MSIBA TENA: MSANII SHERRY MAGALI AFARIKI DUNIA!
Msanii
nyota wa filamu nchini Sherry Charles Magali akiwa hoi hospitalini
Wodi Namba 8 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro katika picha
hii iliyopigwa na mwandishi wetu Ijumaa iliyopita, Okt 17, 2014.
Msanii
huyo, amefariki leo saa nne asubuhi baada ya kuugua kwa muda mrefu. Kwa
mujibu wa familia, taarifa zaidi za mazishi zitatolewa baadae. Global
Publishers imekuwa ikifuatilia hali ya msanii huyu na kuwajulisha
mashabiki wake mara kwa mara. Mara ya mwisho kuandika habari zake
ilikuwa Februari 21 mwaka huu wakati alipokuwa amelazwa kwenye hospitali
Kilimani maeneo ya Big Brother jijini Dar chini ya kichwa cha habari MTOTO WA MAGALI HOI KITANDANI.
Global Publishers inatoa pole kwa wafiwa na kumtakia marehemu alale pema- ameen!
PICHA NA STORI: DUSTAN SHEKIDELE - MOROGORO
Post a Comment