ISABELA AMVAA MAMA WEMA
MSANII wa Filamu na Muziki
Bongo, Isabela Mpanda amemvaa mama wa msanii mwenzake, Wema Sepetu,
Miriam Sepetu na kumtaka aache kuingilia mapenzi ya mwanaye kwani
mapenzi hayaingiliwi.
Msanii wa Filamu na Muziki Bongo, Isabela Mpanda.
Akistorisha na gazeti hili, Isabela alisema
siku zote unaopenda ni moyo siyo mwili kwa hiyo mama Wema kama anataka
mwanaye aachane kabisa na Diamond basi amtoe moyo uliompa nafasi
mwanaume huyo.
Mama mzazi wa msanii maarufu bongo, Wema Sepetu.
“Mama Wema kama mzazi anatakiwa akae kimya, amuache mwanaye moyo wake
ufanye utakavyo maana kutoa maneno na kufanya sherehe kwa sababu ya
mwanaye ameachana na Diamond siyo sawa, akumbuke kwamba Diamond naye ana
wazazi, hivi mama yake anajisikiaje jamani?” alihoji Isabela.

kama umezaaa baadaye utajua kwanini mama wema alikuwa anafanya hivi, kwa sasa endelea kushangaa na kujuiliza na kuhoji ,
ReplyDelete