MUSEVENI AMFUTA WAZIRI MKUU KAZI
Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uganda, Amama Mbabazi.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni amemfuta kazi waziri mkuu na mwandani wake Amama Mbabazi.
Kwenye
taarifa yake Museveni alimshukuru bwana Mbabazi kwa mchango wake kwa
nchi ya Uganda ambapo pia alimtangaza mrithi wake Ruhakana Rugunda
ambaye sasa anasubiri kuidhinishwa na bunge.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni.
Bwana Mbabazi alikuwa anatarajiwa na wengi kuwa mpinzani wa Museveni katika uchaguzi ujao.
Rais
Museveni ametangaza kuwa amemteua daktari Ruhakaan Rugunda kama waziri
mkuu mpya ambaye ataaanza kushikilia wadhifa wake mara moja.
Waziri mkuu mpya wa Uganda, daktari Ruhakaan Rugunda.
Waziri
mkuu anayeondoka Amama Mbabazi alionekana kuwa angemrithi rais Museveni
lakini miaka mitatu ambayo amehudumu katika wadhifa huo uhusiano kati
yake na Museveni haujakuwa mzuri.
Mapema mwaka huu chama
kinachotawala kiliidhinisha azimio kikisema kuwa rais Museveni ambaye
amekuwa uongozini kwa muda wa miaka 28 atakuwa mgombea wa pekee kwenye
uchaguzi wa mwaka 2016.
Hata hivyo mkewe Mbabazi ambaye pia ni afisa wa cheo cha juu chamani amesema kuwa mumewe ameonewa.
Waziri mkuu mpya ambaye ni mtaalamu wa masuala ya afya awali alikuwa amehudumu kama waziri wa afya.
(CREDIT: BBC SWAHILI)



Post a Comment