ad

ad

RICHARD KIEL 'MENO YA CHUMA' WA JAMES BOND AFARIKI DUNIA

Mwigizaji  Richard Kiel 'meno ya chuma' enzi za uhai wake.
MWIGIZAJI wa Marekani, Richard Kiel aliyecheza filamu za James Bond akiwa na meno ya chuma amefariki dunia akiwa na miaka 74 jijini California.

Richard Kiel (kulia) akimkaba Roger Moore katika filamu ya 'The Spy Who Loved Me'.
Kiel amefariki akiwa Kituo cha Afya cha Saint Agnes Fresno jijini California nchini Marekani alipokuwa akitibiwa.

Richard, mwezi Mei 2013 jijini London.
Kifo chake kimekuja ikiwa ni wiki moja baada ya kuvunjika mguu wake.
Kiel anakumbukwa sana katika filamu mbili za James Bond ya 'The Spy Who Loved Me' ya mwaka 1977 na 'Moonraker' ya 1979.

No comments

Powered by Blogger.