ad

ad

VITILIVYOGO (PAPA NA MUHOGO) - 13

MTUNZI: DK. AMBE
Endelea kulike ==>www.facebook.com/2jiachie

“Siyo hivyo Shaka, mara nyingi ninapokuwa na wewe huwa anajua nipo wapi hunipitia na kunisindikiza nyumbani, kwa vile ni shoga yangu humuamini kuwa nimepitia kwao.”
“Bado sijakuelewa, inaonekana hii ndiyo tabia yenu?”
“Tabia gani tena baby mbona najuta kulizua.”
“Siyo kulizua nafahamu kabisa mtindo huu haukuanza leo kwa vile sikukuta msichana.”
“Mungu wangu, yaani umefika huko?”
“Mimi nani yako?”
“Mume wangu.”
“Kwa nini huniambii ukweli?”
“Baby haki ya nani, kuna siku unakumbuka tuliachana saa nne usiku niliporudi nyumbani niligombezwa sana na kuonekana nimeanza umalaya. Nilimueleza siku ya pili Diana ambaye ndiye aliyenifundisha mbinu za yeye kuja kunitembelea na mimi kwenda kwao ili nikikutana na wewe nipate nafasi ya kujitetea. Akiwa hayupo huwa nawahi mwenyewe unafahamu bali unataka kunionea tu.”
Stella alijitetea mpaka machozi yalimtoka kwa kuhofia kumpoteza, Shaka aliingiwa na huruma na kuamini anayosema mpenzi wake.
“Basi mpenzi yamekwisha.”
“Shaka nakupenda sana amini sina mwanaume yeyote zaidi yako.”
“Nimekuelewa mpenzi.”
“Basi nipe haki yangu.”
“Tutachelewa baby.”
“Nikiwa na wewe hata nikipigwa nyumbani siogopi.”
“Kwa sasa ni saa ngapi?”
“Saa mbili usiku.”
“Basi tumalizie baby.”
Waliingia kilingeni Shaka aliendelea kugawa dozi kama hana akili nzuri maufundi aliyofundishwa na Betty, Stella alichanganyikiwa na kumlazimisha Shaka walale pale hotelini.
“Hapana baby sasa ni saa tatu na nusu tuwahi nyumbani.”
“Shaka unanipenda?”
“Tena sana.”
“Basi naomba leo tulale kwa mara ya kwanza.”
“Hapana kitamu huliwa kwa hamu pia ukila na kipofu usimshike mkono.”
“Nimekuelewa,lakini naomba kwa leo tu baby.”
“Unawaheshimu wazazi wako?”
“Ndiyo.”
“Unapenda penzi letu liendelee?”
“Tena tuwe mke mume na mke tuzae na watoto.”
“Basi nyanyuka tukaoge tuwahi nyumbani.”
“Mmh! Sawa babu nakubali kwa vile nakuamini kwa asilimi elfu moja.”
Walikubaliana kwenda kuoga kisha walitoka muda ulikuwa saa nne za usiku, Stella alimteremsha Shaka kwao na yeye kurudi kwao bila kujua atawaeleza nini wazazi wake.
Shaka akiwa hoi alielekea kwao, kutokana na uchovu alipanga akifika ndani tu anabadili nguo na kujitupia kitandani bila kuwasha taa. Alitembea kwa kujivuta akielekea nyumbani. Alipofika alisogea mlangoni ili aingie ndani, alipogusa mlango ili azungushe kitasa kufungua  mlango aliguswa kwa nyuma na kumfanya ashtuke.
Alipogeuka alishtuka kuonana  uso kwa macho na Betty.
“Ha! Betty?”
“Ndiyo mimi,” Betty alisema kwa sauti ya upole.
“Mbona saa hizi unatoka wapi?”
“Shaka nikuulize mimi au wewe?”
“Betty mimi ndiye natakiwa kujibiwa kwa vile nimeuliza,” Shaka aliweka kibesi.
“Shaka huwezi kuamini leo nimekuwa sichezi mbali na kwenu toka saa mbili, kila nikiuliza wanasema hujarudi.”
“Ha! Umemuuliza nani?”
“Wote, huwezi kuamini leo nimeingia chumbani kwako kwa mara ya kwanza ili kupata uhakika, nilijua mdogo wako alikuwa akinidanganya kuwa hujafika.”
“Mmh! Karibu.”
“Shaka ulikuwa wapi mpenzi wangu?”
“Mpirani.”
“Mbona mmechelewa kurudi?”
“Gari lilituharibikia njiani.”
“Lakini si nilikukataza kwenda?” Betty alimuuliza.
“Huwezi kuamini mechi zote walizocheza sikwenda, leo mwalimu alinitishia kuniadhibu ndiyo nikaenda.”
“Si utakuwa umechoka sana mpenzi wangu?” Betty alikuwa mpole.
“Wee acha tu, kuna kipindi tulilisukuma gari kwa umbali mrefu, ukichanganya  na mechi hapa nipo hoi,” Shaka alitengeneza mazingira ya kumkwepa Betty kwani alikuwa amechoka sana.
“Kwa hiyo Shaka?”
“Kama mambo yetu! Utanisamehe, nipo hoi.”
“Shaka usinitanie, una siku gani hujanipa raha zangu, leo Shaka punda afe lakini lazima mzigo ufike.”
“Mpenzi huenda nisikuridhishe, kwa nini isiwe kesho ili nikupe kitu kamili?”
“Shaka utani huo njaa ya leo haiwezi kushiba kwa ahadi ya kesho.”
“Naogopa kukuudhi mpenzi.”
“Huwezi Shaka nitajua jinsi gani ya kufika safari yangu kwa msaada wako.”
“Mmh! Sawa, lakini sijala.”
Shaka hakuwa na jinsi kumchomoka Betty ambaye alikuwa na ugwadu wa muda mrefu.  Betty naye hakutaka kupoteza  muda waliondoka na Shaka hadi kwenye baa na kumnunulia chipsi mayai na nusu kuku, kisha waliondoka hadi  kwake.
Walipofika kwanza alimpelekea Shaka maji ya moto bafuni kuoga kisha alimuandalia chakula mezani ili akitoka kuoga apate chakula na kopo la Red Bull kwa ajili ya kurudisha nguvu zilizopotea. Shaka akiwa bafuni alijiuliza maswali mengi juu ya kukabiliana na Betty, mwanamke mwenye ugwadu kama mfungwa.
Kwa vile alikuwa amemdanganya alipanga muziki utapozimikia basi ndiyo utakuwa mwisho wa burudani, kwani hatakuwa na lawama kutokana na kujihami mapema. Alijiuliza mwisho wake nini kutembea na wanawake wote wale kila mmoja akikutana naye anataka dozi kamili.
Betty naye hali ilikuwa mbaya kutokana na kukosa kipande cha muhogo wa Jang’ombe ambao kila alipougegeda lazima aliulamba mwiko. Siku alizomkosa Shaka na kwenda kwa mpenzi wake alirudi na upele wake kutokana na mkunaji kukosa kucha na mwenye kucha alikuwa anaumwa.
Shaka alitoka bafuni akiwa na upande wa kanga, Betty alichukua upande mwingine na kumfuta mwili mzima. Kisha alimsogeza kwenye chips yai kuku.
“Mpenzi wangu kunywa kwanza hii Red Bull ili irudishe nguvu, kisha ule upande nguvu angalau unipatia mguu wa jini uwe wa kukidhi haja. Kama utaniongeza mbili za mkwezi nitafurahi zaidi. Haki ya nani nitakupa zawadi kubwa.”
“Nitajitahidi mpenzi.”
“Basi kula mi naenda kuoga.”
Betty alisaula  palepale na kuelekea bafuni bila kitu mwilini huku akichezesha vilima viwili vya nyuma ambavyo vilikuwa laini kama mchicha pori. Alifanya vile kumshtua Shaka kwa kuamini hata kama amechoka akiona umbile tamu kama ile lazima atarudi mchezoni.
Shaka naye alimsindikiza kwa macho huku akajishangaa kuweza kupata utamu wa mwanamke kama yule anayemilikiwa na mwanaume mwenye fedha tofauti na yeye kula chakula cha shikamoo. Japokuwa alikuwa amechoka lakini alijiapiza akimkosa sana basi mbili za mkwezi za haja.
Wasiwasi wake ukabakia kwenye kuchoka sana na kushindwa siku ya pili kwenda shule. Lakini aliamini hakumtendea haki Betty mpenzi wake kwa kumdanganya mtu aliyemfanya aonekane machoni  kwa watu. Alipanga  kupigana kufa na kupona kuhakikisha anapata zawadi aliyoahidiwa na Betty.
Betty akiwa bafuni kila alipojishika kwa bibi alihisi kama ameota upele unaohitaji kukunwa na Shaka. Alipanga hata kama Shaka atachoka mapema lakini atatumia mtindo wa mti wa kufulia nazi ambao kazi yake kusimama nazi kupigwa juu yake na nazi hutoka vizuri tayari kwa kupasuliwa na kukunwa.
Betty alitoka bafuni kama alivyoingia bila kitu mwilini  na kurudi kwa Shaka aliyeshambulia msosi kama fisi mwenye njaa aliyevamia bucha. Muziki aliokutana nayo kwa Stella japokuwa ulimchosha ulikuwa wa kitoto ila kazi ilikuwa kwa Betty mama shughuli na shughuli yake lazima ushughulike kisawasawa.
Betty baada ya kukaa pembeni ya Shaka, alivuta upande wa khanga na kuwa saresare maua. Mchezo ulianzia palepale mezani Shaka hakuwa na haraka alianza kwa ulaji wa mboga saba kugusa kila bakuli na kumfanya Betty ambaye tayari mchicha ulikuwa umekolea nazi kuangukia banda la kuku na kupasua yai moja. Betty aliona Shaka chenga nyingi wakati hakabwi na mtu zaidi ya kuusukumia mpira wavuni.
“Shaka punguza chenga nifunge goli bhana, mwenzio maji yamechemka zamani tia mchele uache sufulia lifuate mwiko.”
Siku zote mfungaji mzuri akilaumiwa husahihisha makosa yake kwa kupeleka mpira wavuni na kuwafanya watazamaji walipuke na mayowe ya kufurahia goli na kusahau lawama.
Taratibu Shaka ambaye alikuwa ameanza kuwa mzoefu wa bahari aliingiza chombo majini na kuanza kupiga kasia taratibu kama mamba mzee kwenye mto. Betty dakika ya kwanza tu baada ya konga mbili tatu alikurupuka golini na kupishana na mpira na kumfanya apige kelele.
“Shakaaa, unaona..unaona mambo si ndiyo haya.”
Mtu mzima alikuwa akiokota yai lililopasuka kwenye banda la kuku, kama bondia alikuwa amekutana na ngumi asiyoitegemea na kumpeleka chini. Alinyanyuka harakaharaka na kufuta gloves mchezo ukaendelea.
 Kwa vile Shaka alikuwa ametoka kutumika wazungu walikuwa mbali, kila alipowaita walikuja taratibu ikabidi Betty afungue bomba kwa kupasua madafu mengi, kitu kilichomfanya achoke sana.
Alishangaa Shaka kuwa na nguvu za ajabu kwa kuweza kumliza kilio mara nyingi bila kuonesha naye kamwaga hata tripu moja.
“Shaka hujafika hata mara moja?” Betty aliuliza kwa sauti ya muhemo kutokana na kuchoka sana.
“Bado.”
“Mmh! Ni Red Bull tu au umetumika?” alishtuka.
“Walaa, uchovu wa mpira na kinywaji ulichonipa kimefanya niwe na nguvu kama faru.”
“Mmh! Leo nimepatikana mtoto wa kike.”
“Tuache?”
“Hapana, mpaka ufike na wewe.”  
Betty aliamini kwa mtindo ule atakesha, alikaa mkao wa kibao cha mbuzi mkuno wa nazi. Huku akitweta alimwambia Shaka:
“We tulia niachie kazi hii.”
Shaka alikaa kama alivyoelekezwa na kumuacha mtoto wa kike akiiacha nyonga ifanye kazi yake, kifuu kilijizungusha kwenye meno ya mbuzi. Shaka alijikuta akikutana na kitu kipya kabisa ambacho kilimfanya awahi kupasua yai la bata mzinga. Kwa vile Betty alikuwa mzoefu baada ya Shaka kutua mzigo alimpa pole.
“Pole na safari mpenzi,” Betty alimshukuru Shaka kwa kumtoa jasho la chini ambalo wanaume wengi walishindwa.
“Asante,” Shaka naye alijibu huku akihisi uchovu wa ajabu kwa kusikia kizunguzungu.
Wote wawili walikuwa wamechoka sana, usingizi ukawapitia bila kujijua.
                                                              ***
Betty alikuwa wa kwanza kuamka, alipojaribu kunyanyuka mwili ulikuwa umechoka sana kama alikuwa akiangusha mbuyu kwa kisu cha kukunja. Alipoangalia saa ya kwenye simu ilimuonesha ni saa kumi na moja alfajiri. Alishtuka kwa kujua ulikuwa muda muafaka kwa Shaka kuamka kwenda kujiandaa kwenda shule. Alimuangalia  alikuwa amejilaza akiwa hoi kama mtu aliyekuwa akifua vyuma.
“Shaka,” alimwita huku akimtikisa.
“Mmh!”
“Amka kumekucha wahi kwenu ili ujiandae kwenda shule.”
“Leo siendi.”
“He! Leo hakuna shule?” Betty alishtuka.
“Ipo.”
“Sasa kwa nini huendi.”
“Nimechoka sana kazi uliyonipa jana si ya kitoto.”
“Sasa itakuwaje nyumbani kwenu watasemaje?”
“Wacha nilale kidogo ili baadaye nikalale nyumbani.”
“Hapana Shaka, japokuwa nimechoka naomba nikusindikize kwenu kwani sasa hivi ni saa kumi na moja.”
Shaka alinyanyuka kitandani huku mwili ukiwa umechoka sana, Betty alimsindikiza bafuni kuoga kisha alimsindikiza mpaka kwao. Wakati Betty akimsindikiza Shaka, shoga yake Edna alikuwa akitoka kumsindikiza mumewe aliyekuwa na sindano za masaa lakini hakutaka kumshtua.
Moyoni aliumia kwa kujua kama Betty amefanikiwa kulala na Shaka mpaka asubuhi basi atakuwa amepata raha kamili, utamu thabiti toka kwa kijana mdogo mwenye uwezo kama wa nyati. Moyoni alijilaumu kuolewa mapema, lakini alijipanga kuhakikisha siku moja analala na Shaka mpaka asubuhi.
Shaka baada ya kufikishwa kwao alimgongea mdogo wake baada ya kuingia alifikia kitandani na kuutwanga usingizi wa haja. Asubuhi alipoamshwa kwenda shule alisingizia ugonjwa, siku ile aliamka saa sita mchana. Hakuwa yeye tu aliyepigika hata Betty naye alikuwa hoi.
Baada ya kurudi kumsindikiza Shaka alipofika kitandani naye usingizi mzito ulimpitia. Majira ya saa nne asubuhi shoga yake Edna alitaka kupata umbeya, alikwenda kwa shoga yake. Alipofika alikuta mlango umerudishwa aliingia ndani na kuita lakini hakujibiwa, alikwenda chumbani na kumkuta Betty amelala usingizi mzito akiwa hajitambui.
Mlalo aliolala ulikuwa unaonesha jinsi gani alivyokuwa amechoka, alikuwa amejitandaza kitanda kizima huku akikoroma. Edna alijikuta akimuonea wivu shoga yake na kujiuliza siku gani na yeye anapata kipigo kile cha pweza. Aliamini akimuamsha atakuwa sawa na kuzuia chafya kwani alitakiwa kuachwa alale ili hamu zake zimuishe aamke mwenyewe.
Alimuacha bila kumwamsha na kurudi kwake huku akiwa na mawazo mengi juu ya uwezo wa Shaka. Kilichomshangaza kuwa na uwezo japokuwa hakuwa mtaalamu sana wa kitandani lakini nguvu zake zilimfanya mwanamke kulia kilio cha mvua ya machozi.
Siku hiyo Betty aliamka saa nane mchana, kutokana na kuwa na njaa kali, kuoga aliona anachelewa alijifunga vitenge na kukimbilia kwenye baa ya karibu na kuagiza mchemsho na kuteremshia na pombe kali. Edna aliyekuwa anapita karibu na baa ile alishangaa kumuona shoga yake mchana ule akipata kinywaji huku akionekana hajatulia.
Alimfuata na kumsalimia.
“Shoga vipi mbona upo hivyo?”
“Mmh! Shoga wee acha tu, Shaka jana kidogo aniue.”
“Kivipi?”
“Toka nivunje ungo jana kidogo roho iachane na mwili kwa utamu usioisha hamu.”
“Kwa nini?” Edna alishtuka na kukaa kitako macho yamemtoka pima kama aliyeona samaki wakivuliwa kwenye lami.
“Shoga si ya kuzungumza hapa ngoja nimalize kinywaji twende nyumbani, yule mtoto lazima atakuwa amechanjia. Jana nilimwaga mpaka tenki likakauka mtoto ndo kwanza anakuja. Huwezi amini njaa niliyokuwa naisikia, kuoga niliona nachelewa.”
“Mmh! Shoga inatosha utanimalizia nyumbani.”
Betty alimaliza kinywaji chake haraka na kulipa kisha waliongozana kurudi nyumbani. Edna alikuwa na shauku ya kujua kitu gani Shaka alichomfanyia mpaka akasababisha tenki kuvunja mpaka likakauka.
                                                     ***
Majanga hayakuwa kwa Shaka na Betty tu, Stella asubuhi ilipofika kitanda kilikuwa kitamu kama nini, alijishauri mara mbilimbili juu ya kwenda shule. Alijikuta akiamua kupumzika kwani mtanange wa jana usiku ulikuwa wa kufa mtu na kumfanya achoke sana. Alikubaliana na maneno ya Diana kuwa Shaka haonjwi mara moja akakuisha hamu.
Aliamua siku ile kulala nyumbani na kusingizia kwa mama yake anaumwa tumbo baada ya kwenda kumuamsha. Diana alimpitia rafiki yake kama kawaida, alipofika alipokelewa na mama yake.
“Shikamoo mama.”
“Marahaba Diana.”
ANGALIZO: ITAENDELEAMPAKA MWISHO HAPA KAMA SHARE ZITAFIKA 3,000 NA COMMENT 2,000 VINGINEVYO MTAMALIZIA KATIKA KITABU
ITAENDELEA SIKU YA KESHO

No comments

Powered by Blogger.