AMIGOLAS WA TWANGA PEPETA AFARIKI DUNIA

Mwimbaji wa zamani wa Twanga Pepeta, Hamis Kayumbu 'Amigolas' enzi za uhai wake.
Mwimbaji
wa zamani wa Twanga Pepeta, Hamis Kayumbu 'Amigolas' amefariki dunia
usiku wa kuamkia leo baada ya kulazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
kwa siku kadhaa.
Amigo alilazwa Muhimbili kwa matatizo ya moyo
ambapo taratibu za kufanyiwa upasuaji zilikuwa zikiandaliwa lakini mauti
yakamkuta kabla ya lolote kufanyika.
Mwimbaji huyu ambaye hadi anafariki, alikuwa mtumishi wa bendi ya Ruvu Stars inayomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Amigo
alikuwa mmoja wa wanamuziki waasisi wa Twanga Pepeta, akaitumikia kwa
uaminifu mkubwa kwa miaka mingi kabla ya mwanzoni mwa mwaka huu yeye na
wenzake kadhaa kuanzisha Super Stars Band ambayo baadae ikachukuliwa na
JKT na kuwa Ruvu Stars Band.
Akiwa Twanga Amigo akajijengea
umaarufu wa aina yake na kuwa kama moja ya nembo ya bendi, katika
utumishi wake uliotukuka ndani bendi hiyo, akafanikiwa kutunga wimbo
mmoja 'AMINATA' ambao ulikamata chati kwa miaka mingi tangu
ulivyorekodiwa mwaka 2003.
Kufariki kwa Amigo ni pengo kubwa kwa Ruvu Stars hasa kutokana na ukweli kuwa yeye ndiye alikuwa
Kufariki kwa Amigo ni pengo kubwa kwa Ruvu Stars hasa kutokana na ukweli kuwa yeye ndiye alikuwa
‘injinia’ wa mipango yote kuanzia Super Stars hadi Ruvu.
Kabla ya Twanga Pepeta, Amigo aliitumikia pia bendi ya Bicco Stars chini ya Kinguti System.
Msiba uko nyumbani kwa mama mzazi wa marehemu Mburahati jijini Dar es Salaam jirani kabisa na Shule ya Msingi Mianzini, na kwamba taratibu za mazishi zinasubiri ndugu na jamaa kutoka Tabora na Kigoma.

Post a Comment