GARDNER ATAKA JIDE AELEZE UKWELI JUU YA NDOA YAO
Habari ya mjini katika ulimwengu wa mastaa Bongo ni kitendo cha
mtangazaji mwenye jina kubwa wa Kipindi cha Maskani cha Redio Times FM,
Gardner G Habash ‘Kepteini’ kutaka mwanamuziki Judith Wambura Mbibo
‘Jide’ ndiye aeleze ukweli juu ya ndoa yao.
Mtangazaji wa Redio Times FM, Gardner G Habash ‘Kepteini’
Akizungumza kwenye Kipindi cha Mkasi kinachorushwa hewani kupitia
Televisheni ya EATV chini ya ‘hosti’ wake, Salama Jabir, Jumanne
iliyopita, Gardner alikataa kuzungumzia ndoa yake inayodaiwa kuvunjika.
Endelea kulike: www.facebook.com/2jiachie
Tembelea: www.2jiachie.com
Tembelea: www.2jiachie.com
Pamoja na mambo mengine ambayo aliyajibu kwa ufasaha, Gardner
alipoulizwa juu ya habari zinazozungumzwa mtaani kuhusu kuvunjika
uhusiano wake na Jide au Lady Jaydee, aligoma kulizungumzia kwa kigezo
kwamba kipindi hicho kilimhusu yeye tu.
Mwanamuziki wa Bongo fleva kitambo, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’
Mtangazaji huyo alikwenda mbele zaidi kwa kumwambia Salama kwamba
amwite Jaydee kwenye kipindi hicho ili alielezee jambo hilo kwa
undani.Gardner na Jaydee ambao walifunga ndoa mwaka 2005, wamekuwa
wakidaiwa kuwa hawapo pamoja tena huku majukumu ya mtangazaji huyo
ambaye alikuwa meneja wa mwanamuziki huyo yakielea.
Kupitia kipindi chake cha Diary of Lady Jaydee kilichokuwa
kikisimamiwa na Gardner ambacho sasa kinaongozwa na ndugu wa msanii huyo
aitwaye Wakazi, Jumapili iliyopita Jide alionekana kwenye harusi ya
ndugu yake aitwaye Lameck Mbibo ‘Dabo’ ambaye pia ni msanii wa Dance
Hall akiwa mpweke bila mumewe kama ilivyozoeleka.
Endelea kulike: www.facebook.com/2jiachie
Tembelea: www.2jiachie.com
Tembelea: www.2jiachie.com

Post a Comment