USIKU WA KIGODORO - 8
Endelea kulike: www.facebook.com/2jiachie
Tembelea: www.2jiachie.com
ILIPOISHIA: James alikuwa bafuni akijimwagia maji, Lina akavuta simu yake na kuanza kusachi majina ili alipate la Kindaundau…
“Kindaundau…Kindaundau…Kindaundau…”
Akakumbana nalo limeandikwa…
“Kindaundau 2.”
KANYAGA NAYO…
Haraka sana akaisevu namba hiyo kwenye simu yake na kuirudisha simu mahali pake. Akajibalaguza akifikiria namba ambavyo atawasiliana na mtu huyo na kumwambia chondechonde asije akatumbua jipu kama si kidonda.
***
James alipotoka kuoga alijiweka kwenye kitanda na kumwita Lina mke wake ili ambembeleze kwa mahaba mazito kwa wakati ule ingawa pia, Lina alikuwa na mawazo kichwani ya kuangalia namna atakavyoaga na kurudi kwa mumewe Semi.
“Baby, njoo basi, unajua nimekumisi sana!”
“Hata mimi my love, nimekumisi pia.”
“Basi kumbe tumemisiana.”
“Ni kweli d.”
Kwa muda huo wakiwa juu ya sita kwa sita, James alikuwa fiti kimahaba lakini Lina alionekana kuwa chini kuliko kiwango chake jambo ambalo lilimshangaza sana James, akamuuliza huku mechi ikiendelea…
“Nahisi kama hauko sawa dear.”
“Ni kweli.”
“Kwa nini? Kuna nini kimetokea?”
“Ah! Basi tu, sijui leo nimeamkaje?!”
“Unajisikiaje kwani?”
“Mwili na akili vyote havipo sawasawa.”
“Unawaza nini?”
“Sijui tu.”
James aliposikia hivyo aliamua kujitahidi mwenyewe na alipomaliza safari yake akajiweka pembeni, naye akazama kwenye mawazo kuhusu Lina…
“Hii ndoa ipo haipo? Mbona kama sielewielewi…
“Mtu anasema ana mawazo, mawazo gani sasa wakati mimi nipo na ndiyo kwanza tupo kwenye ndoa mpya tena fungate.”
Lina aliiona hali ya James akajua naye hayuko sawa kama yeye, lakini alishindwa kumuuliza waziwazi.
“Lina,” aliita James…
“Abee.”
“Naomba leo tuondoke kwenda nyumbani, sina amani tena na hapa hotelini.”
Lina alishtuka sana lakini kwa siri ili asijulikane, aliamini kitendo cha kwenda nyumbani kwa James ndiyo mambo yatakuwa wazi mapema sana jambo ambalo hakulipenda…
“Kuna nini kimetokea baby?”
“Nimeamua hivyo tu.”
“Ndiyo umeamua, kuna nini?”
“Hakuna kitu Lina, fuata ninayosema.”
“Oke, sawa! Nimekuelewa!”
“Kama umenielewa vizuri, naomba jiandae kwani tunaondoka muda huuhuu, sioni sababu ya kupoteza muda.”
Lina alijiandaa, akili ilizidi kuvurugika, aibu aliiona mbele ikimnyemelea, angesema nini…
“Hivi likibumbuluka nitasema nini mimi?” alijiuliza mwenyewe.
Walishuka hadi kwenye gari la kifahari la James, wakazama humo na kuondoka hadi nyumbani kwa James ambapo Lina alipokelewa kwa shangwe na wafanyakazi wa ndani wa James wakijua amekwenda rasmi na si kama mchumba. Salamu zikawa nyingi, karibu za kumwaga!
Moyoni Lina alisema…
“Mh! Mngejua nimelikoroga wala msingenishobokea, yaani nyie mko huru kuliko mimi hapa.”
Bado Lina alikuwa na mawazo ya jinsi gani ataaga kurudi kwa Semi. Aliona afadhali walivyokuwa hotelini kuliko pale nyumbani.
“Bosi samahani, alikuja Bryan, akasema ukija muonane, amepata ule mzigo,” alisema mlinzi wa getini akimwambia James.
James aliachia tabasamu kusikia maneno hayo, palepale alimuaga Lina kwamba anaondoka atarudi ndani ya dakika 50 mpaka saa moja.
“Sawa baby.”
***
Baada ya James kuondoka, Lina aliingia chumbani, akatoa simu yake huku akifurahi kwamba atapata nafasi ya kuongea na Kindaundau sasa, akapiga simu hiyo lakini haikuwa hewani!
“Mungu wangu! Au Kindaundau 2 niliyoichukua haitumiki kwa sasa?” alijiuliza mwenyewe Lina huku mapigo ya moyo yakiendelea kumdunda.
***
Katika kuelekea nyumbani kwa Bryan, James alipita mahali akakutana na Eg, rafiki wa Lina akiwa na rafiki zake wawili, wamejikwatua hao mfano hakuna, akasimamisha gari ili kumsalimia…
“Shemu vipi?”
“Shwari shemeji yangu, hajambo Lina?”
“Hajambo, wapi shemeji mbona umependeza sana?”
“Tunakwenda kwenye kikao cha hawa rafiki zangu, kinafanyika Mikocheni.”
“Ooo! Sawa! Mgonjwa anaendeleaje?”
Eg ndiyo akashtuka kusikia habari ya mgonjwa, akakumbuka dili lake na Lina. Kwa jinsi alivyojipara alishindwa kusema mgonjwa bado kalazwa, angeonekana hajali, akasema…
“Mgonjwa katoka mchana wa leo shemeji, hivi hata Lina hajui lolote.”
“Ala! Afadhali, poleni sana,” alisema Lina huku akiingiza mkono kwenye mfuko wa shati na kutoa shilingi elfu hamsini, akampa…
“Ongezea nauli shemeji.”
“Jamani shemeji, asante sana jamani, Mungu akubariki sana.”
“Usijali shemeji.”
***
Baada ya kuondoka tu, Eg akampigia simu Lina ili kumpa tukio hilo…
Sasa kaondoka, akirudi nitakwambia ili unipigie simu usingizie yule mgonjwa, kwamba unaniomba nikalale naye ili wewe urudi nyumbani, niweze kurudi kwa Semi la sivyo mwenzio naumbuka…”
“Shoga pole, haitawezekana,” alijibu kwa mkato Eg…
“Eh! Eg, kwa nini? Ni wewe au mwingine?”
“Yaani namaanisha tumekutana na shemeji sasa hivi?”
“Yupi?”
“Si James. Sasa hivi, tunaagana ndiyo na mimi nikaamue kukupigia simu. Amesema anakwenda wapi sijui, lakini kwa rafiki yake.”
“Mh! Alikuuliza kuhusu mgonjwa?”
“Ndiyo swali lake la kwanza. Kauliza vipi mgonjwa shemeji? Na mimi kwa jinsi nilivyovaa na kujipata leo nakwenda kwenye kile kikao cha akina Mama Mumba, nikajikuta nimemwambia mgonjwa katoka.”
“Ayaaaa! Umeniua Eg, nitadanganya nini sasa kwa James mpaka anikubalie kutoka na kwenda kulala hukohuko mpaka kesho?”
“Aisee! Sijui iweje! Halafu mbaya zaidi nilimwambia kabisa kwamba nakwenda kikao cha harusi.”
Lina alikata simu kwa hasira. Alimchukia Eg. Aliamini anaweza kuwa chanzo cha lolote litakalotokea kwake na James na Semi.
“Khaa! Sasa huyu mbona amekata simu?” alijihoji Eg akianza kuingiwa na wasiwasi.
Kwa upande wake, Lina aliamua liwalo kwa siku hiyo na liwe, alishajua kisingizio hakuna tena. Aliamua kupanda kitandani na kujipumzisha huku akiwaza sana kuhusu hatima yake.
“Sijui nini hatima ya hili sakata langu, nahisi Eg naye ameanza kunikimbia, ni kwa nini amwambie anakwenda kwenye kikao cha harusi wakati anajua yeye ndiyo tegemeo langu la kuondokea kwa James?”
***
James alirejea nyumbani hapo saa kumi juu ya alama. Alipoingia ndani tu aliita kwa sauti ya juu…
“Baby wa James.”
Lina alikuwa chumbani kwa hiyo hakusikia, ila mfanyakazi mmoja wa ndani alimwambia bosi wake huyo kwamba, Lina alikuwa chumbani.
Alikwenda chumbani na kusukuma mlango, akazama ndani na kwenda kumkumbatia Lina…
“Baby nimekumisi sana…”
“Mmmh! Jamani baby, hata mimi. Ila sina amani sana dear…”
“Kisa nini tena?”
“Nimetumiwa meseji mama anaumwa sana nyumbani, Korogwe! Si unakumbuka hata kwenye harusi yangu nilikwambia hatakuja?”
“Ndiyo…sasa?”
“Da! Sijui niende?”
“Ah! Lina mke wangu, suala la mama kuumwa ni la kuamua uende au usiende? Unatakiwa kwenda, ikibidi hata kesho asubuhi na mapema.”
“Ooh! Nashukuru kwa ruhusa baby, nilijua hutapenda ukizingatia tumetoka kwenye ndoa juzi tu.”
“Kutoka kwenye ndoa si ishu Lina, uzima wa mama ni wa mbele. Hata kama tungekuwa tumefunga ndoa leo, usiku ukaambiwa mama anaumwa, ingebidi kwenda.”
***
Usiku uliingia, Lina aliamua kuzima simu ili Semi asimpate moja kwa moja. Alijua angepigiwa na angeshindwa kujibu au kudanganya mbele ya James…
“Lakini sasa hatima yake ni nini kama hatanipata hewani? Je, atanitafuta kwa Eg? Na kama atakwenda kule halafu asinikute, nini kitafuata? Da! Huu mzigo ni mkubwa sana kwangu, vigumu kuubeba,” aliwaza moyoni Lina kiasi kwamba, James aligundua hilo…
“Baby, pungumza mawazo. We kesho nenda, asubuhi sana mimi nitakupeleka stendi. Kama ungekuwa unaweza kuendesha gari ungetumia gari moja,” alisema James huku akiwa anamshikashika sehemu mbalimbali mkewe huyo.
Lakini Lina alikumbuka kitu, akawasha simu ili amtumie meseji Eg kumshawishi wapange uongo mpya kwa mumewe, Semi.
Hata hivyo, kabla hajamtumia meseji yoyote, meseji iliingia kwenye simu yake, ilitoka kwa mumewe…
“Baby, pole na kazi! Nimekupigia simu haupo hewani, pole. Mimi niimepata dharura, nakwenda Iringa na wale jamaa wauza madini, tunarudi keshokutwa. Please take care.”
Lina alihisi ameona nyota ya bahati kwa kupata ujumbe ule kwani ndiyo sababu pekee iliyokuwa na uwezo wa kumpa nafasi ya kulala nje ya nyumbani kwake kwa siku hiyo.
Alimwangalia James kwa macho yaliyojaa furaha, akamkumbatia na kumsogeza kifuani pake kisha kuanza kumpa mabusu mfululizo.
ITAENDELEA SIKU YA KESHO
Endelea kulike: www.facebook.com/2jiachie
Tembelea: www.2jiachie.com

Post a Comment