UNANG'ANG'ANIA KUPENDA USIKOPENDEKA ILI IWEJE? - 2
WIKI iliyopita tuliianza mada hii ambayo inatufundisha juu ya kutong’ang’ania kupenda pasipopendeka. Unampenda mtu wakati yeye moyo wake haupo kwako, utateseka bure wakati mwenzako wala hayajui mateso unayopitia.
Endelea kulike: www.facebook.com/2jiachie
Tembelea: www.2jiachie.com
Utaambulia maumivu yatakayokugharimu kwa kiasi kikubwa usipokuwa makini, leo tumalizie mada hii kwa kutazama madhara ya kung’ang’ania penzi hilo.
TUENDELEE…
Uking’ang’ania kupenda sehemu usiyopendwa kitakachofuata hapo ni kuanza kujiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu.
Yawezekana alikuwa akikupa moyo kutokana na majibu yake na kukufanya uendelee kuwa karibu yake kwa muda mrefu lakini kuna wakati utachoka, utaanza kujijengea maswali yasiyokuwa na majibu.
Utajiuliza kwamba, inamaana muda wote ule niliokuwa niko naye alikuwa akicheza na akili yangu? Kwa nini lakini akufanyie hivyo? Utawaza kwamba ni bora angekukataa mapema kuliko kuendelea kukufurahia machoni wakati moyoni anakung’ong’a.
Kipindi hicho ndicho ambacho mtu ni rahisi kusikia amefanya maamuzi ambayo yanaweza kumgharimu. Wapo wanaoamua kujiua au kumuua yule aliyempenda eti kwa sababu tu ametendwa kitu ambacho si sahihi. Ni vyema kila mmoja akatambua umuhimu wa kupenda pale unapopendwa ili kuepusha maumivu mazito mwishoni.
Wakati wa kufanya uchaguzi, wakati wa kumtafuta mchumba ndiyo wakati ambao watu wanapaswa kuwa makini. Ni vigumu kuzizuia hisia lakini tunapaswa kuzidhibiti. Macho yanaona, yanapeleka ujumbe katika moyo kwamba hapa nimependa na akili inaamua kwamba ngoja nirushe ndoano.
Unarusha ndoano, unakutana na kisiki. Japo mara nyingi kwa desturi za Kiafrika mwanaume ndiye anakuwa wa kwanza kumpenda mwanamke na kuthubutu kumwambia kisha baadaye mwanamke naye anapokea na kuzama penzini lakini si kila utakayempenda naye atakupenda pia.
Endelea kulike: www.facebook.com/2jiachie
Tembelea: www.2jiachie.com
Kuna athari nyingi za kung’ang’ania kupenda sehemu ambayo hupendwi. Hapa chini nitakuonesha baadhi ya athari ambazo mtu huzipata pale anapopenda sehemu ambayo hapendwi.
Kuishi kwa hofu
Mtu anapompenda mtu na kuweka asilimia zake nyingi kwamba atafanikiwa, akikosa huwa anatawaliwa na hofu. Hofu huwa kubwa, anakuwa mtu wa kujishtukia, anajihisi ana kasoro kumbe kiuhalisia wala hana tatizo lolote.
Kitendo cha kukataliwa kwake hugeuka kuwa hofu, inamtesa. Tena hofu huongezeka hususan kama mhusika aliyemkataa wanaonana naye mara kwa mara.
Pasipokuwa na sababu, hofu hiyo inaweza kudumu kwenye akili yake kwa muda mrefu. Baadhi ya watu wamekuwa wakibadilisha hata njia kumkwepa yule ambaye alimkataa. Anahisi atamdharau. Kumbe mwenzake wakati huo anakuwa ameshasahau kama aliwahi kutamkiwa kuwa anapendwa, haoni hata haja ya kuliwaza
suala hilo maana halipo akilini mwake. Akili na mawazo yake yote huwa yanakuwa kwa mpenzi wake.
Kuharibu majukumu
Hii pia ni athari nyingine ya mtu kupenda asipopendwa. Akili yake inakufa kwa kutokubaliana na jibu kwamba hapendwi. Kama ni mfanyakazi, mwanachuo au hata mfanyabiashara, mambo hayaendi tena sawa wakati huo.
Ndiyo wakati ambao kama ni bosi ofisini, utendaji wa kazi utashuka. Ni rahisi hata wafanyakazi wake kuathirika na jambo hilo. Mambo yote yatakwenda ovyoovyo eti kisa tu amekataliwa na mtu.
Kukonda
Mawazo yanapokuwa mengi, kinachofuata huwa ni mtu kukonda. Pasipokuwa na sababu za msingi, unaanza kudhoofu mwili kwa sababu ya kukataliwa. Akili yako inaamini kwamba umpendaye ndiye huyo na hakuna mwingine unayeweza kumpenda.
Nini cha kujifunza?
Unapaswa kukubaliana na matokeo hususan pale unapoona hakuna muelekeo wa unayemtaka kukuelewa. Uvumilivu unatakiwa wakati unamsaka mchumba lakini upande wa pili unapaswa kukubaliana na matokeo kwamba yawezekana ukapenda lakini usikubaliwe.
Mtu anakukataa kwa vigezo vyake, yawezekana anaye anayempenda. Kelele zako zote za kumshawishi zitakuwa kazi bure. Yawezekana hamuendani kisura, tabia na vitu vingine, usilazimishe!
Mwisho.
Endelea kulike: www.facebook.com/2jiachie
Tembelea: www.2jiachie.com

Post a Comment