OBAMA: EBOLA NI TISHO KWA USALAMA
Rais wa Marekani Barack Obama, amelitaja janga la Ebola katika kanda ya Afrika Magharibi kuwa tisho la usalama wa kimataifa.
Obama ametoa kauli hiyo huku akitangaza jukumu la Marekani katika kupambana na janga la Ebola.
''Dunia
nzima inaelekeza macho ya kutaka msaada kwa Marekani,'' alisema Rais
Obama, lakini akaongeza kwamba mlipuko unaoshuhudiwa wa janga hilo,
unahitaji kushughulikiwa na jamii ya kimataifa.
Hatua ambazo
Marekani imetangaza ikiwemo kupeleka wanajeshi 3,000 katika kanda hiyo
kupambana na Ebola na kujenga taasisi za afya.
Ugonjwa wa Ebola umewaua watu 2,461 mwaka huu, kulingana na shirika la afya duniani (WHO).
Tangazo hilo limetolewa huku
Maafisa wa Umoja wa Mataifa wakitaja ugonjwa huo kuwa janga la kimataifa
na pia janga kubwa kushuhudiwa kwatika miaka ya hivio karibuni.
Pesa
za msaada zinazohitajika kupambana na Ebola zimeongezeka mara kumi
katika mwezi mmoja uliopita na kwamba dola bilioni ndizo zinahitajika
kukabiliana na ugonjwa huo.
Hii ni kwa mujibu wa mratibu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ebola.
Rais
Obama amezitaka nchi zingine kuongeza kasi ya kusaidia katika vita
dhidi ya Ebola kwani kukithiri na kuendelea kuenea kwa ugonjwa huo
kutasababisha changamoto za kiuchumi , kiusalama na kisiasa.
CREDIT: BBC SWAHILI

Post a Comment