ad

ad

LAVEDA AFUNIKA UFUNGUZI WA BIG BROTHER HOTSHOTS


Irene 'Laveda' akionyesha ufundi wa kutumia saxophone wakati akitoa shoo kwenye ufunguzi wa Big Brother Hotshots.
MSHIRIKI wa shinadano la Big Brother Hotshots kutoka Tanzania, Irene 'Laveda' amefunika vilivyo katika shoo ya ufunguzi wa shindano hilo usiku huu nchini Afrka Kusini.
Laveda ameongoza kwa kura zilizopigwa na watu waliokuwa mjengoni akipata asilimia 85 kutokana na shoo yake kali aliyotoa akicharaza vilivyo saxophone na kuwafunika washiriki wengine 25 kutoka mataifa mengine ya Afrika.
Kwa ushindi huo, Laveda hatakuwemo katika orodha ya washiriki watakaopigiwa kura kwa ajili ya kutolewa mjengoni kuanzia wiki ijayo.

No comments

Powered by Blogger.