MALICK: MWACHENI ROSE NDAUKA AJIRUSHE
BAADA ya msanii wa filamu Bongo, Rose Ndauka
kuonekana akijiachia viwanja mbalimbali tofauti na alivyokuwa akiishi
awali, mzazi mwenzake, Malick Bandawe, ameibuka na kumfungukia kuwa
aachwe ajirushe.
Malick Bandawe.
Malick alifungua kinywa kufuatia madai kwamba alipokuwa akiishi na
Rose alikuwa akimpa sheria kali na kumkataza kwenda ‘out’ ndiyo maana
alikuwa hajiachii kama ilivyo sasa na hiyo ni moja ya sababu
zilizosababisha uhusiano wao kuvunjika.
“Mimi siyo mkali wala sina sheria hizo ninazoambiwa ila nilikuwa
nachukua muda mwingi sana kuzungumza na Rose na ninaamini amejifunza
mengi sana mazuri ambayo akiyazingatia yatamsaidia maishani.
Msanii wa filamu Bongo, Rose Ndauka.
“Sababu za Rose kujiachia hivyo ni kutokana na maisha ambayo tulikuwa
tunaishi hivyo anahitaji muda atatulia na atakuwa sawa na hapo ndipo
atakapoanza kuyafanyia kazi yale mazuri aliyoyapata kutoka kwangu,
sitegemei yeye kufanya mabaya ila nategemea afanye mazuri kwa ajili ya
mtoto wetu,”alisema Malick.

Post a Comment