ad

ad

SHUJAA SENZO MEYIWA AZIKWA KWA HESHIMA KUBWA DURBAN


Hatimaye jana aliyekuwa kipa wa Orlando Pirates, Senzo Meyiwa amezikwa kwa heshima kubwa.
Meyiwa aliyekuwa pia nahodha wa timu ya taifa ya Afrika Kusini ‘Bafana Bafana’ amezikwa kwao Durban.

Amezikwa kwenye makaburi ya watu maarufu ya Chesterville karibu kabisa na alipozikwa aliyekuwa mwandishi maarufu Nat Nakasa.
Mashabiki walijitokeza kwa wingi kuuaga mwili wake katika Uwanja wa Moses Mabida mjini Durban.

Kipa huyo aliuwawa kwa kupigwa risasi na watu wanaominiwa kuwa majambazi na tayari mtu mmoja amekamatwa akituhumiwa kwa mauaji hayo.

No comments

Powered by Blogger.