KIM POULSEN KOCHA MPYA SIMBA
Na Ezekiel Kitula
SIMBA imeamua kufanya mabadiliko kwa kumtwaa kocha Kim Polusen raia wa Denmark katika nafasi ya Mzambia, Patrick Phiri.Simba imeingia kwenye harakati za kumng’oa Phiri ambaye ameiongoza Simba katika mechi sita tu za Ligi Kuu Bara na zote ametoka sare. Simba imefunga mabao sita, imefungwa sita na ina pointi sita.

Mdenishi Poulsen ambaye yuko kwao nchini Denmark baada ya kuzinoa
timu za taifa za vijana na baadaye Taifa Stars, aliondolewa kwenye kiti
chake baada ya kuingia kwa uongozi wa Jamal Malinzi.Habari za uhakika
ambazo Championi Jumatano limezipata ni kuwa, Simba wamefanya mazungumzo
na Poulsen na kukubaliana kila kitu na yupo tayari kuja nchini wakati
wowote.
Lakini kumekuwa na suala la Phiri kidogo limekuwa likiwagawa baadhi
ya wajumbe wa kamati ya utendaji kutaka apewe mechi ya mwisho ambayo
itakuwa ni dhidi ya JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar,
Jumapili.
“Kweli viongozi wamejadili kila kitu na Poulsen, ni uhakika kama
ulivyosema. Wamekubaliana suala la mshahara na kila kitu kipo
wazi.“Poulsen amewaeleza mshahara, mwisho wamekubaliana. Halafu
likafuatia suala la nyumba, kocha amesema angependa kuishi Masaki, pia
wamekubaliana katika hilo.
“Mwisho lilikuwa ni suala la usafiri na tiketi za kwenda na kurudi
kwao Denmark, hilo pia wamekubaliana. Hivyo wanachosubiri huenda kikawa
ni mechi ya Jumapili na kama si mechi hiyo, basi angekuwa ameishatua,”
kilifafanua chanzo.
“Ila hata hivyo inachanganya, kama Simba ikishinda sijajua itakuwaje.
Kinachoonekana ni kwamba kocha Phiri si mbaya, ila hana nguvu kwa
baadhi ya wachezaji ambao wamepoteza nidhamu.
“Pia amekuwa na tabia ya kutotaka kuwaudhi watu, anataka kila mtu afurahi hata kama anaharibu. Ndiyo maana viongozi wameona vema kumleta Poulsen.”
“Pia amekuwa na tabia ya kutotaka kuwaudhi watu, anataka kila mtu afurahi hata kama anaharibu. Ndiyo maana viongozi wameona vema kumleta Poulsen.”
Iwapo Simba itashikilia msimamo wake wa kumleta Poulsen, basi lazima
itaendelea na rekodi yake ya kuwa timu iliyofukuza makocha wengi zaidi
kwa misimu mitatu mfululizo.Katika misimu miwili iliyopita, Simba
ilifundishwa na makocha wanne tofauti, kila mmoja akifundisha nusu
msimu.
CHANZO: CHAMPIONI

Post a Comment