ad

ad

AHADI YA NDOTONI - 01

Like: www.facebook.com/2jiachie
Web: www.2jiachie.com
Jeska alitembea kwa mwendo wa taratibu akiwa amepoteza muelekeo wa maisha yake, alijiona ni kiumbe asiye na thamani. Pamoja na uzuri aliojaaliwa na Muumba, bado alikuwa kiumbe chenye mikosi. Hakuamini uzuri aliojaaliwa na Mungu amekuwa kiumbe wa kuchezewa na wanaume.

Wazo lake lote lilikuwa kujiua ili kujiepusha na walimwengu ambao wamekuwa hawaoneshi ushirikiano naye. Alikuwa ameisha kaa na wanaume zaidi sita ambao wote walimuahidi kumuoa, lakini mwisho wa siku ilikuwa kutendwa na kushindwa kuelewa tatizo ni nini.

Katika mitihani ya maisha Jeska amejikuta akibakwa kila alipokuwa akijaribu kutoka ili kutuliza mawazo, mara ya mwisho alibakwa na wanaume zaidi ya sita ambao hawakutumia kinga. Kwa hali ile aliamini anaweza kuwa ameambukizwa virusi vya ukimwi.

Kupima aliogopa kwani aliamini angekufa kwa presha, kimuonekano alijikatia tamaa akawa si mtu wa kujiheshimu tena. Mawazoni mwake alijua huenda Mungu alimuumba ili aje amtese, tokea ajali mbaya ya moto iliyochukua uhai wa wazazi wake wote pamoja na ndugu zake akiwa na umri wa miaka saba.

Baada ya vifo vya wazazi wake waliofia ndani ya nyumba, Jeska alichukuliwa na ndugu wa baba yake na kumlea, huku wazazi wake wakiwa wamemuachia mali nyingi. Lakini kwa bahati mbaya walioachiwa kumlea walihodhi mali yote na mwisho wa siku alifukuzwa kama mbwa baada ya kuhoji mali za baba yake.

Tokea hapo Jeska alianza kuonja adha ya maisha, pamoja na kufukuzwa na ndugu wa baba yake na kutishiwa kuuawa kama atataka kujua mengi zaidi. Siku zote Mungu hamtupi mja wake aliangukia katika mikono ya wazazi wa shoga yake. Ambao walimchukua na kumuahidi kumsomesha mpaka mwisho wa elimu yake.

Jeska alishukuru Mungu na kuwaza kusomea sheria akifika chuo kikuu ili siku moja alirudishe mali iliyochuliwa na ndugu wa baba yake. Maisha kwake yalikuwa mazuri yaliyomfanya asahau mateso ya ndugu wa baba yake, aliweza kumaliza vizuri kidato cha nne kwa kupata matokeo mazuri na kumuwezesha kujiunga na kidato cha tano. Akiwa kidato cha tano huku umbile alilojaaliwa na Mungu likizidi kupendeza na kutamanisha wanaume wakwale.

Siku moja hakuamini aliposhtuka usingizini na kumkuta baba wa shoga yake aliyemuheshimu kama wazazi wake akiwa juu ya mwili wake akimbaka. Jeska aliumia sana na kulia kwa uchungu. Lakini baba wa shoga yake alimbembeleza na kumuomba aifiche siri ile yupo tayari kumfanyia chochote katika maisha yake hata kumnunulia gari.

Jeska hakutaka kuisambalatisha familia ile kwa kuogopa kumsema baba wa rafiki yake kwa mkewe, aliamua kufa na siri moyoni ambayo ilikuwa ikimla siku hadi siku hata kupoteza uwezo wake darasani. Kila alipomuona baba wa shoga yake moyo ulipasuka na kujikuta akikimbia chumbani kwake na kuanza kulia.

Aliona kama ni uonevu kwa upande wake, wazazi wake wote wamekufa kwa mpigo ndugu waliobaki kumlea wakidhurumu mali. Na mwisho wa siku mtu aliyemtegemea kuyaokoa maisha yake amegeuka kiumbe mbaya kumbaka bila ridhaa yake. Kitendo kile kilimla sana Jeska kiasi cha kupungua siku hadi siku huku akiwaweka wenyeji wake katika njia panda wasijue Jeska anaumwa nini.

Kila walipomuuliza aliishia kulia na kuamini kauli yake huenda ikawa bomu litakalo isambaratisha familia ile. Siku zote alimuomba Mungu ampe ujasiri ili weze kuyakabili majaribu yale, Edna shoga yake muda wote alikuwa karibu yake kumdadisi kutaka kujua shoga yake amekubwa na tatizo gani ambao linaweza kutafuliwa na familia yake.

Kila alipoulizwa alisema hana tatizo lolote bali hujikuta akikosa amani kufikilia jinsi wazazi wake walivyokufa ghafla kabla hawajamtengenezea mazingira ya kujitegemea. Mama Edna na Edna walimuweka chini na kumpa mifano mingi ambayo ni mitihani ya wanadamu, mama Edna alimueleza.

“Jeska mshukuru Mungu, usipige teke fadhira zake, ni bahati kupata sehemu salama kama hii. Ni wangapi wamefiwa na wazazi wao lakini leo hii wanahangaika na kuishiwa kubakwa na kuambukizwa ukimwi.”

Kauli ile ilimfanya Jeska aangue kilio na kuamini hata yeye katika mawazo yake aliamini walio ndani ni salama kuliko wanaozurula. Lakini akili yake ilibadilika na kuamini watu wachache wenye uwezo huwa na huruma ya mamba kukuchekea kumbe wanakutamani kukutafuna utakapoingia kwenye maji kama alivyofanya baba Edna.

Alijuliza ni wangapi wamo katika mikono inayoonekana salama kumbe kuna watu wenye roho ya mamba kuwatafuna watu huku machozi yakiwatoka, wakiamini wanawaonea huruma kumbe na furaha ya kutafuna minofu na kiumbe kisicho na hatia.

Kilio chake kilizidi kuwaweka njia pana na kuanza kumdadisi upya.
Ndoto zake za kuwa daktari zilifutika na kuzihamishia kuwa mwanasheria mkubwa sana ambaye ataweza kuwasaidia wote waliodhulumiwa mali zao na ndugu wa mume wakiwemo yatima na wajane.

Kingine alichokifikiria ni kuanzisha NGO’S ya sheria atakayotoa huduma kwa bei ya chini hasa ikiwalenga wanyonge. Usongo aliokuwa nao na uchungu wa kudhulumiwa mali zake na kumfanya kuishi maisha ya kubahatisha kuishia kuangukia katika mikono ya wabakaji.

Mwezi wa tatu toka abakwe na baba Edna aligundua mabadiliko katika mwili wake, siku zake za hedhi hazikuonekana. Pia maumivu ya kichwa na mwili kuchoka vilimtia wasiwasi. Mabadiliko yale mama Edna aliyaona, wasiwasi wake mkubwa ulikuwa malaria.

Ilikuwa siku ambayo Jesca aliamka na kushindwa kwenda shule, kichefuchefu kilikuwa kikali sana kilichofanya atapike kila chakula alichokula asubuhi ile. Baada ya kuona dalili zote za malaria, alimpeleka hospitali, Jesca ambaye hakuwa anaelewa kilichokuwa kikiendelea, alipoulizwa na daktari alimueleza anavyojisikia.

Alichukuliwa vipimo vya malaria, majibu yalikuja hana marelia. Ilibidi kichukiliwe kipimo cha mkojo, ambacho kileleta majibu. Daktari hakutaka kumpa majibu wakiwa wote alimtoa nje Jesca ili ampe majibu mama yake.

Jesca hali ile ilimtisha japo anajua virusi vya ukimwi vinapimwa kwa damu, wasiwasi wake huenda ameathirika baada ya kubakwa na baba Edna.
Ndani daktari alimueleza majibu ya vipimo yanavyosema.
“Mama binti yako vipimo vinaonesha ni ujamzito.”
“Eeh!?” Mama Edna alishtuka kusikia vile.

“Ndiyo, binti yako anaujauzito wa miezi mitatu.”
“Mtumee, mtoto huyu!”
Mama Edna alishika mkono mdomoni na kujikuta akikumbuka miezi mitatu ya nyuma hali ya Jesca ndani ilibadilika na kuwaweka katika sifahamu. Aliamini kama Jesca amefikia hatua ya ufuska lazima atamuambukiza mwanaye Edna ambaye amekuwa naye karibu zaidi.

Wazo la kumfukuza lilikuwa gumu, kwa kuhofia jamii ingemtazama vibaya, alipanga akitoka pale amueleze mume wake, nini wafanye kutokana na tabia za chui za Jesca kujificha katika ngozi ya kondoo ya upole na ukimya.
Alitulia tuli huku akiwa amehama kimawazo na kushtuliwa na daktari.

“Mama nafikiri umenielewa?”
“Nimekulewa baba, asante.”
“Nafikiri hili swala si la kulitolea maamuzi mazito, kwani siku hizi mabinti zetu wamekuwa katika wakati mgumu kutokana na Mafataki. Wasiwasi wangu asiwe ameambukizwa ukimwi tu.”
“Mmh, hapo ndipo nachanganyikiwa.”

“Basi mama kakaeni naye chini muulizeni kwa utaratibu lazima mwenye ujauzito atamtaja. Kama kuna ushahidi mfungulieni mashtaka.”
“Nashukuru baba kwa ushauri wako.”
Mama Edna akiwa amechanganyikiwa kidogo, alitoka na kumpitia Jesca aliyekuwa hajui nini kilichokuwa kikiendelea ndani.
“Twende zetu.”

Jesca alinyanyuka na kumfuata mama yake aliyekuwa anatoka nje ya hospitali bila kuelewa nini kilichokuwa kikiendelea mule ndani.
Jioni ya siku ile baada ya kurudi baba Edna mkewe alimwita na kumueleza kilichotokea hospitali, Jesca alijisogeza kwa kujificha nyuma ya mlango ili asikie mama atamueleza nini baba na nini atakijibu juu ya kilichoelezwa hospitali.

“Za saa hizi mume wangu?”
’Nzuri, vipi za hospitali?”
‘Mmh, si nzuri,” kauli ile ilimshtua Jesca na moyo kuanza kwenda mbio na kujiuliza huenda wazo lake la kuathirika ni kweli. Mwili ulimtetemeka na kumuomba Mungu amuepushe na janga lile.

“Mbona unanitisha kuna habari gani?”
“Jesca ni mjamzito,” kauli ile ilimshtua Jesca na kushika kifuani kwa hofu huku akipiga ukelele wa chini.
“Mama yangu weee nimekwisha.”
“Eeh!?” Mzee Ezekiel alishtuka.

“Ndiyo, usishituke habari ndiyo hiyo, mtoto mbaya tunamuona mkimya kumbe ana mambo ya chini chini. Unafikiri atamfundisha nini Edna kama siyo kuwa malaya kama yeye.”
Maneno yale makali yalikuwa msumari wa moto kwenye moyo wa Jesca binti yatima asiye na kosa lolote ambaye ukimya wake ulikuwa umemponza sawa na mshumaa kuwaangazia wengine huku unateketea.
“Mke wangu taratibu, Jeska ni mtoto wetu kama Edna hivyo tumchukulie kama ni Edna amekosa na wala si mtu baki.”
“Hata angekuwa Edna nisingefurahia upuuzi huo?”
“Sifurahii na pia ningemkanya kama nitakavyo mkanya Edna, hatuwezi kuwabangua kwa vile Jeska sasa hivi ni binti yetu.Umeisha mueleza tatizo lake?”

“Bado, kwa vile nilikusubiri kwanza wewe kabla ya kumueleza mwenyewe, ili nijue tutalitatua vipi.”
“Basi kazi hiyo niachie mimi,” baba Edna aliuchukua mzigo ule kwa kuamini kabisa huenda muhusika ni yeye japo hakuwa na uhakika kamili.

Mzee Ezekiel alikubaliana na mkewe, kabla ya kubadili nguo alimtuma Edna amwite Jeska aliyekuwa nyuma ya mlango akilia kwa majuto ya ujauzito alioupata baada ya kubakwa na mzee Ezekiel. Edna alimkuta nyuma ya mlango akitokwa na machozi na macho kuvimba.
“Jeska vipi mbona kila siku umekuwa mtu wa majonzi ndugu yangu?” Edna alimuuliza kwa sauti ya huzuni.

“Basi tu, naona huu ni mwaka wangu,” Jeska alisema kwa sauti ya kilio huku machozi yakiendelea kumwagika.
“Jeska una nini tena jamani?”
“Nina imani naishi kimakosa.”
“Jeskaaa!!”

“Kila balaa linaniandama mimi, unafikiri kuna umuhimu wa kuendelea kuishi?”
“Jamani Jeska maneno gani hayo ya kusema ndugu yangu.”
“Sina mengine zaidi ya hayo, kilichobakia ni utekelezaji, likitokea usishangae ila ujumbe nitakuachia.”
“Mama yangu, Jeska unataka kufanya kitu gani Mungu wangu hebu muondoe pepo wa mauti kwenye moyo wa Jeska. Jeska usifanye hivyo hata siku moja bado una nafasi kubwa ya kuishi na kutatua matatizo yako”

“Edna, umri wangu ni mdogo lakini matatizo yanamzidi mtu aliyeishi miaka mia moja. Kama nitaendelea kuishi nafikiri kuna balaa kubwa zaidi”
“Kwani kuna nini tena Jeska”

“Ipo siku utajua”
“Basi baba anakuita naomba umueleze yanayokusumbua,” Edna naye machozi yalimtoka kwa hofu ya maamuzi mazito ya Jeska.
Jeska aliongozana na Edna mpaka sebuleni alipokuwa amekaa mzee Ezekiel, alishangaa kumuona Jeska akitokwa na machozi na macho yamemvimba.

“Jeska, una nini tena mama?”
“Basi tu baba.”
“Hebu njoo hapa binti yangu mpenzi.”
Jeska alisogea pembeni ya mzee Ezekiel, ambaye kabla ya kuzungumza naye alitoka naye nje na kwenda naye kwenye bustani. Walipofika alimuuliza kwa sauti ya upole.

“Jeska una tatizo gani?”
“Mama ameisha kwambia?”
“Una rafiki wa kiume?”
“Sina baba.”

“Una..na..taka kuniambia au una uhakika una mimba?” Mzee Ezekiel aliuliza kwa sauti ya kigugumizi.
“Mimi sijui mama ndiye aliyeambiwa majibu yangu.”
“Sasa unalia nini wakati hujajua kama una ujauzito?”
“Si mama kakwambia na hali yangu ilikuwa na kila dalili za ujauzito.”

“Mmh, unaweza kuwa wa nani?”
“Sijawahi kukutana na mwanaume hivi karibuni zaidi yako.”
“Kabla yangu umepita muda gani?”
“Mwaka wa tatu sasa.”

“Mmh, makubwa, unataka kuniambia ujauzito ni wa kwangu?”
“Labda wewe unaweza kumjua mtu mwingine zaidi yako au wa roho mtakatifu.”
“Mama yako ameisha kuuliza ujauzito wa nani?”
“Ataniuliza vipi, toka tumetoka hospitali hana habari na mimi.”

“Sasa sikiliza, nitafanya mipango kuitoa hiyo mimba ili uendelee na masomo.”
“Sawa,” Jeska alikubali.
“Akikuuliza mama yako mweleze ni ya kijana mmoja kondakta wa daladala.”
“Sawa baba.”

“Ila kesho nina safari ya kikazi kwa wiki nzima nikirudi tutaitoa, ila naomba iwe siri yako”
“Sawa baba.”
“Shika hii pesa itakusaidia kwa vitu vya hamu,” alimpa laki moja.
“Asante baba.”

Baada ya makubaliano walirudi ndani, sebuleni alikuwa Edna na mama yake. Jeska alipitiliza chumbani kwake kulala, hakuwa na hamu na kitu chochote kwa siku ile.
ITAENDELEA SIKU YA KESHO HAPA HAPA
TOA MAONI YAKO JUU YA SIMUIZI HII HAPACHINI
Like: www.facebook.com/2jiachie
Web: www.2jiachie.com

No comments

Powered by Blogger.