DENTI AJICHOMA KISU KWA MADAI YA USALITI WA MAPENZI
Moza Kasim Mohemed akiwa hoi baada ya kujichoma kisu cha tumbo.
Stori: Musa Mateja LOO!
Mwanafunzi wa Chuo cha T.I.A tawi la mkoani Singida, Moza Kasim Mohemed
(20) ambaye ni mkazi wa jijini Dar es Salaam, amejichoma kisu tumboni
kwa madai ya kuchoshwa na usaliti wa mpenzi wake aitwaye Joel ambaye pia
ni mwanafunzi wa chuo hicho.
Tukio hilo la kushangaza lilitokea usiku wa kuamkia Oktoba 10, mwaka
huu maeneo ya Jovena katika Hosteli za Miami ambapo Moza alikuwa akiishi
na mpenzi wake huyo.
Chanzo chetu kilidai kuwa, siku hiyo muda mfupi kabla ya tukio hilo
kulitokea kutoelewana kwa wawili hao ambapo majirani walimsikia Joel
akimtuhumu Moza kwamba amekuwa msaliti na anahisi ana simu nyingine ya
ziada ambayo anaitumia yeye akiwa hayupo.
Muonekano wa kisu hicho baada ya kujichoma.
Timbwili lilisikika kwa muda mrefu kiasi
kwamba ilibidi majirani waanze kuchungulia dirishani na wakamsikia Moza
akimwambia Joel kwamba, kwa vile hamwamini hadi anafikia kumpiga bora
ajichome kisu afie mbali.Kwa mujibu wa chanzo chetu, Joel naye alisikika
akimjibu Moza kwa kumwambia kama dhamira yake ni hiyo, basi ajichome
tu.
Akiwa hospitalini baada ya kutolewa kisu tumboni.
Malumbano hayo yaliendelea kuchukua ukurasa mpya ambapo Joel
aliendelea kumpa kibano na baadaye alimuacha na kutoka nje, baada ya
dakika chache zikasikika kelele za ajabu kutoka kwa Moza ambapo majirani
ambao ni baadhi ya wanafunzi wenzake wakatoka na kuingia chumbani na
kumkuta akigalagala na damu zikimvuja huku kisu kikiwa tumboni.
“Hawa watu walikuwa na tabia ya kukwaruzana mara kwa mara na Joel
alikuwa akimpiga yanaisha ila siku hiyo ilikuwa ni mzozo wa hatari,
baada ya tukio watu walijaa lakini kila mtu akawa anaogopa kumgusa Moza,
Joel alipata ujasiri yeye na rafiki yake wakambeba na kumkimbiza
Hospitali ya Mkoa wa Singida,” kilisema chanzo.
Hostel aliyokuwa anaishii Moza Kasim Mohemed .
Kikaendelea: “Jana (juzi Jumapili) tulikwenda hospitali kumsalimia,
tulikuta ameshatolewa kisu na ameshashonwa, hali yake inaendelea vizuri,
ila habari ya mjini Singida kwa sasa ni juu ya tukio hilo, hata
tulipofika hospitali tulikuta wanafunzi wengi.”

Post a Comment