ad

ad

MOYO WANGU BADO UNAVUJA DAMU - 05




“Najua kwamba umenikatalia ombi langu la kuwa nawe, yaani hadi hili la kula nawe chakula unanikatalia. Tafadhari Simon, nakuomba” Natasha alimwambia Simon.
   Tayari machozi ya uongo yakaanza kudondoka kutoka katika macho ya Natasha. Alijioa kuwa na kila sababu ya kudondosha machozi hayo kwani aliamini kwamba ni lazima Simon angemunea huruma na kukubaliana na ombi lake. Simon alibaki akimwangalia Natasha kwa macho ya huruma, tayari machozi ambayo yalikuwa yakimtoka Natasha yakaanza kuumba huruma moyoni mwake.
   “Sawa. Ila naomba uniahidi kit kimoja” Simon alimwambia Natasha.
   “Kitu gani?”
   “Kwamba hatutofanya kitu chochote kile na wala kuniambia chochote kuhusu mapenzi” Simon alimwambia Natasha.
   “Nakuahidi”
   “Sawa” Simon alijibu na kisha kuondoka huku wakipanga kwenda kula chakua cha usiku katika baa moja iliyokuwa Kinondoni.
                                                                             ***********
   Bado macho ya Walter yalikuwa yakiliangalia jina la Baby Beatrice ambalo lilikuwa likionekana katika kioo cha simu yake. Alitamani aipokee simu ile lakini kwa upande mwingine alikuwa akihofia kufanya hivyo. Hakutaka kumuudhi Jalia, bado alikuwa akimpenda na kumuhitaji zaidi ya jinsi alivyokuwa akimuhitaji Beatrice.
   Alichokifanya ni kuikata simu ile na kuitupa pembeni. Jalia akaonekana kushtukia kitu lakini hata kabla akili yake haijakaa sawa, akashtukia akipigwa na busu zito shavuni na kisha kulazwa pale kitandani. Walter akaanza kumwangalia Jalia usoni kwa macho yaliyojaa mahaba.
   “Uko tayari?” Walter aliuliza.
   “Tayari kufanya nini?”
   “Usijifanye mtoto mpenzi. Hebu nijibu basi” Walter alimwambia Jalia.
   Jalia hakujibu chochote kile, alibaki akimwangalia Walter huku tabasamu likionekana usoni mwake. Walter alikwishajua kwamba tabasamu lile lilikuwa likimaanisha jibu la ‘ndio’. Alichokifanya ni kuanza kumvua nguo ile ya ndani ambayo alibaki nayo na kisha mchezo mzima kuanza hapo.
   Ilikuwa ni kazi kubwa, Walter alijitahidi kadri ya uwezo wake lakini akaonekana kuzidiwa nguvu kabisa. Muda wote alikwa akishambuliwa yeye. Mpaka mchezo unamalizika, alikuwa hoi huku akiwa ahamini kama msichana kama Jalia angeweza kufanya mambo kama yale.
   “Kuna haki ya kumsahau Beatrice” Walter alijisemea.
   Hawakutaka kuendelea kukaa hotelini, walichokifanya kwa wakati huo ni kutoka na kisha kuanza kumpeleka Jalia nyumbani kwao. Njia nzima Walter alikuwa akionekana kuwa na furaha, kwa wakati huo,Beatrice alikuwa amesahaulika kabisa.
   Mapenzi yake yakaaanza kuhama taratibu. Jalia akaanza kuonekana mtu muhimu katika maisha yake. Hakutaka tena kuwa na Beatrice tena  na alitamani sana amwambie ukwel juu ya uamuzi ambao alikuwa ameufikia lakini aliona vigumu kufanya hivyo.
   Alijiona kuhitaji muda zaidi wa kutaka kufanya ule uamuzi ambao alikuwa akiuona kufaa. Alijiona kutokukurupuka katika kufanya uamuzi ule. Ni kweli hakumpenda Beatrice kwa kipindi hicho lakini itampasa kujifanya kumpenda ili asiweze kushtukia kitu chochote kile.
   Hakujua maisha yangekuwaje kwa Beatrice ambaye moyo wake wote alikuwa ameutoa kwake yeye. Ni kweli kwenye mapenzi usaliti mara kwa mara hutokea lakini moyo wake kwa kipindi hicho ulikuwa mgumu kuuamua uamuzi ule ambao alikuwa akitaka kuuchukua.
   Aijulikana nyumbani kwa kina Beatrice. Kila mtu alikuwa akionekana kumkubali. Alijiona kutaka kucheza faulo, tena faulo mbaya ambayo ingemuweka mtu fulani nje ya mchezo kwa muda mrefu. Kila wakati alikuwa akijiuliza namna ambayo alitakiwa kuanza kumwambia Beatrice kwamba kwa sasa hakuwa moyoni mwake.
   Alijaribu kuvuta picha ya namna Beatrice atakavyokuwa. Hakutaka kuiona hali ile ambayo itampata Beatrice Alimuonea huruma kwa kuwa aliyajua maisha ambayo alikuwa akiishi nyumbani kwao. Kitendo cha kumwambia juu ya jinsi moyo wake ulivyojisikia kulimaanisha kwamba Beatrice angekuwa katika hali mbaya zaidi.
   “Acha nimwambie. Usaliti ni sehemu ya mchezo huu wa mapenzi” Walter alijisemea huku akiingia garini pamoja na Jalia.
                                                                               ******
   Siku hiyo walipanga kukutana katika Pub ya Mamba saa mbili usiku kwa ajili ya kupata chakula. Natasha alionekana kuwa na hamu ya kuonana na Simon mahali hapo. Saa moja na dakika tano, tayari alikuwa akilipaki gari lake karibu kabisa na Pub ya Mamba.
   Akateremka na moja kwa moja kuanza kupiga hatua kuifuata baa ile na kisha kuingia na kuchagua meza iliyokuwa katika sehemu iliyokuwa na giza. Akayapeleka macho yake katika kila kona ndani ya baa ile huku lengo lake kuona kama Simon alikuwa amefika, hakumuona.
   Natasha akamuita mhudumu na kisha kuagiza kinywaji. Akaletewa kinywaji kile na kuanza kunywa. Mara kwa mara alikuwa akijaribu kuipiga namba ya simu ya Simon lakini simu wala haikuwa ikipokelewa. Natasha alionekana kukasirika lakini kwa sababu yeye ndiye aliyekuwa na shida, ilimbidi kuvumilia.
   Muda ulizidi kwenda zaidi na zaidi. Baada ya saa moja kupita, Simon akaanza kuingia ndani ya baa ile. Akayapapeleka macho yake katika kona mbalimbali mahali pale, macho yake yakatua kwa Natasha ambaye alikuwa akimuita.
   Simon akaanza kupiga hatua kumfuata Natasha ambapo mara baada ya kumfikia, akakaa katika kiti kingine kilichozunguka meza ile. Simon hakutaka kuongea kitu, alikuwa kimya huku akimwangalia Natasha ambaye akaagiza chakula kiletwe mahali hapo.
   “Unatumia kinywaji gani?” Nataha alimuuliza Simon.
   “Chochote, isipokuwa pombe” Simon alimwambia Natasha na kisha Pepsi kuletwa mahali hapo.
   Natasha alikuwa kimya, kichwa chake kilikuwa kikifikiria ni kwa jinsi gani angeanza kuongea kile kitu ambacho kilimfanya kumuita Simon mahali hapo. Natasha akaona ni afadhali akae kimya kwanza, alitaka kwanza wamalize kula na ndipo hapo atakapoanza kumwambia ukweli.
   “Unaniangalia sana Natasha. Unanifanya hadi naogopa” Simon alimwambia Natasha mara baada ya kumaliza kula.
   “Kila mtu huangaliwa ila jaribu kutafakaria kwa aina gani ya macho ambayo ninatumia kukuangalia” Natasha alimwambia Simon. Simon akaachia tabasamu pana.
   Natasha akajina kuwa mbali na Simon, alichokifanya kukisogeza kiti chake karibu na Simon na kisha kutulia. Natasha akajiona kusisimka zaidi mara baada ya mwili wake kugusana na mwili wa Simon ambaye alikuwa ametulia huku akiangalia kila hatua ambayo Natasha alikuwa akipitia.
   Natasha alibaki kimya kwa muda huku akijaribu kuunyonganyonga mwili wake katika staili ya mahaba, alionekana kuanza kushikwa na ashki kubwa ya mahaba. Simon hakutaka kuongea kitu, alichotaka kukiona ni kitu gani kingefuatia baada ya hapo.
   “Unautesa moyo wangu Simon. Kwa nini lakini?” Natasha alimuuliza Simon.
   “Nautesa? Kivipi?” Simon aliuliza huku akijifanya kutokujua kitu chochote kile.
   “Ni mara ngapi unataka nikwambie kwamba nakupenda?” Natasha aliuliza kwa sauti ya chini iliyojaa mahaba.
   “Na wewe ni mara ngapi unataka nikwambie kwamba nina mtu nimpendae?” Simon nae aliuliza.
   “Nafahamu Simon. Mwanaume mzuri kama wewe ni vigumu kuwa peke yako. Naomba unipe nafai moyoni mwako. Hata kuwa mtu wa pili nadhani nitaifurahia nafasi hiyo” Natasha alimwambia Simon.
   “Naogopa kuumiza moyo wa mtu Natasha. Mtu anapojitolea kukupenda kwa moyo mmoja halafu unakuja kumsaliti, unafikiri inapendeza kweli?” Simon aliuliza.
   “Inapendeza kama hatojua ila haipendezi kama akijua” Natasha alijibu.
   “Nimekuelewa. Tufanye haipendezi kwa kuwa atajua” Simon alimwambia Natasha.
   “Atajuaje? Utamwambia?”
   “Haujui kwamba mapenzi kikohozi?” Simon alimuuliza Natasha.
   “Nafahamu”
   “Nashukuru kwa kufahamu” Simon alimwambia Natasha.
   Simon hakutaka kuendelea kubaki mahali hapo. Tayari aliona kila dalili kwamba Natasha angeweza kutumia kila hila kumlaghai mahali pale. Simon alijua asilimia mia moja kwamba angeweza kupatwa na udhaifu na kumkubalia Natasha kie ambacho alikuwa akikihitaji kutoka kwake.
   Hakutaka kuendelea kumuua nyani huku akimwangalia usoni. Akasimama na kisha kuanza kuondoka. Natasha hakukubali kushindwa, hakutaka kabisa kumuacha Simon aondoke na wakati bado hakuwa amekubaliana nae juu ya kile ambacho alikuwa amemwambia.
   Alichokifanya ni kuanza kumfuata Simon na kisha kumshika mkono. Simon akageuka nyuma, uso ake tayari ulionekana kubadilika, alionekana wazi kuwa na hasira.
   “Samahani kama nitakuwa nimekuuzi” Natasha alimwambia Simon.
   “Naomba uuachie mkono wangu” Simon alimwambia Natasha kwa sauti ya chini.
   “Sawa. Ila naomba unisamehe”
   “Usijali. Naomba usijaribu tena kuongea kitu chochote kuhusu mahusiano kati yangu na wewe. Nakuheshimu sana Natasha. Naomba uuheshimu uamuzi wangu pia” Simon alimwambia Natsaha na kisha kuondoka mahali hapo.
                                                                                    ********
   Maisha yakaonekana kuanza kubadilika. Walter akaanza kuwa adimu machoni mwake. Kila siku Beatrice alikuwa akijaribu kumtafuta Walter simuni lakini hakuwa akimpata na kama kulikuwa na kipindi kikatokea kumpata basi hawakuongea sana.
   Walter alijifanya kuwa bize na masomo, hakutaka kukumbuka mapenzi, muda mwingi alikuwa akiutumia kuizima simu yake. Kwa Beatrice hali ilikuwa ni ya majonzi makubwa kupita kawaida, maisha kwake bila Walter yalionekana kuwa magumu.
   Beatrice akakosa amani, furaha yote ambayo alikuwa nayo katika kipindi cha nyuma ikatoweka. Masomo yakaanza kumwendea vibaya, muda mwingi wa kusoma alikuwa akimfikiria Walter. Afya yake nayo ikaanza kubadilika na kuwa dhoofu.
   Hakujua ni kitu gani ambacho kilikuwa kinaendelea katika maisha ya Walter. Suala la Walter kwamba alikuwa ametafuta msichana mwingine wala halikuweza kumuingia akilini. Alimuamini sana Walter kiasi ambacho wakati mwingine aliona ni vigumu kwa mvulana huyo kumsaliti.
   Kitu ambacho kilikuwa kikimpa nguvu ni kwamba wazazi wa pande zote mbili walikuwa wakiufahamu uhusiano huo ambao ulikuwa ukikua kadri siku zilivyokuwa zikizidi kwenda mbele nyakati za nyuma. Kitendo cha Walter kumsaliti kilionekana kuwa kitendo kigumu kutokea katika maisha yote.
   Siku zikakatika pasipo kumuona Walter wala kuongea nae. Beatrice alikuwa akivumilia kila siku. Wiki ya kwanza ikakatika, wiki ya pili nayo ikakatika, ya tatu na mpaka mwezi kukatika lakini wala hakuweza kuwasiliana na Walter.
   Maisha yake yakaonekana kubadilika, aliiona dunia ya mapenzi ikianza kumgeukia. Mara kwa mara alikuwa akijaribu kwenda nyumbani kwa kina Walter lakini wala hakuweza kumkuta. Kitu alichokifikiria Beatrice ni kuanza kwenda katika shule ya Kenton, huko napo hakuweza kuonana na Walter.
   Kikafika kipindi ambacho Beatrice akaona kwamba Kwa wakati huo Walter hakuwa wake tena. Hakuelewa sababu abazo zilimpelekea Walter kutokumpigia simu katika kipindi chote cha mwezi mmoja. Akajua kwamba kuna kitu cha tofauti ambacho kilikuwa kimeingilia uhusiano wao katika kipindi hicho.
   Beatrice akaendelea kuivumilia hali hyo mpaka katika kipindi ambacho akaamua kwenda nyumbani kwa kina Walter. Safari hii hakutaka kmpigia mama yake Walter kwamba alikuwa akielekea nyumbani hapo. Alitaka kwenda ndani ya nyumba hiyo pasipo taarifa yoyote ile.
   Tayari kichwa chake kilikuwa kikimweleza kwamba kulikuwa na kitu ambacho kilikuwa kikiendelea nyuma ya pazia. Mara baaada ya kutumia dakika arobaini, akafika nje ya geti la nyumba ya kina Walter. Alitamani kugonga lakini akaamua kuacha.
   Alichokifanya ni kuelekea katika sehemu ambayo ilikuwa na mti mmoja mrefu na kutulia huku macho yake yakiangalia getini. Dakika zilikatika mpaka kufikia saa moja kasoro, muda ambao gari la Walter likaanza kupiga honi nje ya geti lile.
   Beatrice akajificha huku macho yake yakiangalia kule lilipokuwa gari lile. Geti likafunguliwa na kisha gari kuingia ndani. Beatrice akaanza kupiga hatua za haraka haraka kuelekea kule getini. Hata kabla geti halijafungwa, Walter akaonekana akiteremka huku akielekea katika upande mwingine na kuufungua mlango.
   Msichana mrembo Jalia akaanza kuteremka. Wote wakaanza kupiga hatua kuelekea ndani ya nyumba ile. Moyo wa Beatrice ukapigwa na mshtuko akabaki akiwa ameduwaa. Mwili wake aliuhisi ukikosa nguvu, hakuamini kile ambacho alikuwa akikiona mbele yake.
   Kwa jinsi muonekano wao ulivyoonekana wala hakukuwa na swali ambalo lilitakiwa kuulizwa juu ya uhusiano ambao walikuwa nao, walionekana kuwa wapenzi. Macho yake yakaanza kulengwa na machozi, wala hazikupita sekunde hata kumi, machozi yale yakaanza kumtoka.
   Kumbukumbu zake zikaanza kurudi nyuma kama mkanda wa filamu. Akaanza kuikumbuka siku ya kwanza ambayo alikutana na Walter na kuanza uhusiano. Beatrice hakuishia hapo, akaanza kuzikumbuka siku zote ambazo alikuwa akimkataa Simon.
   Moyoni alijiona kuruka majivu na kukanyaga moto. Mara mlinzi akaanza kulifunga geti lile huku Beatrice akionekana kusimama wima kana kwamba alikuwa akiimba wimbo wa Taifa. Mara akili zake zikamrudia. Akaanza kupiga hatua kulifuata lile geti na kuanza kuligonga kifujo fujo.
   “Mbona unagonga geti kifujo fujo?” Mlinzi alimuuliza Beatrice mara baada ya kulifungua geti.
   “Nataka kuongea na mpenzi wangu” Beatrice alimwambia mlinzi.
   “Mpenzi wako! Nani?” Mlinzi aliuliza.
   “Walter” Beatrice alijibu.
   “Hayupo” Mlinzi alijibu.
   “Hayupo? Amekwenda wapi?”
   “Uganda. Kwani hakukuaga?” Mlinzi aliuliza swali lililomchanganya Beatrice.
   “Unasemaje wewe? Hebu nipishe huko. Nimemuona halafu unaniambia hayupo!” Batrice alimwambia mlinzi huku akimsukuma na kuingia ndani.
   Beatrice akaanza kupiga hatua kuufuata mlango wa mbao wa kuingilia sebuleni. Alionekana kuwa na hasira kali kupita maelezo, hakuonekana kutaka kuelewa kitu chochote kile kwa wakati huo, kitu ambacho alikuwa akikitaka ni kuonana na Walter na kumpa ufanfanuzi juu ya msichana yule aliyemuona nae.
   “Ngo... Ngo... Ngo...” Beatrice aliugonga mlango ule wa mbao kwa hasira.
                                                                     *****

   Moyo wa Natasha ulikuwa katika maumivu mazito. Kila siku mapenzi juu ya Simon yalikuwa yakiusumbua moyo wake. Hakuna kitu ambacho alikuwa akikihitaji kwa wakati huo zaidi ya mapenzi, tena mapenzi mazito kutoka kwa Simon.
   Nyakati za usiku hasa wakati wa kulala kwake zilikuwa za tabu, akili yake ilikuwa imetawaliwa na Simon kupita kawaida. Kwa kipindi hicho, mapenzi ndio ambayo yalichukua sehemu kubwa ya moyo wake ambao kila siku alikuwa akiulinda kimahusiano.
   Ni kweli kwamba alikuwa ametoka katika familia iliyokuwa na utajiri mkubwa. Alikuwa na uwezo wa kununua kitu chochote ambacho alikuwa akikihitaji kwa wakati huo. Mapenzi yalishindwa kununulika kwa fedha alizokuwa nazo lakini kama yangekuwa na uwezo wa kununulika, basi angefanya hivyo.
   Mara kwa mara alikuwa akitumia kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya kununulia zawadi mbalimbali na kumgawia Simon. Simon akawa mtu wa kushukuru kila siku lakini kamwe hakutaka kumkubalia Natasha ambaye alionyesha kuwa na mapenzi ya kweli kwake.
   Simon alifahamu fika kwamba katika wakati huo alikuwa ndani ya mahusiano pamoja na Violeth japokuwa hakutaka kumwambia ukweli kwa kuhofia kumfikiria zaidi badala ya masomo. Hakutaka kumsaliti Violeth, alijiona kuwa na uhitaji wa kuwa na Violeth kwa ajili ya kumfariji kwa kipindi kile kirefu ambacho alikuwa akimfikiria shuleni.
   Aliyatambua maumivu ambayo alikuwa nayo Natasha, kwani maumivu yale ndio ambayo nae alikuwa akiyapata katika kipindi ile shuleni kwa kumpenda Beatrice ambaye wala hakuwa katika moyo wake. Kumsaliti Violeth kilionekana kuwa kitu kiguu ambacho hakukitaka kabisa kitokee katika maisha yake yote.
   Aliijua thamani ya mapenzi, zaidi ya yote alijua fika kwamba mapenzi yalikuwa na picha gani. Mara kwa mara alikuwa akiwasiliana na Violeth huku wakisisitiziana kuwa waaminifu mpaka pale ambapo wangekuwa pamoja na kutengeneza familia moja yenye furaha na amani.
   “Usinisaliti mpenzi” Violeth aliwambia Simon.
   “Usijali. Sitokusaliti katika maisha yangu” Simon alimwambia Violeth simuni.
   “Nashukuru kwa kusikia hivyo. Nadhani nitakupigia simu kesho kukujulia hali” Violeth alimwambia Simon.
   “Kwa nini nisikupigie mimi?”
   “Huwa tunapiga simu kwa wizi. Si unajua mambo haya ya shuleni, tunaogopa kukamatwa. Usijali mpenzi, nitakupigia simu” Violeth alimwambia Simo.
   “Poa. Hakuna shida”
   “Nakupenda”
   “Nakupenda pia”
   Hayo ndio maisha ambayo kila siku walikuwa wakiishi. Walikuwa wakipigiana simu kila siku na kuongea mambo mbalimbali huku wakisisitiziana kuwa waaminifu katika maisha yao. Hakukuwa na mtu ambaye alikuwa na wasiwasi na mwenzake, wote walikuwa wakiaminiana kupita kawaida.
   Siku ziliendelea kukatika mpaka kufikia siku ambayo Violeth alimpa taarifa mbaya Simon, taarifa ya kwamba wazazi wake walikuwa wakihamia mkoani Kigoma kikazi. Hivyo kila mwanafamilia alitakiwa kuhamia mkoani Kigoma.
   “Taarifa zako zimenichanganya mpenzi” Simon alimwambia Violeth.
   “Nimechanganyikiwa zaidi mpenzi. Yaani inamaanisha kwamba likizo hii sitorudi Dar s Salaam zaidi ya kuelekea mkoani Kigoma” Violeth alimwambia Simon.
   “kwa hiyo hatutoweza kuonana?”
   “Nafikiri”
   “Kwani hauna ndugu wa kumtembelea huku Dar es Salaam?”
   “Wapo. Ila wazazi wamenitaka kwenda kwanza mkoani Kigoma. Wanaonekana kufahamu matatizo ya ndugu zetu na ndio maana hawataki mimi kuelekea huko kuishi na hao ndugu” Violeth alimwambia Simon.
   “Furaha yote imepotea. Yaani ulibakia mwezi mmoja tu kuonana nawe”
   “Hata mimi pia mpenzi. Ila cha msingi yatupasa kuendelea kuwa waaminifu. Tutafikia malengo yetu tu”
   “Sawa. Nafikiri kuna siku tutaonana na kuweza kuoana kama tulivyoahidiana”
   “Ndio mpenzi. Nakupenda sana”
   “Nakupenda pia”
   Simon akauhisi mwili wake kuishiwa nguvu, niguu yake ikalegea na kujikuta akikaa chini. Alijiona kama kutokusikia vizuri kile ambacho alikuwa ameambiwa na mpenzi wake, Violeth. Moyo wake ulikuwa umemkumbuka sana Violeth kiasi ambacho alijiona kama kuchanganyikiwa mara baada ya kuambiwa kwamba asingeweza kumuona katika kipindi cha karibuni.
   Katika kipindi hicho ndicho ambacho Simon alikuwa katika mapenzi mazito na Violeth. Kila siku alikuwa akijishangaa juu ya hali hiyo. Mawazo juu ya msichana Beatrice yalikuwa yamepotea kabisa, na kama ilitokea siku alimkumbuka basi alikuwa akiyashangaa mabadiliko hayo.
   Violeth ndiye ambaye alikuwa kila kitu katika maisha yake, kamwe hakutaka kumuacha, aitaka kuishi nae katika maisha yote. Ila bado kuna kitu ambacho kilikuwa kikimsumbua akilini mwake, juu ya ndoto ambayo alikuwa ameiota katika miaka kadhaa iliyopita.
   Kila siku alikuwa akiendelea kujiuliza juu ya msichana yule ambaye alikuwa amemuona ndotoni. Sura yake ilikuwa ngeni kabisa machoni mwake. Hakuwahi kumuona hata sehemu moja katika maisha yake. Kipindi cha nyuma alipanga kumtafuta ila baada ya kuwa na Violeth, akaamua kuachana na wazo la kutaka kumtafuta.
   Kwa sasa mawazo juu ya msichana yule yakaanza kujirudia tena kichwani mwake. Nyakati za usiku Simon alikuwa akiteseka kitandani. Mawazo juu ya Violeth na msichana ambaye alikuwa amemuona ndotoni yalikuwa yakimsumbua kila siku.
   Kiu yake kubwa ilikuwa ni kutaka kuonana na msichana huyo ili ajue ni kitu gani ambacho kingetokea baada ya hapo. Hakujua ni kitu gani ambacho angetakiwa kukifanya katika kipindi hicho kama tu angekutana na msichana huyo huku akiwa katika mapenzi ya Violeth.
   Hakujua ni kitu gani ambacho angetakiwa kukifanya kwa wakati huo, kumchukua msichana huyo au kuendelea kuwa pamoja na Violeth ambaye alimsumbukia kulitaka penzi lake toka shuleni. Simon akabaki akiwa hana jibu kwa wakati huo, ila kitu pekee ambacho alikiona kuwa ni sahihi kilikuwa ni kuisubiria siku hiyo ya kuonana na msichana huyo aliyemuona ndotoni.
                               ********
   Mlango ukafunguliwa na mfanyakazi wa ndani, Beatrice hakutaka kuuliza kitu chochote kile, akaingia ndani. Uso wake ukaonyesha hasira kubwa aliyokuwa nayo moyoni, kitendo cha kusalitiwa kwake kilionekana kumuumiza kupita kiasi.
   Sebuleni hakukuwa na mtu yeyote kitu ambacho kikamfanya kuanza kupiga hatua kuelekea chumbani kwa Walter. Alijaribu kuufungua mlango, mlango ulikuwa umefungwa kwa ndani. Akaanza kuugonga kifujo fujo, wala hazikupita sekunde nyingi, mlango ukafunguliwa na Walter kutoka nje huku akiwa na taulo.
   “Msichana gani umeingia nae ndani?” Beatrice aliuliza huku akionekana kukasirika.
   Walter hakujibu chochote kile, alibaki na tabasamu huku akimwangalia Beatrice usoni. Tabasamu lile likaonekana kumkasirisha Beatrice kiasi ambacho akatamani kumvamia Walter na kupigana nae. Tayari akajiona kuwa katika wakati mgumu, Walter, kwake akaonekana kubadilika na kuwa Walter mpya ambaye wala hakuwa na mapenzi kwake.
   “Nimeingia na Jalia” Walter alijibu kwa kujiamini huku tabasamu likiendelea kuwa usoni mwake.
   “Jalia! Jalia ndiye nani?” Beatrice aliuliza huku hasira zikionekana kuwa usoni mwake.
   “Msichana wangu” Walter alijibu.
   Beatrice aliuhisi mwili wake kama umepigwa na shoti ya umeme, hakuamini kile ambacho alikuwa amekisikia kutoka mdomoni mwa Walter kilikuwa ndicho kile alichokisikia au hakuwa amesikia vizuri. Machozi yakaanza kuonekana machoni mwake na baada ya sekunde kadhaa yakaanza kutiririka mashavuni mwake.
   “Unasemaje?” Beatrice aliuliza kana kwamba hakuwa amesikia.
   “Toka lini Beatrice umekuwa kiziwi? Umenisikia sahihi kabisa kile nilichokisema” Walter alimwambia Beatrice ambaye alionekana kuchanganyikiwa.
   “Yaani umeamua kunisaliti!”
   “Cha ajabu kipi sasa? Kusalitiwa ni kitu cha kawaida tu katika mchezo mzima wa mapenzi, namaanisha kama kuchezewa rafu uwanjani” Walter alimwambia Beatrice.
   Beatrice akalifuata kochi na kutulia, bado machozi yalikuwa yakiendelea kutiririka mashavuni mwake. Moyo wake uliumia kupita kawaida, hakuamini kama Walter yule ambaye alimpenda kwa moyo wa dhati ndiye ambaye leo hii alikuwa akimwambia maneno yale.
   Wala hazikupita sekunde nyingi, Jalia akatokea sebuleni pale akitokea chumbani. Beatrice akazidi kuumia zaidi, kitendo cha kumuona Jalia usoni mwake kulimuongezea hasira. Beatrice akashindwa kuvumilia, kwa kasi ya ajabu akasimama na kisha kumvamia Jalia kwa lengo la kumpiga.
   Walter hakutaka kuingilia, alichokifanya akakaa kochini na kuangalia mchezo mzima. Ni ndani ya dakika mbili tu, Beatrice alikuwa chini akilia, uso wake ulikuwa umejaa damu, blauzi yake nyeupe ambayo alikuwa ameivaa ilikuwa imebadilika rangi kabisa na kuwa nyekundu.
   “Utakuja kufa” Walter alimwambia Beatrice.
   Beatrice hakutaka kubaki mahali hapo, kwa haraka haraka akasimama na kuanza kuondoka ndani ya nyumba hiyo. Mwili wake alikuwa akiusikia maumivu makali. Moyoni ndipo ambapo aliumia zaidi, kusalitiwa na Walter kwa msichana kama Jalia kulionekana kumuumiza.
   Kila alipokuwa akimfikiria Jalia aliona kutokuwa na sababu kwa Walter kumsaliti. Aliuona vizuri uzuri ambao alikuwa nao, alivutia kwa kila kitu na si kama ambavyo alivyokuwa Jalia. Njia nzima Beatrice alikuwa akilia, kila kitu ambacho kilikuwa kikiendelea kwa wakati huo kwake kilionekana kuwa kama filamu ambayo muda wowote ingeisha au ndoto mbaya ambayo baada ya muda angeamka kutoka katika usingizi mzito.
   “Mbona hivyo mwanangu?” Mama yake, Bi Imelda aliuliza.
   Beatrice hakujibu chochote kile, moja kwa moja akaanza kuelekea chumbani kwake na kujifungia. Siku nzima alikuwa akilia huku akiijutia hatua aliyochukua ya kuwa pamoja na Walter. Alkaanza kuulazimisha moyo wake kumchukia Walte lakini akajiona kushindwa kabisa.
   Ukweli ni kwamba alikuwa akimpenda sana Walter kiasi ambacho alishindwa kabisa kumchukia kwa haraka namna ile. Bado aliona kulikuwa na nafasi moyoni mwake ya kumsamehe walter kwa kila kitu ambacho alimfanyia. Pamoja na kufikiria hayo bado hakuwa akijua kama Walter angekuja kwake kuomba msamaha au la.
   Usiku kwake ukawa mgumu, hapo ndipo alipogundua maumivu ya kusalitiwa yalikuwa vipi. Siku iliyofuata hakutaka kutoka nje, alibaki chumbani kwake akiendelea kulia. Alilia na kunyamaza, baadae alipokuwa akikumbuka kile kilichomtokea, alilia tena na tena.
   “Namchukia Walter” Beatrice alijisemea ingawa alijua fika kwamba moyo wake ulikuwa tofauti na kile alichokuwa akikisema.
                                                                          ********
   Msichana wa ndotoni. Huyu ndiye ambaye alikuwa akikisumbua kichwa cha Simon, kila wakati alikuwa na mawazo juu ya msichana huyu. Moyo wake ulitamani sana kukutana na msichana huyu ambaye kwa mara ya kwanza alikuwa amemuona ndotoni.
   Aliikumbuka sana sura ya msichana yule kiasi ambacho kamwe asingeweza kumsahau. Hakujua ni kwa jinsi gani angemuona na kuanzisha nae uhusiano. Kila siku alipokuwa akitembea sehemu mbalimbali alikuwa akijaribu kupitisha macho yake huku na kule lengo lake likiwa ni kuona kama angeweza kumuona msichana yule.
   Miezi ilikuwa ikiendelea kukatika lakini hakuweza kukutana na msichana yule. Bado mawasiliano yake na msichana wake, Violeth yalikuwa yakiendelea kama kawaida. Kila siku maneno ya mapenzi ndio ambayo yalikuwa yakitawala katika midomo yao.
   Walikuwa wakionyeshana mapenzi ya kweli huku kila mmoja akijitahidi kumuonyesha mwenzake ni kwa jinsi gani alikuwa na thamani kubwa katika maisha yake.
   Simon alionekana kuwa gizani, kadri siku zilivyozidi kwenda mbele na ndiivyo ambavyo Violeth alivyozidi kuukamata oyo wake, hakujua ni kwa jinsi gani angeweza kumuacha Violeth katika kipindi ambacho angekutana na msichana yyule ambaye alimuona ndotoni mwake miaka kadhaa iliyopita.
   “Nikimaliza shule lazima nije Dar es Salaam kuonana nawe mpenzi” Violeth alimwambia Simon.
   “Ninakusubiri mpenzi, nina hamu kubwa ya kukuona tena” Simon alimwambia Violeth.
   “Unajua kwamba nimeshaanza kubadilika?”
   “Umekuaje?”
   “Mnene. Hai ya hewa ya huku naoa imeanza kunikubali sana”
   “Kwa hiyo umeanza kuwa bonge?”
   “Ndio hivyo”
   “Usiwe mnene sana mpenzi. Hata kama utanenepa jaribu kuwa na unene wa kawaida”
   “Nitajitahidi”
   “Kwa hiyo umeridhika na maisha ya huko?”
   “Naweza nikasema ndio ila kuna kitu ambacho kila siku najitahidi kukipata lakini sikipati”
   “Kitu gani?”
   “Kukuona wewe”
   “Usijali. Ila nadhani ukiniona ndio utaridhika zaidi na kuongezeka mwili zaidi”
   “Hapana mpenzi. Naomba unitumie hata picha zako. Sanduku letu la posta si nimekwishakupa?”
   “Nakumbuka. Nitakutumia. Usijali mpenzi” Simon alisema.
   Mapenzi makubwa ndio ambayo yalikuwa moyoni mwa kila mmoja. Bado Simon hakuonekana kuwa na furaha kama iliyotakiwa awe nayo, mawazo yake yalikuwa juu ya yule msichana mrembo ambaye alikuwa amemuota katika miaka kadhaa iliyopita.
   “Nitajua nitafanya nini” Simon alisema katika kipindi ambacho msichana Natasha alikuwa akiingia darasani hapo huku akiwa ameshika ua zuri jekundu.
                            ********
   Uso wa Natasha ulikuwa ukionyesha tabasamu pana katika kipindi ambacho alikuwa akipiga hatua za taratibu kumsogelea Simon mahali pale alipokuwa amekaa. Simon alibaki kimya, alitamani kuondoka mahali hapo ili mladi tu lile ua ambalo alikuwa amelishika Natasha asiweze kulipokea.
   Mara baada ya kumfikia Simon, Natasha akakaa pembeni yake na kisha kuanza kumwangalia usoni. Macho yake yalikuwa yakimtazama katika hali ya kimahaba. Lugha ya macho ndiyo ambayo ilikuwa ikitumika mahali hapo, Simon aliweza kuisoma lugha ile vilivyo.
   “Nimekumiss sana Simon” Natasha alimwambia Simon.
   “Unasemaje?”
   “Nimekumiss sana” Natasha aliyarudia maneno yake.
   Simon hakuongea kitu chochote kile, alibaki kimya kwa muda huku akimwangalia Natasha. Uso wake ukaonekana dhahiri kutokufurahishwa na kile ambaho alikiongea Natasha kwa wakati ule. Alichokifanya ni kusimama kutoka pale alipokuwa na kuanza kupiga hatua kuelekea nje.
   “Mbona unanikimbia?” Natasha alimuuliza.
   “Nilikwambia nini kabla?” Simon alimuuliza.
   “Kuhusu nini?”
   “Kwa hiyo umesahau?”
   “Uliniambia mengi tu. Ila vyote ulivyoniambia sijui kama vinahusiana na jambo lolote linaotokea mahali hapa” Natasha alimwambia Simon.
   “Naomba uniache Natasha. Nimekwishakwambia kwamba sihitaji kitu chochote kutoka kwako. Kwa nini unakuwa haunielewi?”
   “Nimekuelewa Simon. Ila nimefanya nini?”
   Simon akanyamaza. Akabaki kimya huku akimwangalia Natasha. Hakuelekewa amwambie nini kwa wakati huo. Alielewa fika kwamba ua lile ambalo alikuwa ameliona ndiocho kitu ambacho kilimfanya kumkumbushia kile ambacho alimwambia katika siku za nyuma.
   Natasha alionekana kutokuelewa, kitendo cha kuzuiliwa kuongelea mapenzi mbele ya Simon kilionekana kuwa kitu kigumu sana katika maisha yake.Kamwe hakuweza kukaa kimya katika kipindi ambacho alikuwa akimuona Simon mbele yake, alijisikia kuongelea mapenzi kila wakati.
   “Naomba unielewe Natasha. Unaponiona hapa ni lazima ujue kwamba nina msichana wangu nimpendae kwa dhati” Simon alimwambia Natsaha.
   “Nafahamu hilo Simon kwa sababu ulikwishaniambia kabla” Natasha alimwambia Simon.
   “Sasa mambo ya maua yanakujaje mahali hapa?” Simon alimuuliza Natasha.
   “Nafahamu kwamba nimechelewa Simon. Ila samahani sana, naomba uniruhusu niwe naongea kuhusu mapenzi kila ninpokutana nawe. Najisikia furaha sana. Hata kama haunitaki, naomba uniruhusu kuongea kuhusu mapenzi. Nakuomba” Natasha alimwambia Simon.
   “Itakusaidia nini sasa na wakati sitaki kuwa nawe?” Simon aliuliza.
   “Itanifanya kuwa na furaha maishani mwangu”
   Simon hakuongea tena kitu chochote kile, alichokifanya ni kuanza kupiga hatua kuelekea nje ya darasa lile. Akili yake ilionekana kuchanganyikiwa, moyoni hakuwa na mapenzi juu ya Natasha ambaye kila siku alikuwa akijitahidi kuwambia maneno mengi ya mapenzi.
   Hakujua afanye nini kwa wakati huo. Ni kweli kwamba moyo wake haukuwa kwa Natasha ambaye mara kwa mara alikuwa akimuonyeshea jeuri ya fedha. Moyo wake ulikuwa kwa msichana ambaye kwake alionekana kuwa mtu muhimu sana, Violeth.
   Maisha yake ya shule hayakuwa ya furaha kutokana na usumbufu ambao alikuwa akiupata kutoka kwa msichana Natasha. Natasha alionekana kutokuelewa kabisa, kila siku usumbufu wake ulikuwa kwa Simon ambaye hakuwa na penzi lolote kwake.
   Miezi iliendelea kukatika na hatimae kuingia kidato cha sita. Bado alikuwa akiendelea kuwasiliana na mpenzi wake, Violeth. Miezi iliendelea kukatika na hatimae kuanza kufanya mitihani ya Taifa ya kidato cha sita. Bado mawasiliano kati yake na Violeth yalikuwa yakiendelea kila siku.
   Baada ya miezi kadhaa, matokeo yakatolewa na hatimae Simon kuchaguliwa kujiunga na chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Hiyo ilikuwa ni furaha kwake pamoja na kwa mama yake, Bi Martina. Tayari akaiona ndoto yake ya kuwa daktari wa mifupa ikianza kutimia kama alivyotaka iwe.
   Alichokifanya chuoni ni kusoma kwa bidii. Alitamani ile ndoto ambayo alijiwekea toka utotoni itimie kama vile alivyopanga. Mawasiliano pamoja na Violeth hayakuisha, bado walikuwa wakiendelea kuwasiliana japokuwa miaka mitatu tayari ilikuwa imekatika bila kuonana.
   “Endelea kuwa muaminifu Mpenzi” Simon alimwambia Violeth ambaye alikuwa akisomea Elimu katika chuo cha SAUT jijini Mwanza.
   “Usijali mpenzi. Japokuwa miaka mingi imepita lakini bado nitaendelea kuwa pamoja nawe” Violeth alimwambia Simon.
   Simon aliesoma kwa bidii chuoni, usiku hakulala, kitu ambacho alikuwa akikiangalia mbele yake ni kutimiza malengo ambayo alikuwa nayo moyoni mwake. Simon alikuwa mwanachuo ambaye alifanya vizuri mwaka wa kwanza na wa pili kiasi ambacho Maprofesa wa chuo cha Muhimbili kumhitaji kwa ajili ya kuwafundisha wanachuo wa chuo hicho kwa malipo makubwa.
   Maisha yake akayaona yakianza kubadilika. Kutokana na foleni kubwa pamoja na mkusanyiko mkubwa wa watu katika daladala, Simon akaamua kununua gari dogo kwa ajili ya kulitumia. Tayari alikuwa akijikusanyia fedha kwa wakati huo.
   Akawa akielekea chuoni kusoma huku akielekea katika chuo cha Muhimbili na kufundisha. Baada miaka minne kumaliza kusoma, hapo ndipo ambapo akaajiliwa rasmi kufundisha ndani ya chuo hicho. Kila mwanachuo alikuwa akimfurahia Simon namna ambayo alivyokuwa akifundisha.
   Alipopata fedha za kutosha, akaamua kupanga nyumba nzima iliyokuwa Sinza. Maisha yake yakaanzia hapo huku akiwa pamoja na mama yake. Hawakulala na njaa tena kama ilivyokuwa zamani. Kwa wakati huo walikula kila chakula ambacho walikuwa wakitaka kula.
   Simon hakutaka mama yake, Bi Martina afanye kazi yoyote jambo ambalo lilimpelekea kumuajiri mfanyakazi wa ndani. Maisha hayakuwa ya machungu tena, kila siku walikuwa wakiishi kwa furaha.
   “Nataka kumpigia simu Violeth aje Dar es Salaam ili niongee nae kuhusu mpango wetu wa kufunga ndoa” Simon alimwambia mama yake.
   “Yule msichana wa kipindi kile cha nyuma?” Bi Martina aliuliza.
   “Ndio. Yeye ndiye chaguo langu japokuwa kuna kitu kinanitatiza sana” Simon alimwambia mama yake.
   “Kitu gani?”
   “Yule msichana niliyemuona katika ndoto”
   “Yaani bado unakumbuka tu! Achana nae, ile ilikuwa ni ndoto tu ya kawaida” Bi Martina alimwambia Simon.
   “Lakini mbona kila siku inakaa kichwani mwangu mama? Ndoto nyingi nilizoziota nimezisahau lakini ile bado naikumbuka. Tena nakumbuka kila kitu. Hadi sura ya msichana mwenyewe” Simon alimwambia mama yake.
   “Ila hautakiwi kukumbuka kitu chochote kile” Bi Martina alimwambia Simon.
   Baada ya wiki moja kupita, Simon akaanza kufanya mawasiliano na Violeth huku lengo lake likiwa ni kumtaka afike jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumtambulisha kwa mama yake. Violeth hakutaka kukataa, japokuwa hakuwa amemuona mpenzi wake huyo kwa miaka sita, akaamua kuanza safari ya kwenda Dar es Salaam.
   Ndani ya treni, Violeth alikuwa na mawazo juu ya mpenzi wake, kichwa chake kilikuwa kinafikiria mambo mengi ambayo yalikuwa yametokea katika maisha yao ya nyuma. Hakujua ni kwa jinsi gani angempokea katika stesheni ya treni mara baada ta kumuona.
                               *******
   Moyo wa Beatrice bado ulikuwa katika majonzi mazito, kilio kwake ikawa kama sehemu ya maisha yake. Akili yake haikutaka kabisa kukubali kama Walter ndiye ambaye alikuwa amemfanyia kile ambacho alikuwa amemfanyia. Furaha kwake ikaonekana kukatika kabisa.
   Maisha yake akayaona kuwa kama ndoto mbaya na ya kuhuzunisha ambapo baada ya muda angeshtuka kutoka katika usingizi mzito. Kila wakati Beatrice alikuwa akifikicha macho yake kuona kama kweli alikuwa kwenye ndoto au la. ITAENDELEA KESHO

Endelea kulike: www.facebook.com/2jiachie
Tembelea: www.2jiachie.com

No comments

Powered by Blogger.