MBOWE AKINUKISHA NYUMBANI KWA SITTA URAMBO
Urambo.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amefanya mkutano mkubwa Urambo Mashariki na kumshutumu Mbunge wa jimbo hilo, Samuel Sitta kwa kuchakachua maoni ya wananchi katika mchakato wa Katiba Mpya.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amefanya mkutano mkubwa Urambo Mashariki na kumshutumu Mbunge wa jimbo hilo, Samuel Sitta kwa kuchakachua maoni ya wananchi katika mchakato wa Katiba Mpya.
Katika mkutano huo ulifanyika katika Uwanja wa
Extended mjini hapa takriban mita 100 kutoka nyumbani kwa Sitta
aliyeongoza Bunge la Katiba, Mbowe alisema historia ya nchi hii
itamhukumu mbunge huyo kwa maovu hayo.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akiwasili kwenye Uwanja wa Extended mjini Urambo, Tabora alikohutubia mkutano wa hadhara juzi.
Alisema kutokana na uovu huo wa Sitta ambaye amekuwa akiisifia Katiba Inayopendekezwa kuwa itakuwa nzuri Afrika Mashariki na Kati, vyama vya upinzani vitaendelea kuidai katiba ya wananchi hata kwa miaka 100 ijayo.
Aprili mwaka huu, wabunge wa vyama vya upinzani
chini ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), walisusia Bunge la Katiba
mjini Dodoma wakilalamikia kuvunjwa kwa kanuni na kutofuatwa kwa
mapendekezo ya wananchi yaliyotolewa katika Rasimu ya Tume ya Mabadiliko
ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba.
Akihutubia mamia ya wafuasi wa chama hicho kwenye Operesheni Delete CCM, Mbowe ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa Ukawa, alisema ana uhakika Sitta ataipata hukumu hiyo ya historia kwa kile alichosema kudhulumu haki ya Watanzania milioni 45.
Mbowe anayetumia chopa katika ziara hiyo, alifika katika uwanja huo saa 11.45 na kuhutubia kwa dakika 30.
“Mzee Sitta najua upo nyumbani hapo na unanisikia, kama hunisikii basi mke wako Mama Margreth Sitta atakuwa ananisikia, lakini kama naye hayupo basi kutakuwa na wahudumu watanisikia na watakuja kukueleza,” alisema huku akiwaonyesha wafuasi wa chama hicho nyumba ya Sitta iliyopo jirani na uwanja huo.
Alisema Sitta alipuuza maoni ya wananchi waliyotoa
katika mchakato wa Katiba Mpya na ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba
badala yake akaweka maoni ya chama chake cha CCM.
“Tunasema kwamba historia ya nchi hii itamhukumu kwa maovu aliyoyafanya kukataa maoni ya wananchi na kuweka maoni ya chama chake,” alisema.
Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani
Bungeni na Mbunge wa Hai, alisema baada ya maoni ya wananchi
kuchakachuliwa... “Sasa tutaidai Katiba Mpya hata kwa miaka 100 ijayo.”
Alisema wabunge wa vyama vya upinzani walimwamini Sitta kwa kumpigia debe na baadaye walimpa kura iliyomfanya awe Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba kutokana na rekodi yake alipokuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Tulifanya hivyo kwa kumwamini kutokana na rekodi
zake akiwa spika, tunajuta kumchagua hatukufahamu kwamba atatusaliti na
kudhulumu haki za Watanzania,” alisema Mbowe.
Mbowe alisema Sitta ambaye pia ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, alidiriki kuwatukana hata viongozi wa dini waliomshauri kuhusu umuhimu wa maoni ya wananchi katika Katiba.
Wakati wa Bunge la Katiba linakaribia ukingoni Septemba mwaka huu, Sitta alitumia maneno makali kuwajibu viongozi wa dini waliotoa waraka kukosoa mwenendo wa Bunge hilo, akisema waraka huo ulikuwa wa kipuuzi na haukuwa na utukufu wa Mungu.
Ufisadi bomba la gesi
Hivi karibuni Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi
alilieleza gazetin hili katika mahojiano maalumu kuwa Sitta aliwageuka
wapinzani baada ya kuwaomba wamchague kuwa mwenyekiti akiahidi kupigania
serikali tatu, lakini baada ya kupata nafasi hiyo akapigania serikali
mbili, madai ambayo Sitta aliyapuuza akisema Sugu hakuwa saizi yake.
Mbowe alisema Sitta ambaye pia ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, alidiriki kuwatukana hata viongozi wa dini waliomshauri kuhusu umuhimu wa maoni ya wananchi katika Katiba.
Wakati wa Bunge la Katiba linakaribia ukingoni Septemba mwaka huu, Sitta alitumia maneno makali kuwajibu viongozi wa dini waliotoa waraka kukosoa mwenendo wa Bunge hilo, akisema waraka huo ulikuwa wa kipuuzi na haukuwa na utukufu wa Mungu.
Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Vijana wa Chadema
(Bavicha), Patrobazi Katambi alisema kwa heshima ya wananchi wa Mkoa wa
Tabora, Sitta (72), anatakiwa kupumzishwa katika nafasi zake zote za
uongozi kutokana na umri wake.
“Ni kweli mzigo mzito anatakiwa kubebeshwa
Mnyamwezi lakini kwa umri alionao Sitta ni kama tunamkosea adabu kwani
huu ni muda wake wa kupumzika, tusimchague tena,” alisema huku
akishangiliwa na wafuasi wa chama hicho.
Ufisadi bomba la gesi
Mbowe alitumia mkutano huo kuitaka Serikali
kuitisha wakaguzi wa kimataifa ili wachunguze mkataba wa ujenzi wa
bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam ambao alidai kuna ufisadi
wa Sh1.2 trilioni, vinginevyo atawaeleza wananchi ili waamue.
Juzi, Mbowe aliwatuhumu vigogo wa Serikali kuwa
waliongeza fedha katika mradi huo ambazo waligawana kwa masilahi yao
binafsi lakini mkopo huo kutoka China utalipwa na Watanzania wote.
Alisema mradi huo ulikuwa wa Sh1.2 trilioni lakini vigogo hao waliongeza kiasi kama hicho na kugharimu Sh2.4 trilioni.
Alisema ukaguzi unatakiwa kufanyika ili kufahamu
thamani ya fedha halisi zinazotakiwa kujenga bomba hilo na fedha
zilizotolewa na Serikali.
“Hili nitalisema popote bila woga na niko tayari
kukamatwa lakini sitakaa kimya nikishuhudia Watanzania wakilipa deni la
fedha walizogawana vigogo hao,” alisema Mbowe.
Alisema ikiwa Serikali ina nia ya dhati kupambana
na ufisadi, iweke hadharani mkataba wa ujenzi wa bomba hilo... “Ndiyo
maana mikataba hii imekuwa siri, inafichwa ili wananchi wasiione lakini
tunasema Chadema tutaendelea kuipata na mafisadi watajulikana.”
CHANZO: MWANANCHI
Post a Comment