ad

ad

MAJONZI, ZLATAN KUIKOSA BARCELONA LIGI YA MABINGWA LEO

PSG watapambana katika mechi yao ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Barcelona bila ya mshambuliaji wao nyota, Zlatan Ibrahimovic.

Katika mechi hiyo itakayopigwa leo kwenye dimba la Parc des Princes, PSG haitakuwa na Zlatan aliyewahi kuichezea Barcelona.
Uongozi wa matajiri hao wa Ufaransa, umethibitisha kuwa Mswidi huyo ameumia mguu wake, hivyo hataweza kuivaa Barcelona.
Hilo ni pigo kubwa kwa Kocha Laurent Blanc ambaye lazima alimhitaji Zlatan.
Lakini Zlatan pia angefurahi kucheza dhidi ya timu yake hiyo ya zamani aliyowahi kusema wachezaji wake wanaishi kama watoto wa shule.

No comments

Powered by Blogger.