ad

ad

SIMBA YA AVEVA YAANZA UJENZI WA UWANJA BUNJU, DAR



Rais wa SImba SC, Evans Aveva akizungumza na Waandishi wa Habari leo Msimbazi

KLABU ya Simba imeingia mkataba na kampuni ya uchoraji ramani ya Envirolink ili iweze kuwapatia michoro ya hosteli na namna ya kuendeleza mradi wa Bunju ambao utaigharimu Simba zaidi ya Sh 2.5 bilioni hadi kukamilika kwake.

Rais wa Simba, Evans Aveva amesema kuwa kampuni ya Envirolink tayari imewakwisha wasilisha  michoro ya mradi huo na kuwa matarajio ni kuwa shughuli hiyo itaanza mapema iwezekanavyo.

Ni imani yetu kuwa wazee wetu waliweza kujenga kwa nguvu zao wenyewe makao makuu yetu pale Msimbazi, Kariakoo jijini Dar es Salaam, na sisi hatuna shaka kizazi hiki kitajenga mradi huu wa Bunju," alisema Aveva.

Rais Aveva amesema kuwa muendeno wa timu ya Simba hadi sasa haaendani na hadhi ya klabu hiyo na hivyo wamefanya mabadiliko mengi baada ya kugundua matatizo.
Aveva alisema, " Tuligundua kuwa sababu zilizokuwa zikituangusha ni uwepo wa timu changa, ugeni wa kocha Patrick Phiri  lakini pia ugeni wa viongozi wengi kwenye soka.

"Nafasi tuliopo haiendani na hadhi, uzoefu na ukongwe wetu kwenye ligi lakini sasa naamini kuna mengi yanafanyika ikiwemo kumpa kocha nafasi ya kufanya baadhi ya mabadiliko yakiwemo kwenye usajili," alisema.

No comments

Powered by Blogger.