MASTAA KUMFANYIA PATI LOWASA
Staa katika tasnia ya filamu Bongo, Jacqueline Wolper.
SIKU chache baada ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward
Lowassa kutangazwa kuwa anaongoza katika kinyang’anyiro cha urais 2015,
mastaa mbalimbali wanaomuunga mkono wameandaa mkakati wa kumfanyia
sherehe ya kumpongeza.
Chanzo makini kilichopo ndani ya kamati ya wasanii hao wa Bongo
Movies, kitendo cha Taasisi ya Twaweza kutangaza kuwa Lowassa anaongoza
na kuwagaragaza makada wenzake ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kwao
ni ishara tosha ya ushindi wa kishindo katika uchaguzi ujao.
“Mastaa wa Bongo Movies wanaomuunga mkono
Lowassa wameandaa bonge la pati la kumpongeza Lowassa na siku hiyo
watakula, watakunywa maana mipango yao tayari wanaona inakwenda vizuri
na hakuna mtu ambaye anaweza kumuangusha katika chama hicho,” kilisema
chanzo bila kutaja lini na wapi watakapofanyia sherehe hiyo.
Staa katika tasnia ya filamu Bongo, Esha Buheti.
Mbali na sherehe hiyo kuhudhuriwa na mastaa mbalimbali, chanzo hicho
kimeeleza kuwa wanatarajiwa pia kualikwa wananchi mbalimbali wanaomuunga
mkono Lowassa.
“Safari ya kuelekea uchaguzi mkuu ndiyo imeanza rasmi, Twaweza
wametafiti na kubaini kile ambacho sisi tulikuwa tunakiamini, Lowassa
hana mpinzani CCM, ushindi ni lazima,” kilisema chanzo hicho.
Staa katika tasnia ya filamu Bongo, Mahsein Awadhi.
Wasanii ambao wanatajwa kuwa upande wa Lowassa ni Jacqueline Wolper,
Esha Buheti, Mahsein Awadhi ‘Dk. Cheni’, Wema Sepetu ‘Madam’ na wengine
kibao.
Taasisi ya Twaweza iliyofanya utafiti kwa mwezi Septemba, ilitangaza
matokeo hayo Jumatano iliyopita na mtafiti wake, Elvis Mushi ambapo
alisema wananchi 1,445 walihojiwa kwa njia ya simu ambapo Lowassa
alipata asilimia 13 huku waziri mkuu wa sasa, Mizengo Pinda akimfuatia
kwa kupata asilimia 12.
Wema Sepetu ‘Madam.
Wengine waliopigiwa kura katika utafiti huo ni Katibu Mkuu wa
Chadema, Wilbrod Slaa aliyepata asilimia 11, Mwenyekiti wa CUF, Profesa
Ibrahim Lipumba akipata asilimia 6 huku Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard
Membe akiondoka na asilimia 5.
Post a Comment