora wa Ligi kuu Bara ukiwa ndiyo msimu wake wa kwanza kuichezea Simba.

Raia huyo wa Burundi alikuwa anavaa jezi namba 17 ambayo Yanga inavaliwa na Mrisho Ngassa.
“Walinipa jezi namba 19 na 20 nichague, nimeona namba 19 ndiyo itakuwa nzuri kwangu,” alisema Tambwe.

Yanga imempa shilingi milioni 78 ikiwa fedha za usajili shilingi milioni 34 pamoja na mshahara wa dola 2000 (milioni 3.4) kwa mwezi, ikiwa ni mara mbili zaidi ya ule aliokuwa akilipwa Simba, hivyo kwa mwaka mmoja staa huyo wa Burundi atakuwa akiingiza kitita hicho cha fedha.


(CREDIT: GAZETI LA CHAMPIONI)

No comments

Powered by Blogger.