MKUU WA MKOA WA ARUSHA AIKABIDHI NGAO VODACOM TANZANIA
Mkuu
wa mkoa wa Arusha Bw.Magessa mulongo, akimkabidhi ngao Ofisa Mkuu wa
Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Georgia Mutagahywa kwa
kutambua mchango na jitihada za Vodacom kuhakikisha usalama
barabarani,ngao hiyo ilikabidhiwa wakati wa kilele cha maadhimisho ya
Wiki ya Nenda kwa Usalama barabarani yamefanyika kitaifa mkoani
Arusha,kampuni ya Vodacom ni moja wa wadhamini wakubwa wa wiki ya nenda
kwa usalama barabarani mwaka huu
Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Georgia Mutagahywa akiwa na maofisa wa jeshi la polisi wakisilikiza hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Bw.Magessa mlongo,wakati wa kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama barabarani ambayo imefanyika kitaifa mkoani Arusha,ambapo Vodacom Tanzania wamepewa tunzo ya kutambulika kwao katika kutoa mchango na jitihada za kuhakikisha usalama barabarani,Tuzo hiyo wamekabidhiwa katika siku ya ufunguzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani mwaka huu.
Baadhi
ya wananchi waliohudhuria sherehe za uzinduzi wa Wiki ya Nenda kwa
Usalama Barabarani wakimuangalia mtaalamu wa masuala ya uokoaji Bw.
Nelson Gachiru,aliyekuwa kwenye moja ya banda la maonyesho katika uwanja
waSheikh Amri mjini Arusha,Vodacom Tanzania ni moja ya wadhamini wakuu
wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani mwaka huu na kuweza
kujinyakulia ngao ya kutambulika kwa mchango wake na jitihada za
kuhakikisha usalama barabarani


Post a Comment