ad

ad

MAXIMO, JAJA, COUTINHO WAANZA LIKIZO BRAZIL

Kocha Mkuu wa Yanga, Marcio Maximo na wachezaji wake wawili, Jaja na Coutinho wametua nchini Brazil salama salimi.

Taarifa zinaeleza kocha huyo na wachezaji hao wawili, wameanza mapumziko rasmi ya siku 10.
“Kweli kocha, Jaja, Coutinho wameanza mapumziko na watarudi nchini baada ya Novemba 20.
“Pia wachezaji wengine wamepewa mapumziko na wataanza mazoezi pamoja,” kilieleza chanzo.

Maximo, Jaja na Coutinho hawatakaa Brazil muda mrefu kwa kuwa wanatakiwa kurejea mapema kuanza maandalizi ya mechi ya kirafiki dhidi ya Simba.

No comments

Powered by Blogger.