ad

ad

JINI LA DARAJA LA SALENDA - 16




Like: www.facebook.com/2jiachie
Web: www.2jiachie.com
#SOMA SEHEMU ZILIZOPITA ZA SIMULIZI HII HAPA ==>http://bit.ly/


ILIPOISHIA: Alifuta machozi na kwenda hadi mlangoni na kuufungua, alikutana na kijana mtanashati aliyekuwa ameshika mkabrasha.

“Karibu,” Muddy alisema huku akionesha dalili za kumkaribisha mgeni yule.
“Ahsante, siingii ndani natokea Mahakama ya Mwanzo, kuna barua ya madai kutoka kwa aliyekuwa mkeo.”
“Nimefanya nini?”

“Inavyoonekana mkeo anadai, anataka mgawane mali baada ya kuachana,” alisema huku akitoa barua na kumkabidhi.
“Mungu wangu, pamoja na kunifilisi sasa ananimaliza kabisa,” Muddy
alisema huku akiangua kilio na kusahau yote aliyoelezwa na Balkis.

Baada ya jamaa kuondoka, Muddy aliingia ndani na kuifungua barua,
yalikuwa yale yale aliyoelezwa na Balkis, kwamba mkewe alikuwa akitaka
wagawane nyumba na gari. Nguvu zilimuishia na kujikuta akiinama kwenye
meza na kuanza kulia.
Hakukuwa na suluhu yoyote mbele yake zaidi ya kwenda jikoni kuchukua kisu ili ajitoe uhai wake SASA ENDELEA...

LAKINI likatokea jambo la ajabu, Muddy kila alipokuwa akikitafuta kisu hakukiona. Alihangaika nyumba nzima, hakukiona. Wazo lingine lilikuwa ni kutafuta kamba ili ajinyonge, vile vile alishangaa kuikosa kamba hata ile aliyotaka kujinyongea usiku na kuiacha kwenye gari, alipoifuata pia hakuikuta.

Hakurudi ndani, alikwenda dukani na kuchukua sumu ya panya, aliichanganya katika chupa ya maji ya kunywa kisha akanywa yote na kwenda kulala akisubiri malaika wa kifo amchukue.
***
Ashura mke wa Muddy alikuwa mwenye furaha, yeye pamoja na mwanaume wake walikuwa wakipongezana kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kumfilisi Muddy.
“Nina imani kazi imekwenda vizuri,” mwanaume huyo alisema.

“Ni kweli, lakini pamoja na kuyafanya yote bado namuonea huruma Muddy. Kwa nini tusimuachie gari na nyumba?” Ashura alisema katika hali ya kumuonea huruma Muddy.
“Tukiwa na huruma hatuwezi kuifanya kazi hii, ona leo tulivyo na utajiri wa kutisha.”
“Mmh! Kweli.”

Wakati Ashura na mwanaume wake wakiwa katikati ya mazungumzo, mlango uligongwa. Wote walikaa kimya kusikiliza, mlango ulipogongwa tena mwanaume alinyanyuka na kwenda mlangoni. Alipoufungua alikutana uso kwa uso na Balkis, akamkaribisha.
“Karibu mrembo.”

“Ahsante sijui Ashura anakaa hapa?”
“Wewe nani?”
“Sasa kaka yangu badala ya kunijibu, unaniuliza mimi nani?”

“Eeh, si vibaya kukujua wewe ni nani kwa vile unayemuuliza ni mke wangu na wewe ni mgeni kwangu.”
“Mimi naitwa Balkis, ina maana Ashura ameshaachana na Muddy?” Balkis aliuliza swali la uongo.
“Hiyo haikuhusu, sema kilichokuleta.”
“Kilichonileta ni kuonana na Ashura.”
“Karibu ndani.”

Alimkaribisha sebuleni ambapo alimkuta Ashura amejilaza kwenye kochi. Ashura alimshangaa yule mgeni kutokana na uzuri wake wa ajabu, pia vito vya thamani alivyovaa mwilini mwake. Hata manukato yake yalikuwa mageni puani ambayo yaliifanya nyumba nzima kunukia.
“Habari Ashura?”

“Nzuri, umenijuaje?”
“Ina maana jina lako ni siri? Wanapaswa kulijua watu wachache?”
“Siyo kwamba ni siri  ila sikujui.”
“Huwezi kuwajua wote mdogo wangu.”
“Mh! Nikusaidie nini?”
“Nimetumwa na Muddy.”
“Muddy! Muddy ndiye nani?”
“Mumeo.”

“Mimi nina mwanaume anayeitwa Muddy?”
“Sasa unashangaa au unakataa? Ndoa yako na Muddy imevunjika lini wakati mpaka jana usiku majira ya saa sita mmenipita Daraja la Salenda mkiwa pamoja, leo hii unamkana?”
“Basi muda mfupi baada ya kutuona wewe ndipo tulipoachana.”
“Sasa nani kamuacha mwenzake?”
“Maswali gani hayo?”

“Ndiyo maana nipo hapa,” Balkis alisema kwa kujiamini.
“Wewe ni nani kwa Muddy?” Ashura alihamaki.
“Kabla sijakujibu nataka useme ukweli mbele ya mwanaume wako, upo tayari kurudiana na Muddy?”
“Sipo tayari.”

“Na ukirudiana naye tena?”
“Nitembee uchi.”
“Rudia.”
“Nitembee uchi.”
“Kaka umesikia?” Balkis alimgeukia mwanaume wa Ashura na kumuuliza.
“Umesikia?”

“Kuwa?”hi akirudiana na Muddy.”
“Basi ni hayo niliyofuata hapa.”
“Mbona umeniuliza hivyo?” Swali la Balkis lilimtisha Ashura.
“Si umeachana na Muddy?”

“Ndiyo, nirudiane naye kwa kitu gani alichonacho, tena muda si mrefu ataokota makopo.”
“Usiokote makopo wewe, tena kabla sijaondoka nawapeni onyo mchezo wenu wa kudhulumu mali za watu utawatokea puani,”
Balkis alimweleza Ashura ambaye bado alikuwa akimshangaa kwa maswali yake.

Nini kiliendelea? Fuatilia katika Gazeti la Risasi Jumamosi.
Vituko
ndani ya daladala
Abiria wawili ambao majina yao hayakujulikana, juzikati walitwangana makonde mazito baada ya mmoja wao kutoa nauli ya shilingi 200 badala ya 300.

Abiria wa kwanza alipanda daladala hiyo Buguruni akielekea Gongo la Mboto na wa pili Vigunguti.
Kondakta alipoanza kutoza nauli, abiria wa kwanza alitoa shilingi 200. Kitendo hicho kilionekana kumkera abiria wa pili kwa kumwambia kwa nini katoa nauli nusu.

Abiria hao walianza kuzozana na kondakta akaungana na kauli ya abiria wa pili ya kumtaka wa kwanza kutoa shilingi 300 na si 200.
Hali hiyo ilionekana kumkera abiria wa kwanza na kuamua kumrushia ngumi abiria wa pili. Kitendo cha abiria huyo kurusha konde kilisababisha timbwili kali kwa washkaji hao kuanza kutwangana kavukavu.

Mbaya zaidi abiria wa kwanza alikuwa amekaa kiti cha mbele na walipoanza kurushiana makonde mazito gari lilianza kuyumba na kusababisha abiri wengine kuanza kupiga kelele ya kumuomba dereva asimamishe gari.

“Dereva simamisha gari utatuua, tunakuomba sana tumeshinda salama tunataka tufike nyumbani tukiwa wazima, tafadhali,” alisikika abiria mmoja huku wengine wakimuomba Mungu awaepushe na balaa hilo.

Wakati abiria wakipiga kelele, daladala hilo ilikuwa mwendo mkali. “Jamani mnataka kutuua kwa sababu ya shilingi 100? Acheni kugombana nitampa konda,” jamaa mmoja alisikika akisema.
Gari liliposimama jamaa hao walishuka na kuanza kukunjana vema na abiria wengine wakaingia ndani ya gari na kumwambia dereva aendeshe.
Mabondi hao wasiotambuliwa na shirikisho la ngumi Bongo waliachwa kituoni hapo wakitifuana.
Muddy alishtuliwa katika usingizi mzito na sauti ya Balkis, aliposhtuka alijishangaa kujiona bado yupo hai hakufa kama alivyodhamilia.
“Muddy vipi?”
Muddy hakumjibu alimshangaa Balkis aliyekuwa ameshikilia barua mkononi.

“Muddy mbona unanuka sumu ya panya?”
Bado Muddy hakuwa najibu aliendelea kupepesa macho na kuitazama glasi aliyokunywa sumu ilikuwa juu ya sturi.
“Muddy kwa nini unataka kujiua?” Balkis alimuuliza akiwa ameshika glasi iliyokuwa na sumu.
“Umejuaje?”

“Muddy nikufundishe mara ngapi swali mwenzake jibu na si swali kwa swali.”
“Umeisoma hiyo barua?”
“Niisome ili iwe nini, haya nilikueleza tokea awali kwa nini hutaki kunielewa?”
“Samahani Balkis nimechanganyikiwa.”

“Nilikueleza toka awali hutakufa bali unaelekea kwenye wendawazimu na usiponisikiliza sasa hivi utaokota makopo.”
Muddy alishangaa jinsi Balkis mwanamke mrembo mara kumi Ashura ameonesha mapenzi ya kweli kwake. Kingine kilikuwa uelewa wa ajabu wa Balkis kuonekana kumfahamu vizuri yeye na Ashura bila kuhadithiwa na mtu.

Hatua ya kupelekwa mahakamani ili wakagawane vitu pia deni la mkewe lililokuwa likizaa liba kila kukicha lilizidi kumchanganya. Alijikuta akinyanyuka na kuketi kwenye kitanda na kumuuliza Balkis.
“Balkis unaonekana unajua mambo mengi juu yangu ya Ashura?”
“Ndiyo maana nipo hapa kuokoa maisha yako, kwa vile lengo la mkeo wa uongo limetimia.”
“Yote haya umeyajulia wapi?”

“Utajua ukinipa moyo wako uliojeruhiwa niuponye.”
“Kwa ukweli niliouona nipo tayari kukukabidhi moyo wangu.”
“Je, Ashura akirudi kukubembeleza?”
“Kwa uliyonieleza siwezi kurudiana na mwanamke yule ambaye kwangu ni muuaji.”

“Nakuhakikishia kama utakuwa mkweli nitayabadili maisha yako, lakini chonde unigeuke baada ya kuwa na maisha mazuri utanisamehe.”
“Nikuhakikishia nitakupenda kwa moyo wangu wote, najiona kiumbe mwenye bahati kupendwa na mwanamke mrembo tena mwenye maisha mazuri. Nakuapia kukupenda mapenzi ya dhati.”
“Asante Muddy.”
                                                           ***
Balkis baada ya kujua Muddy ataletewa barua ya kuitwa mahakamani aliingia ndani kwa Muddy bila kuonekana na kwenda kukaa sebuleni kusubiri kitakacho tokea. Baada ya barua kuletwa na kukabidhiwa Muddy, alijua nini kitafuata. Baada ya kuisoma na kuonekana amechananyikiwa alitumia muda ule kuficha kila kitu ambacho angetumia kwa ajili ya kujitoa uhai. Hata alipokwenda dukani aliyemuuzia sumu ya panya, Balkis alijigeuza na kumuuzia kitu kingine kisicho na madhara yoyote.

Kwa vile alikuwa amechanganyikiwa hakuichumza aliiweka kwenye glasi na kuichanganya na kuinywa kisha aliinywa. Lakini Balkis alikuwa amemuwekea dawa za usingizi ambazo zilimlevya baada ya kunywa na kulala usingizi mzito. Baada ya kumuona amelala,  ndipo alimpomwacha na kwenda kwa Ashura mke wa Muddy.
                                                                ******
Siku ya pili Muddy alifika mahakama kama ilivyopangwa, baada ya kesi kusikilizwa iliahilishwa wiki moja. Muddy alishangaa kutomuona Balkis mahakamani, baada ya kutoka mahakamani aliamua kwenda nyumbani kwao Balkis ili akajue nini kimemsibu baada ya kukosekana asubuhi ile kama alivyomuahidi kufika. Aliendesha gari lake ambalo kutokana na maelezo ya Balkis kuwa litapigwa mnada pamoja na nyumba na kugawana fedha zake, ambazo nazo zitachukuliwa na mtalaka wake na kumuacha bila kitu.

Njia nzima alikuwa na mawazo juu ya hatima ya maisha yake kama atanyang’nywa kila kitu. Alipofika maeneo ya Daraja la Salenda alitembea taratibu kuitafuta nyumba ya kina Balkis ambayo aliamini ilikuwa maeneo yale.
Lakini alijikuta akichanganyikiwa kutoliona jumba la kifahari alilopelekwa na Balkis. Mawazo yake yaliamini huenda amekosea eneo.

Kutaka kupata uhakika wa sehemu aliyopelekwa usiku na Balkis, aliendesha gari mpaka sehemu waliyotelemka na mkewe usiku. Alipofika pale alirudi taratibu huku akipepesa macho kuangalia labda ataliona jumba la kifahari. Lakini hakuona chochote zaidi ya miti na bahari kwa nyuma.

Alijikuta akijiuliza lile jumba alilolala mbona halionekani, alipanda ndani ya gari na kuanza kulitafuta kwa kuendesha gari taratibu kuelekea Masaki labda ataliona jumba lile. Aliendesha gari taratibu huku akipepesa macho labda ataliona jumba la kifahari kama lile ambao katika maisha yake hakuwahi kuona.

Lakini gari lilizidi kwenda bila kuliona, majumba mengi alioyaona yalikuwa mazuri lakini hayakuweza kufikia hata robo ya uzuri wa jumba la kina Balkis  Ambalo lilikuwa na eneo kubwa tofauti na majumba yaliyokuwa yamepangana pia maeneo yake yalikuwa madogo.

Mpaka anafika Sea cliff Hotel hakuona jumba lile alilopelekwa na Balkis, aliamini kabisa atakuwa amekosea tu. Aligeuza gari na kurudi tena hadi sehemu aliyoachwa na mkewe usiku na kuonana na Balkis. Aliamua kutelemka kwenye gari na kutembea kwa miguu kufuata njia aliyopelekwa na Balkis, alikumbuka hakwenda njia ya Masaki bali alirudi kama anakwenda Daraja la Salenda.

Muddy alitembea taratibu huku akipepesa macho huenda akaliona jumba lile la kifahari, lakini mpaka anavuka Daraja la Salenda bado hakuona jumba lile.
ITAENDELEA SIKU YAKESHO

No comments

Powered by Blogger.