WELBECK APIGA BAO ZOTE MBILI, ENGLAND IKIISHINDA USWISS 2-0 NYUMBANI
Mshambuliaji mpya wa
Arsenal, Danny Welbeck, ameibuka shujaa wa England baada ya kufunga mabao yote
mawili na kuipa England ushindi wa 2-0 ikiwa ugenini.
Katika
mechi hiyo iliyomalizika mjini Basle, Switzerland, wenyeji wamelala kwa
mabao hayo mawili ya Wilbeck katika mechi ya kuwania kufuzu michuano ya
Euro.
Welbeck
alianza kufunga bao lake la kwanza katika dakika ya 59 baada ya nahodha
Wayne Rooney kushirikiana vizuri na winga hatari, Raheem Stelring.
Wakati
wenyeji wakiwa wanajitahidi kusawazisha, Welbeck tena alitupia bao la
pili katika dakika ya 90 na kuihakikishia England ushindi.
Welbeck ametua Arsenal kwa kitita cha pauni milioni 16 akitokea Man United.
Post a Comment