KWAHERI PHIRI ATOA NENO ZITO UWANJA WA NDEGE
Na Wilbert Molandi
KOCHA Mkuu wa Simba Mzambia, Patrick Phiri, jana alioondoka nchini kuelekea Zambia kwa mapumziko ya wiki moja, baada ya Ligi Kuu Bara kusimama kupisha michuano ya Cecafa iliyopangwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu.
Mzambia huyo, anarejea kwao baada ya kukabidhi ripoti ya raundi ya kwanza ya Ligi Kuu Bara kwa Kamati ya Utendaji ya Simba, iliyokutana hivi karibuni na kuijadili ripoti hiyo kabla ya kurejea kwao jana saa moja usiku kwa Shirika la Ndege la Kenya.
Kocha huyo, alifika kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam saa 11:00 jioni akiwa peke yake huku akisukuma toroli la kubebea mizigo bila ya kusindikizwa na kiongozi yeyote.
Mara baada ya kufika uwanja wa ndege alionekana kama mtu ambaye hakuwa na furaha huku baadhi ya watu wakimshangaa, alisukuma toroli hilo hadi aliposimamishwa na mwandishi wa gazeti hili na kuanza mahojiano hayo.
Mpaka anafika kwenye uwanja wa ndege, alikuwa hajui tarehe ya kurejea nchini kujiunga na kikosi chake hadi alipofika mapokezi alipokwenda kuulizia tarehe ya kurejea na kujibiwa atarejea Novemba 26, mwaka huu.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Phiri alisema ameomba mapumziko hayo ya wiki moja ili arejee mapema kukiandaa kikosi chake kwa ajili ya mechi ya Nani Mtani Jembe itakayopigwa Desemba 13, 2014 timu yake itakapovaana na Yanga kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
“Katika ripoti nimesisitiza kuwa tukipata mshambuliaji mmoja mwenye uwezo mkubwa wa kufunga mabao yatakuwa mazuri,” alisema Phiri.“Mchezaji mwingine ambaye nimempendekeza ni Amer Ally wa Mtibwa Sugar, pia tukipata kiungo mmoja na beki wa kulia itakuwa vizuri zaidi,” alisema Phiri ambaye wakati anatua nchini kuinoa timu hiyo alipata mapokezi makubwa kutoka kwa viongozi na wanachama wa Simba na kuongeza:
“
Amer nilimuona kwenye mechi ya Mtibwa na Tanzania Prisons huko Mbeya, kiukweli anajua kupambana, lakini pia nataka kiungo na beki mmoja pekee, pia nimesisitiza hakuna kumtema mchezaji yeyote kati ya hao nilionao.”
Aliongeza kuwa, ameutaka uongozi wa timu hiyo kutouza mchezaji yeyote huku akisisitiza kumbakisha mshambuliaji Mkenya, Paul Kiongera, Mrundi, Amissi Tambwe na kiungo Pierre Kwizera wanaotajwa kuachwa kwenye timu yake kwa kuwa anaamini bado wana uwezo mkubwa ndani ya uwanja.
“Kama unavyojua mechi dhidi ya Yanga ni ‘Derby’, licha ya Yanga kutokuwa na rekodi ya kunifunga mara kwa mara ninapokutana nayo lakini nimepanga mara baada ya kurejea nchini, haraka timu itaelekea Zanzibar kwa ajili ya kambi ya pamoja kujiandaa na mchezo huo.”

(CHANZO: CHAMPIONI IJUMAA/GPL)
Post a Comment