MARIA - 02
Giza tayari lilikuwa limeingia kiasi ambacho ilikuwa ni ngumu sana kumuona mtu ambaye alikuwa hatua kumi kutoka ulipo. Zaidi ya hayo yote, kitu ambacho kilionekana kumfurahisha zadi Onesmo ni mara baada ya umeme kukatika.
***********
Maria alikuwa akijisikia kuwa katika hali isiyokuwa ya kawaida tangu siku ya kwanza ambayo alimuona mvulana ambaye alikuwa mgeni machoni mwake, Onesmo. Mara baada ya kufika sebuleni na kumimina maji katika bilauri, muda wote Maria alikuwa akitetemeka kupita kawaida.
Hali hiyo ilionekana kuwa tofauti, haikuwahi kumtokea hata siku moja katika maisha yake. Moyo wake akauhisi kuanza kutengeneza kitu ambacho hakuwa akieewa ni kitu gani. Hadi vijana wale wawili waliokuja nyumbani kwao kuondoka, Maria akajikuta akiwa katika hali kubwa ya mawazo.
Kila wakati Maria alionekana kuwa na mawazo, tayari moyo wake ulikuwa umetengeneza kitu cha tofauti, kitu ambacho kilimfanya kujiona tofauti.Kuanzia hapo maisa yake yakaanza kuwa ya mawazo, kila aipokuwa akila, mawazo yake yalikuwa yakimuwaza mtu ambaye alifanikiwa kumuona kwa siku moja tu, Onesmo.
Siku ziliendelea kukatika mpaka kufikia kipindi ambacho alikuwa akijisikia kuumwa ugonjwa ambao hakuwa na uhakika kama ulikuwa na dawa katika dunia hii zaidi ya kumtia machoni kijana yule. Maria akakosa raha, kila siku mawazo yalikuwa yakiendelea maishani mwake.
Maria hakuyaamini macho yake mara baada ya siku moja kurudi nyumbani na kumuona mtu ambaye alikuwa akimfikiria kila siku akiwa nyumbani kwao. Ugonjwa ambao alikuwa akiumwa na ambao hakuwa akiufahamu akauona ukianza kutoweka.
Furaha ikaanza kuurudia moyo wake, akaanza kujiona mtu wa tofauti kabisa. Kitu kile ambacho alikuwa akijisikia moyoni mwake akakihisi kikizidi kukua zaidi na zaidi. Kila wakati Maria alikuwa akionekana kuwa na furaha, alitamani mwanaume yule amite na kuongea nae tu, sauati yake ilionekana kuwa kitu muhimu maishanimwake.
Kila alipokuwa akikonyezwa, Maria alijisikia furaha, hakuamini kama mwanaume yule alikuwa katka hali kama ambayo akilikuwa nayo yeye. Maria alijiona kubadilika, noto za kuwa sista katika maisha yake tayari aliziona zikianza kupotea.
“Kuwa sista si lazima. Nitakuwa hata mwanasheria” Maria alijisemea kila alipokuwa akimwangalia Onesmo.
Mara baada ya kuitwa na Onesmo ambaye alimuomba miadi ya kuonana nae, Maria akatamani sana kuonana nae katika sehemu ambayo haikuwa na uwezo mkubwa wa kufikiwa na mtu usiku na ndio maana akachagua kuonana nae uwanjani.
“Nimefurahi sana kuitikia wito wangu mrembo” Onesmo alimwambia Maria katika kipindi ambacho walikuwa uwanjani.
Onesmo akaanza kuongea mambo mengi ambayo yalimaanisha ni jinsi gani alikuwa akijisikia juu ya Maria. Kila neno ambal alikuwa akiliongea katika kipindi hicho lilionekana kuwa na mvuto kwa Maria. Maria hakuongea kitu chochote kile, mwili wake ulikuwa ukitetemeka tu.
“Nakuhitaji Maria. Wewe ni msichana ambaye najiona kumuhitaji sana katika maisha yangu, u msichana unayejiheshimu, mzuri na una mvuto mkubwa Maria” Onesmo alimwambia Maria huku tayari maongezi yao yakiwa yamechukua dakika kumi na tano.
“Nahitaji kuwa nawe Maria, nahitaji kukuonyeshea thamani kubwa maishani mwako. Nakuahidi kukujali, kukufurahisha na hata kukufanya kuwa na furaha maishani mwako. Wewe ndiye kila kitu kwangu, wewe ndiye maisha yangu, pumzi yangu na hata uhai wangu” Onesmo alimwambia Maria.
Maria bado hakuongea kitu chochote kile, aliendelea kubaki kimya huku kila kitu ambacho alikuwa akikiongea Onesmo kikiwa kikimuingia moyoni mwake. Ahadi ambazo alikuwa amepewa zikaonekana kumchanganya kupita kawaida, moyo wake ukazidi kuvutiwa na Onesmo.
Onesmo alipoona Maria amekaa kimya, akaanza kujisogeza kwa karibu zaidi, kifua cha Maria kikaanza kumchoma kifuani mwake. Akausogeza mdomo wake na kuanza kumbusu mashavuni. Maria akazidi kutetemeka zaidi, damu ikaanza kuzunguka kwa mzunguko wa kasi mwilini mwake.
Mabusu yaliendelea mfululizo kutoka kwa Onesmo. Baada ya sekunde kadhaa, mdomo wa Onesmo ukaanza kuhamia sehemu nyingine, Maria akajikuta akianza kubadilishana mate na Onesmo hali ambayo ilimfanya kujisikia kuwa katika hali ya raha ambayo hakuwahi kuihisi kabla.
“Nach...elew...a ny..umb..a..n.i..” Maria alijikuta akimwambia Onesmo huku akipumua kama mtu aliyetoka kukimbia mbio ndefu.
Onesmo hakuonekana kusikia, akaizungusha mikono yake kiunoni mwa Maria na kumvutia kwake, Maria akajikuta akianza kutomaswa mwili wake. Hisia kali za mapenzi zikaukamata mwili wake. Akaanza kuhisi kama kulikuwa na wadudu walikuwa wakimtembelea mwilini mwake.
Huku akionekana kuzidiwa na miguso ile, baada ya dakika kadhaa Maria akashangaa kuona akiwa mtupu kama alivyozaliwa. Alitamani kumsukuma Onesmo lakini kila alipotaka kufanya hivyo, aijikuta akizidiwa zaidi. Hata dakika hazikuwa nyingi, akajikuta amelala chini juu ya kanga yake mwenyewe huku Onesmo akiendelea kufanya kile ambacho akili yake ilikuwa ikimtuma kukifanya kwa wakati ule.
Pumzi ndefu mfululizo ziliendelea kumtoka Maria, akaanza kuunyonga nyonga mwili wake. Tayari alionekana kuzidiwa kwa kila kitu, mwili wake ulikuwa tayari kupokea kila kitu ambacho Onesmo alikuwa akikifanya mwilini mwake.
“Nau..miaaaaaaaa....” Maria alijikuta akilalamika mara baada ya kuhisi kuna kitu kilikuwa kikimuumiza chini ya kitovu.
Kila alipokuwa akilalamika, Onesmo hakuonekana kuelewa kitu chochote kile. Maria aliendelea kulalamikia maumivu, tayari alijiona kupoteza kitu ambacho kingemfanya kutokutimiza ndoto yake ya kuwa sista.
Maria bado alikuwa akiendelea kulia, akajihisi akitokwa na damu chini ya kitovu. Aliendelea kulalamikia maumivu lakini Onesmo hakuonekana kuelewa kitu chochote kile mpaka pale alipomaliza baada ya dakika kumi kupita.
“Angalia ulivyoniumiza” Maria alilalamika.
“Usijali Mpenzi. Hii ni siku ya kwanza, mara ya pili hautosikia maumivu yoyote yale” Onesmo alimwambia.
“Niniiiii? Mara ya pili? Sitaki tena kufanya mchezo huu. Sitakiiiiiiiiiiii” Maria alisema, akainuka na kuanza kuondoka kwa mwendo wa kasi.
“Amekwisha” Onesmo alijisemea.
************
Maria alilia usiku kucha, kitendo cha kumruhusu Onesmo kuutoa usichana wake ulimuumiza kupita kiasi. Moyo wake ukaanza kujuta, usiku mzima alikuwa akilia tu. Hakuamini kama ingetokea siku ambayo angetolewa usichana wake kwa urahisi kiasi kile.
Ingawa alikuwa akiujutia uamuzi wake wa kumruhusu Onesmo kuutoa usichana wake lakini upande mwingine wa moyo wake bado ulikuwa ukifurahia kitendo kile. Maumivu ambayo alikuwa akiyasikia kipindi kilichopita yakawa yamekwishapoa, alijisikia kama zamani.
Mpaka asubuhi inaingia, Maria alikuwa macho, akainuka kitandani na kuanza kujiandaa kwa ajili ya kwenda shule. Mwili wake ulikuwa ukijisikia uchovu mwingi, kila wakati kichwa chake kilikuwa kikimfikiria Onesmo.
Mara baada ya kujiandaa, Maria akatoka na kuanza kuelekea shuleni. Darasani mawazo yake yalikuwa juu ya Onesmo, kitendo cha kufanya mapenzi usiku uliopita kilikuwa kimemuumiza kupita kiasi. Alijua kwamba alimwambia Onesmo kutotaka kuurudia mchezo ule tena, lakini hali tayari ikaanza kuonekana tofauti.
Mwili wake ukaanza kumsisimka, hamu fulani ikaushika mwili wake, akatamani kuwa na mvulana pembeni yake, mvulana ambaye angempa nafasi ya kumchezea chezea. Mawazo ya Maria yakarudi kwa Onesmo, akatamani kuonana nae kwa mara nyingine kwa ajili ya kufanya kitendo ambacho alimwambia kuwa asingediriki kukifanya pamoja nae kwa mara nyingine.
Muda wote Maria alionekana kuwa na mawazo hali ambayo kila mwanafunzi alilifahamu hilo. Hakuonekana kuwa katika hali ya kawaida kabisa, kila alipokuwa akiuliza juu ya hali yake, kisingizio kilikuwa ni kutokujisikia vizuri.
Mara baada ya kengele ya kurudi nyumbani ilipogongwa, Maria hakutaka kubaki shuleni kama siku nyingine, moja kwa moja akaanza kurudi nyumbani. Tayari mwili wake ulikuwa na hamu ya kushkwa shikwa na mwanaume, hakutaka kitu chochote katika kipindi hicho zaidi ya kutamani kuwa karibu na Onesmo.
Kama kawaida yao wakapanga sehemu ya kufanyia mchezo wao, hawakutaka tena kufanyia katika sehemu ambayo ingewafanya kuonekana, sehemu ambayo waliipanga ilikuwa ni katika chumba ambacho Onesmo na Issa walikuwa wakikitumia.
“Mhh!.. Utaweza kuingia pasipo kuonekana?” Onesmo aliuliza huku akionekana kuwa na wasiwasi.
“Nitaweza tu Mpenzi. Usijali” Maria alimwambia Onesmo.
Usiku ulipofika wakawa pamoja chumbani huku Issa akiwa nje akihakikisha usalama. Chumba kilikuwa kimya hali iliyoonyesha kuwa kazi kitendo kile kilikuwa kikiendelea. Zilipita dakika arobaini, mlango ukafunguliwa na Maria kutoka nje.
Hiyo ndio ilikuwa mara ya mwisho kufanya katika kipindi hicho. Siku iliyofuata, Onesmo na Issa wakaanza safari kurudi Dar es Salaam huku magunia ya maihindi mia moja yakiwa katika gari lao aina ya Canter ambalo walikuwa wamekuja nalo kijijini hapo.
“Kama vipi nitamuoa tu. Amenivutia sana” Onesmo alimwambia Issa huku akionekana kufurahia.
**********
Siku ziliendelea kukatika kama kawaida, mawazo juu ya Onesmo hayakuweza kufutika kichwani mwa Maria. Mapenzi yalikuwa yamemteka kupita kawaida, kila siku alikuwa akimfikira Onesmo tu. Maisha yake yalionekana kuwa na tabu, maisha pasipo Onesmo yalionekana kuwa kama jehanamu.
Kila siku alitamani kuongea nae, moyo wake ulikuwa na kiu kubwa ya kuonana nae. Siku kwake ikaonekana kuwa ndefu kupita kawaida. Akajiona dhahiri akiumwa, ugonjwa mkubwa wa mapenzi ulikuwa umempata maishani mwake.
Masomo hayakusomeka kama kawaida, kitandani usingizi haukupatikana kama siku nyingine. Chakula hakikuwa kikipita kama kawaida. Mapenzi ambayo alikuwa akiyasikia kuwa yalikuwa yakimfanya mtu kukonda kwa ajili ya mawazo, tayari yalikuwa yamekwishatawala katika maisha yake.
Maria akaanza kujisikia uchovu mwingi, mara kwa mara alikuwa akijisikia mvivu. Maria akajiona dhahiri kuumwa, kichefuchefu kikaanza kumpata. Mara kwa mara alikuwa akitapita, tayari alijiona kuwa tofauti na siku nyingine.
Hali ambayo haikuwa ya kawaida ikaendelea kumuingia, kutapika ikaonekana kuwa sehemu moja ya maisha yake. Wasiwasi ukaanza kumjia, akaanza kuona kuwa tayari alikuwa mjauzito. Maria akaanza kuogopa, ukali wa baba yake ukaonekana kumuogopesha.
Maria hakutaka kujulikana kwa wazazi wake hali iliyomfanya mara kwa mara kutotaka kuonana nao. Kila wakati alikuwa akijifungia chumbani akimung’unya udongo.
Bi Sara ndiye ambaye akaonekana kuhisi kitu, hali aliyokuwa nayo Maria tayari ikaanza kumtia wasiwasi. Bi Sara alifahamu kila kitu, dalili zote za mwanamke aliyekuwa mjauzito zilikuwa zikionekana kwa Maria. Bi Sara hakuonekana kukubaliana na hali ile jambo ambalo lilimfanya kumwambia Maria kuwa ni lazima kwenda hospitalini.
“Mbona najisikia kawaida mama” Maria alijitetea.
Bi Sara hakutaka kukubaliana nae, aliendelea kuweka msisitizo wa kutaka kwenda hospitalini kujua ni kitu gani ambacho kilikuwa kikiendelea kwa binti yake, Maria.
“Mama. Niko salama, siumwi mama” Maria aliendelea kujitetea.
“Hapana Maria. Nina wasiwasi mkubwa na afya yako. Niambie ukweli, una ujazito?” Bi Sara alimuuliza.
Maria hakujibu kitu chochote kile, alibaki kimya kwa muda huku akionekana kufikiria jibu la kutoa. Hakujua kama angemwambia mama yake juu ya kila afya yake ni kitu gani ambacho kingetokea. Aliaminika sana nyumbani kwao, hakuonekana kuongea na mwanaume yeyote yule, swali ambalo lingetawala kichwani mwa kila mtu ni juu ya sehemu alipopatia ujauzito huo.
“Mimi si mjauzito mama” Maria aliendelea kujitetea.
Bado Bi Sara hakuonekana kukubaliana na maneno hayo, aliendelea kusisitiza kwenda hospitalini kwa ajili ya kuchukua vipimo. Ingawa Maria aliendelea kukataa, ikafikia wakati ikambidi kukubaliana nae.
Bi Sara akaamua kumwambia mumewe juu ya kila kitu ambacho kilikuwa kikiendelea. Mzee Bwaro hakuonekana kukubaliana nae, utulivu wa Maria ulikuwa ukimfanya kutokuamini kama kungekuwa na mwanaume ambaye angeweza kumlaghai binti yake.
“Unaikumbuka ndoto yake aliyotuambia kuhusu maisha yake?” Mzee Bwaro alimuuliza mkewe.
“Ndoto ipi?”
“Ya kuwa Sista. Sasa atawezaje kufanya mchezo huo? Maria hawezi kabisa” Mzee Bwaro alimwambia mkewe.
Kitu alichokifanya Bi Sara ni kumwambia mumewe kwamba ni lazima waende hospitalini pamoja na binti yao ili kijua ni kitu gani ambacho kilikuwa kinaendelea juu ya afya ya binti yao. Ingawa mara ya kwanza mzee Bwaro alikataa lakini mwisho akakubaliana nae na safari ya kuelekea katika hospitali ya wilaya kuanza.
Muda wote Maria alikuwa akitetemeka, alijua fika kwamba alikuwa mjauzito, hakujua afanye nini kwa wakati huo, hakujua ni hatua gani wangechukua wazazi wake kama wangegundua ukweli kuwa ni mjauzito. Amani ikatoweka moyoni mwa Maria, alitamani kukimbia, lakini alishindwa kufanya hivyo.
“Tunahitaji umfanyie vipimo vyote. Tunahitaji kulijua tatizo lake” Bi Sara alimwambia dokta Semi.
Dokta Semi akawataka wazazi hao wamsubiri ndani ya ofisi yake huku yeye akimpeleka Maria sehemu husika kwa ajili ya kumchukua vipimo.
“Una ujauziti wa mwezi mmoja” Daktari alimwambia Maria mara baada ya vipimo vilivyochukua dakika kumi.
“Najua dokta, sitaki wazazi wangu wafahamu... nisaidie dokta” Maria alimwambia dokta Semi.
Tayari Maria akaanza kulia, alijua fika kwamba alikuwa mjauzito, moyo wake ulikuwa ukijifikiria juu ya uamuzi ambao wangechukua wazazi wake. Maria aliendelea kuomba msaada kwa dokta Semi lakini hakukuwa na msaada wowote ambao aliahidiwa.
Dokta Semi alitamani kumsaidia Maria lakini alishindwa kujua ni kwa jinsi gani angeweza kumsaidia. Alimwangalia usoni, tayari machozi ambayo yalikuwa yakitiririka mashavuni mwake yalianza kuiloanisha blauzi aliyokuwa ameivaa.
Endelea kulike ==>www.facebook.com/2jiachie
ITAENDELEA SIKU YA KESHO

Post a Comment