VITILIVYOGO (PAPA NA MUHOGO) - 07
VITILIVYOGO (PAPA NA MUHOGO) - 07
MTUNZI: DK. AMBE
Endelea kulike ==>www.facebook.com/2jiachie
Alimwita mhudumu na kuagiza juisi mchanganyiko na pizza. Alipotaka kuagiza nyingine Shaka alisema:
“Unajua nini mpenzi?”
“Hata sijui Shaka.”
“Sisi ni wapenzi haipendezi kila mtu ale yake, tutakula pizza moja, glasi moja ya juisi na mrija mmoja au hunipendi?” Shaka alitikisa kiberiti.
“Aah! Shaka usinifanye nikalia, basi nisamehe nakupenda sana mpenzi wangu,” Stella alipiga magoti kuomba msamaha bila aibu na kumfanya mhudumu kushangaa huku Shaka akiamini mtoto wa kike kaimeza ndoano yote.
“Aaah! Baby nyanyuka,” Shaka alimnyanyua huku akiwa haamini binti mwenye nyodo kama Stella kumpigia magoti.
“Hapana baby bado hujanisamehe.”
“Nimekusamehe mpenzi wangu japo kwangu sioni kosa lako.”
“Asante mpenzi wangu.”
Waliagiza pizza na juisi na kunywa pamoja kama wapenzi wa muda mrefu. Wakiwa wanaendelea kunywa juisi Stella alitaka siku ile isipite tupu alitaka angalau apate hati miliki ya kummiliki Shaka.
“Shaka ukitoka hapa unakwenda wapi?” alimuuliza huku amemlegezea macho.
Japokuwa Shaka alikuwa anatakiwa siku ile akalale kwa Betty alijikuta akichanganyikiwa. Lakini siku zote kipya kina raha yake, hakutaka kuipoteza nafasi ile pamoja na kutojua aliulizwa swali kwa ajili gani.
“Kwani ulikuwa unasemaje mpenzi?”
“Shaka nina hamu ya kuwa na wewe jioni hii.”
“Mmh! Mpaka saa ngapi?”
“Hata nusu saa ili tu siku ya leo iandikwe katika historia ya maisha yangu.”
“Mmh! Sawa, wapi?”
“Sema wewe.”
“Mi mgeni mwenyeji wangu ni wewe.”
“Jamani Shaka nikisema mimi mwanamke si utaniona malaya,” Stella alisema kwa aibu.
“Acha mawazo ya kizamani, wee sema wapi wala usihofu.”
“Unapaonaje Princess Hotel?”
“Mmh! Poa tu, tutaingiaje?”
“Kuna siku nilimsindikiza Diana na kuingia kwa mlango wa nyuma.”
“Basi tufanye hivyo si unajua wote ni wanafunzi tusiwe tu kituko,” Shaka alimtoa wasi lakini akiamini kabisa Stella ni mzoefu wa sehemu zile.
“Usiwe na wasiwasi.”
Stella alitoka nje na baada ya muda alirudi na kumueleza Shaka kuna teksi nje atangulie nayo Princess Hotel.
“Shaka tangulia na hiyo teksi hapo nje akikufikisha usiteremke mpaka nifike. Nikifika nitaingia moja kwa moja nawe nifuate nyuma sawa?”
“Hakuna tatizo,” Shaka alisema huku akitoka nje kwenda kwenye teksi aliyoelezwa na Stella.
Alipofika nje aliiona teksi kali ambayo alipanda na dereva aliondoa gari.
“Vipi mwana?” dereva alimuuliza huku akikanyaga mafuta.
“Poa tu bro.”
“Yule msichana ni dada yako?”
“Kwa nini umeniuliza?”
“Mzuri.”
“Sasa uzuri wake mimi unanihusu nini?”
“Labda demu wako?”
“Hapana,” Shaka alikataa.
“Nani yako?”
“Shida yako nini?”
“Basi nilitaka kujua jina lake, unajua yule demu matawi anachukuliwa na mtoto wa kigogo na hoteli yake hiyohiyo aliyosema nikupeleke.”
“Ushampeleka mara ngapi?”
“Nyingi na dereva wake ni mimi au Tito.”
“Poa, mi nina safari zangu.”
“Au ndiyo anataka kampani yako, unajua mademu kama wale lazima wapate kampani ili kuua soo wanapokuja kukutana na wajanja wao.”
“Walaa, si unaona nipo peke yangu.”
Dereva alisimamisha gari pembeni ya Hoteli ya Princess. Shaka hakuteremka alisubiri kulingana na maelekezo aliyopewa na Stella.
Baada ya muda teksi nyingine ilisimama karibu kabisa na mlango wa hoteli. Stella aliteremka haraka na kuingia ndani ya hoteli, Shaka naye kama alivyopewa maelekezo alifungua mlango ili ateremke.
“Kumbe mwana mzigo wako!”
“Kawaida.”
“Kumbe mwana nawe matawi?”
Shaka hakujibu, aliteremka na kufunga mlango kisha alichepua mwendo kuingia ndani ya hoteli ili asipotezane na Stella. Alimkuta Stella akimsubiri.
“Vipi?”
“Poa.”
“Nisubiri nakuja,” Stella alisema huku akiingia ndani ya hoteli upande wa vyumba.
“Poa.”
Stella aliingia ndani na kurudi bila kutoka nje kabisa na kumwita kwa ishara amfuate. Shaka alimfuata ndani, walielekea moja kwa moja chumbani.
Stella alitangulia na Shaka alifuata kisha walifunga mlango. Baada ya kuingia ndani Stella alishusha pumzi ndefu kitu kilichomshtua Shaka.
“Vipi mpenzi?”
“Mmh! Yaani nimejikaza sijawahi kuingia gesti mwenzio,” Stella alisema akiwa ametawaliwa na hofu.
“Pole, hata mimi ndiyo siku yangu ya kwanza.”
Shaka alifunika kombe mwanaharamu apite, hakutaka kumshushua Stella kwani sicho alichokifuata. Kumpata kwake ilikuwa kama kuokota pochi katikati ya soko.
Ilikuwa ni moja ya ndoto zake japokuwa Betty ndiye alimchanganya zaidi. Kwa upande mwingine aliamini Stella ndiye saizi yake kuliko Betty kwa vile alikuwa na mtu wake aliyekuwa akimmiliki yeye alikuwa kama mwizi.
Moyoni aliapa Stella akitoka pale asisahau katika maisha yake hasa baada ya kuongezwa mautundu na Betty. Baada ya kupumzika kwa muda walikwenda kuoga.
Mchezo ulianzia vyumba vya ukaguzi timu moja ilipata bao la utangulizi na kufanya mechi iongeze ushindani kwa mmoja kutaka kusawazisha na mwingine kuonyesha kufunga bao la mapema hakubahatisha.
Baada ya kutoka bafuni walihamia kwenye tatali lenye nyasi za asili kila mmoja akitaka kushinda mchezo wa kwanza ili kujenga heshima.
Stella aliamini kabisa Shaka si wa kwake mwenyewe lakini alichotaka kukifanya siku ile basi yeye ndiye awe chaguo lake la kwanza.
Wakati akiwaza hayo Shaka aliwaza mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyewe. Kama Stella yupo na mtoto wa kigogo basi atahakikisha nguvu zake ziwe mtaji wa kummiliki mrembo yule mwenye nyodo.
Alijua akichemsha japokuwa aliamini kama Betty alimpigia saluti basi Stella si lolote si chochote kwake alijua atamburuza tu. Lakini alihofia kuchemsha na kuonekana hafai na kuharibu CV yake.
Mchezo ulianza huku kila mmoja akiwa makini kuhakikisha hafanyi makosa dakika za mwanzo.
Shaka kwa kujiamini alitumia uzoefu alioupata kwa Betty kutawala mchezo huku Stella naye akiamini kabisa kwa uzoefu alionao baada ya kuwa na mpenzi mzoefu aliyekuwa mtaalamu wa kuangalia mikanda ya wakubwa.
Mchezo kila ulivyokuwa ukienda ndiyo kila mmoja alitaka kujitoa ajulikane yeye ni nani. Shaka alianza kubadilika na kutawala mchezo kutokana na kujaza viungo wengi katikati kutokana na kuona Stella naye si moto wa makaratasi aliyejua kuitumia nyonga yake barabara.
Stella naye hakuwa nyuma pamoja na kuamini Shaka ni mvulana mzuri lakini alijua ni mgeni wa medani ya mapenzi kwa kutumia nyonga yake laini.
Mwanzo aliyaona maji ya magotini lakini muda ulivyokuwa ukienda maji yalianza kupanda taratibu huku Stella akitumia uwezo wake wote kumdhibiti Shaka ambaye alionekana kujua zaidi yake.
Taratibu yalipanda kuelekea shingoni bado Stella aliamini anaweza kuyakabili kwa kutumia uzoefu katika medani ya uroda na uwezo wake wote kuhakikisha maji yale hayamfuniki.
Maji yaliacha shingo na kukifuata kichwa hapo ndipo Stella alipoamini wimbi la Shaka si la kitoto.
“Hapana...hapana Shaka unajua.”
Shaka hakusema lolote zaidi ya kuendelea kukwea mnazi kama komba mzoefu kwa mbwembwe baada ya wimbi la Stella kutulia. Siku zote aliamini huwezi kulamba asali huku unapiga mluzi, lazima utamu wote utautupa nje na kuishia kujilamba.
“Shaka...Shaka,” Stella alimwita Shaka baada ya wazimu kumpanda na kukuna kichwa kama kina chawa.
Shaka hakumuitikia, aliendelea kuwatambuka mabeki waliokuwa wamekata tamaa ya kumkaba kutokana na usumbufu wa kutotulia sehemu moja, hivyo kuipa wakati mgumu beki ya Stella.
“Shaka niitikie mpe..pe..pee..eeeh.”
Stella alikurupuka golini kuuwahi mpira, lakini alipishana nao kutokana na umahiri wa Shaka anapoingia ndani ya kumi na nane. Lilikuwa bao safi lililomfanya mtoto wa kike atetemeke kama amekunywa Cocacola kisha akatulia, alikuwa amekwenda marikiti kwa mara ya nne.
Shaka naye chombo kilikuwa kimefika pwani, alitupa nanga na kukipaki pembeni na kujilaza ubavuni mwa Stella aliyekuwa hoi baada ya piga nikupige. Wote wawili usingizi mzito uliwapitia kutokana na uchovu.
***
Shaka alishtuka usingizi na kuangalia muda kwenye simu ya Stella na kuonesha ni saa tatu usiku.
“Stella mpenzi amka muda umekwenda sana.”
“Mmh! Nimechoka niache nilale kidogo.”
“Hapana Stella tuondoke muda umekwenda sana.”
“Shaka kwa nini tusilale?”
“Hapana baby sasa ni saa tatu tuwahi nyumbani.”
“Shaka unanipenda?” Stella alimuuliza kwa sauti ya kilevi.
“Tena sana.”
“Basi naomba leo tulale kwa mara ya kwanza.”
“Hapana kitamu huliwa kwa hamu pia ukila na kipofu usimshike mkono.”
“Nimekuelewa, lakini naomba kwa leo tu baby.”
“Unawaheshimu wazazi wako?”
“Ndiyo.”
“Unapenda penzi letu liendelee?”
“Ndiyo, tena tuwe mume na mke tuzae na watoto.”
“Basi nyanyuka tukaoge tuwahi nyumbani.”
“Mmh! Sawa baby nakubali kwa vile nakuamini kwa asilimia elfu moja.”
Walikubaliana kuondoka baada ya kwenda kuoga na kutoka, muda ulikuwa saa nne za usiku. Stella alikodi gari na kumpeleka kwanza Shaka kwao na yeye kurudi kwao bila kujua atawaeleza nini wazazi wake.
Shaka akiwa amechoka alirudi nyumbani kwao ambako alikuta wamekwishalala, kwa vile alikuwa na njaa alikwenda kwenye banda la chipsi na kupata chakula cha usiku kisha akarudi nyumbani kulala.
Kabla ya kulala mdogo wake alimweleza taarifa ya Betty.
“Shaka, Betty alikuja zaidi ya mara tano kukuuliza, leo ulienda wapi?”
“Kucheza mpira.”
“Ndiyo maana, yaani ametoka hapa kukuuliza muda si mrefu, vipi anakudai?”
“Walaa.”
“Nenda kamsikilize.”
“Nitamsikiza kesho.”
“Shaka hujui tu, yaani inaonekana yule dada ana shida sana na wewe.”
“Nitamuona kesho.”
Shaka aliogopa kwenda kwa Betty kuhofia kukutana na kalinyekalinye lingine. Kwa jinsi alivyokuwa amechoka alijua lazima atachemsha na Betty atajua ametumika na kuonesha si muaminifu.
“Erick, Betty akija kuniuliza tena mwambie sijarudi.”
“Poa.”
Shaka kutokana na kuchoka sana alipanda kitandani na usingizi mzito ulimchukua.
***
Siku ya pili Shaka alikwenda shuleni kama kawaida, siku hiyo Stella hakwenda kutokana na kipondo kizito cha jana yake kwani aliamka mwili ukimuuma kila kona kama alikuwa akitwanga chuma. Diana alimpitia shoga yake alipofika hakumuona sebuleni kama kawaida yao. Wasiwasi wake alijua amekwishaondoka, alipomuulizia aliambiwa na mama yake:
“Leo mwenzio ameamka mwili wake si mzuri.”
“Anaumwa nini?”
“Anasema kila kona ya mwili inamuuma.”
“Labda malaria?”
“Mmh! Mwenyewe anakataa eti anasema jana sijui mlicheza netiboli shuleni na kuutikisa mwili,” kauli ile kidogo imchekeshe Diana kwa vile jana yake hakukuwa na michezo.
“Sasa yupo wapi?”
“Yupo chumbani kwake bado amelala.”
“Acha nikamuone niwahi shule.”
Diana alichepua mwendo hadi chumbani kwa Stella, kwa vile mlango ulikuwa umeegeshwa aliusukuma na kuingia ndani. Alimkuta shoga yake kapitiwa usingizi mzito akiwa amejichanua kama anataka kujifungua, mikono na miguu ameirusha ovyo.
Alitulia kwa muda na kumuonea huruma shoga yake, lakini upande mwingine alimuonea wivu kwa kuamini Shaka alimtendea haki mpaka kushindwa kwenda shule kilikuwa kipigo cha pweza. Alimsogelea kitandani na kumtikisa taratibu, kutokana na uchovu Stella alijibu sauti ya kichovu bila kufumbua macho.
“Niache nimechoka.”
“Stella mimi Diana.”
Sauti ile ilimshtua na kufumbua macho kichovu na kujinyanyua kitandani huku akipiga miayo.
“Vipi shoga kulikoni?” Diana alimuuliza.
“Mmh! Wee acha tu,” alisema huku akitabasamu na kujinyoosha.
“Niache nini?”
“Kweli mtama ulimshinda ndege akapasuka tumbo.”
“Mmh! Mbona sikuelewi leo umekuwa mama wa ngano za Kiswahili,” Diana hakumuelewa shoga yake.
“Japokuwa jana sikukuaga, nilikuwa na Shaka mwanaume yule koma.”
“Ina maana shughuli ya jana imekufanya hivi?” Edna alishtuka.
“Wee acha tu, Mose cha mtoto. Shaka si mdogo kama tunavyomuona alikulia tumboni kwa mama yake. Aliyonifanyia jana siwezi kusahau, sikuwahi kumwaga bomba la maji matamu kama jana.
“Kama isingekuwa nipo chini ya wazazi ningelala palepale nilikuwa kama mlevi. Hapa nilipo nipo hoi kama nimemaliza mizinga miwili ya pombe kali.”
“Mi nilijua tu, mlitoka saa ngapi?”
“Saa nne na nusu.”
“He! Ulitaka mkae mpaka saa ngapi?”
“Nilitaka tulale mpaka asubuhi.”
“Na nyumbani ungewaambiaje?”
“Ningejua cha kusema.”
“Mmh! Makubwa, wacha niwahi shule.”
“Poa shoga we wahi shule, kuna elfu ishirini yako ipo kwenye droo ya kabati.”
“Asante shoga.”
“Chukua na elfu hamsini mpelekee Shaka.”
“Mmh! Mbona nyingi sana.”
“Za kwako?” Stella alimjibu kwa ukali.
“Basi shoga mbona umekuwa mkali?”
“Wewe nimekupa ishirini kwa kazi gani, mambo yangu na Shaka nakuomba usiyaingilie la sivyo ushoga wetu utakufa,” Stella aligeuka mbogo.
“Basi shoga nisamehe.”
“Kwa hiyo hizo fedha zifike, nikikutana naye nitamuuliza.”
“Nitampa shoga.”
“Basi wahi shule, niite Mona nimwambie dereva akuwahishe shule.”
Edna alitoka nje na kumwita msichana wa kazi na kwenda moja kwa moja chumbani kwa Stella.
“Abee dada.”
“Mwambie Jacob amuwahishe Diana shule.”
“Sawa.”
“Edna shoga yangu tutaonana jioni wacha niendelee kula raha.”
“Hakuna tatizo.”
“Msalimie sana Shaka mwambie nampenda sana,”
ITAENDELEA
Endelea kulike ==>www.facebook.com/2jiachie

Post a Comment