WEMA ACHEMKA KUMZAWADIA DIAMOND
STAA wa filamu Bongo, Wema Isaack Sepetu ameshindwa
kujibu mapigo ya mwandani wake Nasibu Abdul ‘Diamond’ kwa kutompa zawadi
yoyote katika sherehe ya siku yake ya kuzaliwa iliyofanyika kwenye
Ukumbi wa Golden Jubilee uliopo Posta jijini Dar.
“Hee halafu sijui kwa nini mpaka shughuli imeisha eti sijatoka kumpa zawadi baby wangu, sasa mbona hakuna aliyenikumbusha?” alisema Wema mwisho wa shughuli hiyo.
Staa wa filamu Bongo, Wema Isaack Sepetu akiwa na mwandani wake Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Kutokana na msanii Diamond kumpa zawadi ya gari aina ya Nisani Morano
mwandani wake huyo katika siku yake ya kuzaliwa japo hakuwepo na
kumuachia mama yake amkabidhi, mashabiki wengi walikuwa na kiu ya kutaka
kujua ni kipi ambacho Wema angemzawadia mpenzi wake katika siku hiyo
ili kudhihirisha upendo wake ikiwemo kwa mashabiki kama alivyofanya
Diamond.
Gari aina ya Nisani Morano iliyotolewa kama zawadi kwa Wema kutoka kwa 'Diamond'.
Mpaka shughuli inaisha watu mbalimbali walijitokeza kutoa zawadi zao
huku wengine wakimmwagia noti pamoja na menejimenti yake kumzawadia gari
aina ya BMW X6 lakini mwanadada huyo alishindwa kuonyesha makeke yake
mpaka mwisho wa shughuli na kubaki akijilaumu;“Hee halafu sijui kwa nini mpaka shughuli imeisha eti sijatoka kumpa zawadi baby wangu, sasa mbona hakuna aliyenikumbusha?” alisema Wema mwisho wa shughuli hiyo.
Post a Comment