CHUCHU AZUA TIMBWILI BARABARANI
NI mkalia nyonga wa Vincent Kigosi ‘Ray’, Chuchu
Hansi amezua timbwili la aina yake barabarani baada ya kukimbiza gari la
msanii aitwaye Ester Kiama akijua ni gari la ‘bebi’ wake.
Baby wa Vincent Kigosi ‘Ray’, Chuchu Hancy.
Timbwili hilo lilitokea juzikati maeneo ya Kinondoni jijini Dar
ambapo msichana huyo alikuwa akiendesha gari hilo aina ya Mark X nyeusi
ambalo limefanana na la Ray, Chuchu alipoliona kwa mbali linaendeshwa na
msichana, akaanza kulikimbiza.
Chanzo kilichoshuhudia ishu hiyo kimesema licha ya Chuchu kufanikiwa
kulipata na ‘kuliziba’ kwa mbele gari hilo, aliumbuka pale alipolikagua
na kugundua si la Ray.Alipoulizwa Chuchu na mwanahabari wetu kuhusu
tukio hilo, alijibu kwa kifupi:
“Jamani naomba hilo sipendi kulizungumzia.”
.jpg)
Post a Comment