Y-TONY AMWANIKA DEMU WAKE
Mbongo Fleva anayesumbua na wimbo wa Masebene, Elly Michel Kilema ‘Y-Tony’ akiwa na bebi wake wa ‘long time’, Asia Msemo.
MBONGO Fleva anayesumbua na wimbo wa Masebene, Elly
Michel Kilema ‘Y-Tony’ amevunja ukimya kwa kumwanika mpenzi wake wa
‘long time’, Asia Msemo.
Tukio hilo la kumwanika kimwana wake
alilifanya juzikati baada ya kutua ndani ya Ofisi za Global Publishers,
Bamaga-Mwenge, Dar kutambulisha video ya wimbo wake mpya unaokwenda kwa
jina la Shitobe.
“Ujue ni wanaume wachache sana wanaoweza kutambulisha wapenzi wao
kwenye video za nyimbo zao na kuthubutu kuanika wazi kama ana uhusiano
naye, mimi sioni shida kumtaja Asia kama demu wangu maana nimetoka naye
mbali na nimemtumia kama video queen katika wimbo wangu wa Shitobe,”
alisema Y-Tony.
Post a Comment