NIGERIA:WANAFUNZI 23 WAUAWA SHULENI
Kundi la
Boko Haram limekuwa likifanya mashambulizi mara kwa mara katika mji wa
PotiskumKumetokea shambulizi katika shule moja ya upili wakati wanafunzi
wakiwa wamekusanyika shuleni humo mjini Potiskum Kaskazini Mashariki
mwa Nigeria.
Hata
hivyo hakuna taarifa kamili kuhusu idadi ya majeruhi kufikia sasa ingawa
duru zinasema kuwa wanafunzi kadhaa wameuawa na wengine wengi
kujeruhiwa.
Shambulizi
lilitokea wakati wanafunzi wakiwa wamekusanyika wakati wa asubuhi. Mji
wa Potiskum ambapo shule hiyo ipo, umekuwa kitovu cha mashambulizi
ambayo yamekuwa yakifanywa na Boko Haram.
Shule
hiyo ni ya mafunzo ya sayansi. Mwalimu mmoja alinukuliwa akisema kuwa
alisikia mlio mkubwa wa kutisha wakati bomu hilo lilipolipuka.
Kundi la wapiganaji wa kiisilamu Boko Haram huenda ndilo limefanya shambulizi hilo, ila taarifa bado hazijathibitisha hilo.
Kadhalika
kundi hilo limekuwa likishambulia shule katika harakati zake za miaka 5
likitaka kuunda dola ya kiisilamu huku likipinga elimu ya kimagharibi.
Wiki jana shambulizi la kujitoa mhanga lilifanyika mjini humo na kuwaua watu 15 wakati wa maandamano ya kidini.
CHANZO:BBC

Post a Comment