ad

ad

IDRIS SINA MPANGO WA KUWA NA MPENZI



MSHINDI wa Shindano la Big Brother Hotshots 2014, Idris Rashid Sultan ameweka wazi kuwa bado hajajipanga kuwa na mpenzi na suala hilo halipo kwenye mipango yake kabisa.

Akizungumza na Global TV Online, Idris alisema sasa hivi akili yake ipo katika kubadilisha maisha ya watu ambao wamebadilisha maisha yake mpaka sasa hivi.

Mhariri Kiongozi wa Championi, Saleh Ally (kushoto), Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Richard Manyota (wa pili kutoka kulia), Meneja Mahusiano wa DSTV,  Barbara Kambogi (kulia) wakiwa katika pozi na mshindi wa Hotshots 2014, Idris Sultan.

“Sijajipanga na sitaki kujipanga kwa sababu haipo kwenye mipango yangu, huu ni muda wa mimi kufanya kazi hayo yapo na nitayakuta tu,’ alisema Idris.

No comments

Powered by Blogger.