EXCLUSIVE: MKUDE AMWAGA WINO SIMBA, MIAKA MIWILI, WALIOMTAKA WOTE KIMYAAA
![]() |
| MKUDE AKISAINI MKATABA LEO MBELE YA RAIS WA SIMBA, EVANS AVEVA |
Hatimaye
kiungo Jonas Mkude amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Simba.
Mkude
amesaini mkataba huo leo mbele ya Rais wa Simba, Evans Aveva.
Pamoja
na Aveva na viongozi wengine wa Simba akiwemo Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili
ya Simba, Zacharia Hans Poppe, Mkude alisaini mkataba huo mbele ya waandishi wa
habari.
Awali
kulikuwa na taarifa kwamba Mkude ameishaongeza mkataba Simba.
Lakini akaieleza blogu hii hakuwa tayari amefanya hivyo. Lakini hatimaye Simba imemaliza kazi leo na kuwakata maini wapinzani wao Yanga na Azam FC waliokuwa wameanza kumtolea jicho.

Post a Comment