WEMA, DIAMOND WAZINDUA GARI KWA MAHABA
Endelea kulike: www.facebook.com/2jiachie
Tembelea: www.2jiachie.com
Tembelea: www.2jiachie.com
Stori: Richard Bukos
Mahaba nimalize!
Mastaa wapendanao, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ na Nasibu Abdul ‘Diamond
Platnumz’ wamesababisha tukio jipya kama kawaida yao, safari hii
wameishtua kadamnasi kwa kuzindua gari jipya kwa mahaba mazito ndani
yake, Ijumaa Wikienda lilinyaka mchongo mzima.
Mastaa wapendanao, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ wakikumbatiana kimahaba.
KAMA MUVI YA MAPENZI
Tukio hilo lililojiri kama
muvi ya mapenzi (romantic movie) lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita
kwenye Ukumbi wa Golden Jubilee uliopo Posta jijini Dar wakati Diamond
alipokuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa na kujizawadia ndinga aina
ya BMW X6 ambalo waliligeuza kuwa uwanja wa malovee wakati walipokwenda
kukabidhiwa na menejimenti yake ya Wasafi.
SHEREHE ILIVYOANZA
Awali, waalikwa sambamba na mastaa mbalimbali wakusanyika kwenye ukumbi huo na ilipofika saa 5:00 usiku, Diamond akiwa ameambatana na ubavu wake, Wema sambamba na mama yake mzazi, Sanura Kassim ‘Sandra’, waliingia na sherehe kuanza.
Awali, waalikwa sambamba na mastaa mbalimbali wakusanyika kwenye ukumbi huo na ilipofika saa 5:00 usiku, Diamond akiwa ameambatana na ubavu wake, Wema sambamba na mama yake mzazi, Sanura Kassim ‘Sandra’, waliingia na sherehe kuanza.
Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ wakila 'romansi'
TUKIO LA ZAWADI
Baada ya sherehe hiyo kupambwa
na matukio mbalimbali zikiwemo bendi za asili na wasanii, ulifika wakati
wa zawadi ndipo wageni waalikwa walipoanza kujinadi kupitia kipaza
sauti na mwishoni ikawa ni zamu ya menejimenti ya Wasafi ambayo ilitamka
kuwa inatoa gari hilo.
CHIEF KIUMBE NDANI
Pedeshee maarufu Bongo ambaye
kwa sasa amemrudia Mungu na kuwa mtu wa ibada, Chief Kiumbe hakuwa
nyuma katika eneo la zawadi, alifanya kufuru kwa kumrushia Diamond
mabunda ya dola za Kimarekani.
Mapaparazi wakidaka mchongo mzima laivu.
BABU TALE SASA!
Baada ya kufuru ya kurushiwa
‘madolari’, funga kazi ya zawadi ilimaliziwa na meneja wa msanii huyo,
Bab Tale aliyepanda jukwaani na kutangaza kuwa uongozi na familia ya
mwanamuziki huyo wamemnunulia gari jipya aina ya BMW X6 na kumtaka
ampeleke lilipoegeshwa amkabidhi.
WATU WASHUKA UKUMBINI
Kwa kuwa ukumbi huo upo
ghorofani, waalikwa wote sambamba na ‘birthday boy’, Dangote au Chibu,
walishuka kwa kutumia lifti za jengo hilo kwenda kuliona gari hilo
lililokuwa limeegeshwa katika ‘parking’ maalum.
Wakitoka kwenye ndinga(BMW) kuendelea na sherehe nzima ya bethidei.
MAMA AKABIDHI
Mbwembwe na mikogo ya kimahaba
kati ya Diamond na Wema iliendelea hadi pale mama Diamond, Sandra
alipomkabidhi mwanaye huyo funguo za gari hilo, wakazama ndani.
MAHABA MAZITO
Kitendo cha wawili hao kuingia
ndani ya gari hilo lenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 90 za
Kitanzania na kufunga milango, kilikuwa ni mwanya mzuri kwao kuanza
kuoneshana mahaba motomoto ambapo Diamond alimminia mtoto wa kike mabusu
ya kumwaga kisha kugandana kama kumbikumbi.
WATUMIA DAKIKA 20
Wapendanao hao walionekana
kuzidisha mahaba ambapo walijifungia ndani ya gari hilo kwa zaidi ya
dakika 20 na kufanya yao huku watu wapenda ‘ubuyu’ wakiwachungulia kwa
dirishani lakini wale waungwana waliamua kutazama pembeni wasione mambo
ya chumbani hadharani.
Baada ya kushuka ndani ya gari hilo, wawili
hao walikumbatiana tena na kurudi ukumbini ambapo burudani za kula na
kunywa ziliendelea.
KUMBUKUMBU MUHIMU
Hivi karibuni ilifanyika
bethidei ya Wema ambapo Diamond alimzawadia mpenzi wake huyo gari aina
ya Nissan Murano lenye thamani ya Sh. milioni 36 za madafu huku meneja
wa wema, Martin Kadinda akimpa BMW ambalo limeibua mjadala juu ya
uhalali wa meneja huyo kuwa na uwezo wa kulinunua.
Endelea kulike: www.facebook.com/2jiachie
Tembelea: www.2jiachie.com
Tembelea: www.2jiachie.com
(CREDIT: GPL)


Post a Comment