DORIS MOLLEL ACHANGIA VITABU SHULE YA MSINGI MPUNGUZI, DODOMA KWA USHIRIKIANO NA MAK SOLUTIONS LTD
Alipokuwa njiani kuelekea mpunguzi, Doris alipata nafasi ya kuongea machache na baadhi ya wanafunzi wa vijiji vya jirani.
Wanafunzi wakimsikiliza kwa makini.
Doris
Mollel (kulia) akitia saini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili
shuleni Mpunguzi. Kushoto ni Afisa elimu - ufundi manispaa ya Dodoma Bw
Mnyagatwa Mazengo na katikati ni mwalimu mkuu wa shule ya mpunguzi Bi
Neema Mando.
Doris
akiuleza uongozi wa shule nia na madhumi ya safari yake. Kushoto ni
mwalimu mkuu msaidizi Bw Danctan Chipalo na mwalimu mkuu Bi Neema mando.
Afisa
elimu - ufundi manispaa ya Dodoma Bw Mnyagatwa Mazengo akimsaidia Doris
kuchambua vitabu hivyo kutoka kwenye boksi la MAK Solutions Ltd.
Doris akiwaeleza wanafunzi umuhimu wa kupenda kujisomea tangu wakiwa wadogo.
Kutoka kushoto: Bw Danctan Chipalo, Bw Mnyagatwa Mazengo Bi Neema Mando na Doris.
Doris akiwa na baadhi ya wanafunzi baada ya kugawa vitabu.
Wanafunzi wakifurahia vitabu vyao.
Akimuelekeza mmoja wa wafunzi juu ya mambo yaliyomo kwenye kitabu cha ‘WATER’
Wakiwa na Vitabu.
Makabidhiano.
Doris akiongea jambo na mwalimu mkuu mara baada ya makabidhiano hayo.
Akiwa kwenye picha ya pamoja kwenye viwanja vya shule hiyo muda mfupi kabla ya kuondoka shuleni hapo.
Dodoma, Novemba 2014.
Katika
kuadhimisha siku ya watoto duniani inayofanyika tarehe 20 Novemba kila
mwaka, Mrembo wa Redds Miss central Zone 2014 Doris Mollel amechangia
Vitabu vyenye thamani ya Shilingi Milioni moja (1,000,000/=) katika
shule ya msingi Mpunguzi iliyopo katika kijiji cha Mpunguzi mkoani
Dodoma.
Doris,
ambaye pia ni mshindi wa tatu kwenye Redds Miss Tanzania 2014 amejikita
katika sekta ya elimu kama sehemu ya huduma zake za jamii ambapo
amedhamiria kuendeleza mchango kwenye elimu ya msingi kwa kuchangia
vitabu kwenye shule zenye uhitaji zaidi.
Msaada
huo wa Vitabu 200 vya kiada na ziada ameutoa kwa ushirikiano na kampuni
ya uuzaji wa Vitabu ya MAK Solutions yenye duka lake Mlimani City
jijini Dar es salaam ambapo mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Bi
Meetal Kirubakaran alisema MAK solutions wanafurahi kutoa vitabu hivyo
kama mchango wao katika kusaidia sekta ya elimu Tanzania.
Doris
akijadiliana jambo na Afisa elimu wa mkoa wa Dodoma Bw. Juma Kaponda
(Katikati) mjini Dodoma kabla ya kuelekea Mpunguzi. Wa kwanza kushoto ni
Afisa elimu - ufundi manispaa ya Dodoma Bw Mnyagatwa Mazengo na
anayefuata ni Afisa elimu – Taaluma wa mkoa Bw Eliud Njogela.
Akizungumza
kwenye hafla iliyofanyika shuleni hapo, Mollel alisema ‘Ni muhimu
kuwajengea watoto wetu utamaduni wa kujisomea tangu wakiwa wadogo ili
kuwakuza kukabiliana na changamoto za dunia ya sasa ambayo inahitaji
uelewa mpana. Najivunia kuwa sehemu ya kampeni hii na nitaendelea
kuongeza jitihada za kuwafikia watoto wengi zaidi’
Afisa
elimu wa mkoa wa Dodoma Bw. Juma Kaponda amempongeza Doris kwa juhudi
zake za kusadia jamii hasa sekta ya elimu na ameomba wadau wengi kuiga
mfano huu kuendeleza sekta hii.
Hafla
hiyo ya makabidhiano ilihuduriwa na mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi
Mpunguzi Bi Neema Mando, Makamu mwalimu mkuu wa shule Bw Danctan
Chipalo, Afisa elimu - ufundi manispaa ya Dodoma Bw Mnyagatwa Mazengo,
Afisa elimu – Taaluma wa mkoa Bw Eliud Njogela pamoja na wanafunzi wote
wa shule ya Mpunguzi.
Post a Comment