STAA WA FILAMU: TIKO ABONDWA NA HAWARA WAKE
Staa wa filamu za Kibongo, Tiko Hassan akiwa na jeraha la kipigo kutoka kwa hawara yake.
STAA wa filamu za Kibongo, Tiko Hassan, hivi karibuni alionja joto ya jiwe baada ya kushushiwa kipigo kizito na hawara wake aliyetajwa kwa jina moja la Ally.
Kwa mujibu wa chanzo makini, siku ya tukio Tiko alikuwa na Ally
nyumbani kwake, Mwananyamala ndipo ghafla hali ya hewa ikachafuka baada
ya pedeshee mmoja kumpigia simu mwigizaji huyo.
“Mzozo ulianzia kwenye simu na huwezi amini amemvunjia simu yake
kwani alimpiga kwa sababu alikuwa akiongea na mwanaume mmoja kimahaba na
hapo ndipo timbwili lilipoanza,” kilidai chanzo hicho.
Kikazidi kumwaga ubuyu kwamba, wakati kipigo cha ngumi kikiendelea,
mwanaume huyo alimrushia chupa Tiko ambayo ilimpasua usoni na kumuacha
na jeraha kubwa lakini hakwenda kumshtaki polisi kwa kuwa anampenda
sana.
Tiko Hassan akiuguza jeraha lake.
Baada ya habari hizo kutua gazetini, mapaparazi wetu walimtafuta Tiko
na kufanikiwa kumpata nyumbani kwao Mbagala ambapo alifunguka:
“Yule ana wivu sana na mimi, huyo mtu aliyenipigia simu simjui na
alikuwa akijaribu kunitongoza na mimi nilikuwa nikimkaripia lakini kibao
kilinirudia, nikapigwa.
“Nilitibiwa katika Hospitali ya Cam hapa Mbagala, kwa sasa nauguza
kidonda nikipona nitajua cha kumfanyia kwani amenifanya niwe na jeraha
usoni.”
CREDIT:GPL
Post a Comment