ad

ad

VITILIVYOGO (PAPA NA MUHOGO) - 05


Betty aliuliza baada ya kujiona pumzi zimeanza kukata.
“Kwani wewe tayari?”
“Mi zaidi ya mara nne.”
“Hata mi tayari.”
“Mara ngapi?”
“Mbili.”
“Mmh! Mbona sijaona kushusha mzigo?”
“Kelele zako zilinichanganya, kila uliponiambia Shaka usitoe pasi ingia nayo basi nilikuwa najiona uwanjani nipo peke yangu na kuingia nayo na kila nilipoingia kelele zako zilinichanganya kabisa.”
“Mmh! Japo una staili moja kama njia ya treni lakini lazima nikiri una nguvu kama nyati.”
“Mpaka naomba kuvaa kiatu chako niliamini mguu wangu unatosha.”
“Shaka kuna vitu nikikuongezea utatisha, unaonekana damu bado inachemka ukimshika mwanamke lazima akutaje jina lako.”
“Kwa hiyo umetosheka?”
“Mmh! Leo sitaki tena nipo hoi nikilala sijui nitaamka saa ngapi?”
“Kwa hiyo mpenzi naweza?”
“Unatisha Shaka, nimeinjoi ile mbaya, kumbe nilitaka kumfukuza nyuki asali hii tamu ningeipata wapi?”
5
Sifa za Betty zilimfanya Shaka avimbe kichwa na kujiona kidume mbele ya wanaume. Moyoni hakuamini kama angeweza kumliza kilio cha utamu mwanamke mzoefu kama Betty. Shaka naye alitumia nguvu nyingi kuhakikisha anafuta makosa ya awali ya kutukanwa saizi yake wanuka mikojo wenzake.
Mwili wa Betty uliokuwa umenona kama kitimoto ulimchanganya sana Shaka ambaye alipoutazama chuma hakikulala hata kidogo. Ukichanganya na kelele za Betty zilizompa kichwa kuwa anaweza, alipata wazimu kabisa na kujikuta hatoi pasi, kila mpira alioupata aliingia nao mpaka alipofunga goli au alipogongana na kipa.
Alimtaza Betty aliyekuwa amejilaza pembeni yake bila kitu mwilini, mdomo ulikuwa ukitaka kuendelea kula lakini maungo yalikuwa yamechoka na kujilaza pembeni ya Betty, usingizi mzito ukawachukua.
                                 ***
Betty alikuwa wa kwanza kuamka ambaye kwa mara ya kwanza alihisi uchovu mkubwa sana tofauti na alivyokuwa akidhania uwezo wa Shaka aliyekuwa amejilaza hajitambui kuwa ni mdogo.
Japokuwa alikuwa mgeni katika medani ya mapenzi lakini alikuwa na nguvu sana, anapoamua kushambulia alikuwa harudi nyuma na kumfanya mwanamke kufika safari yake, tofauti na wanaume wengi waliokuwa wakiwaacha  wanawake na shombo.
Njaa nayo ilikuwa ukimuuma kama kidonda, aliamka na kwenda bafuni kujimwagia maji kisha alijifunga vitenge na kukimbilia kwenye baa ya jirani kununua mchemsho ili kutuliza njaa iliyokuwa ikimuuma sana.
Baada ya kununua mchemsho na kurudi ndani, alimuamsha Shaka aliyekuwa akikoroma kama usiku wa manane kuonesha jinsi gani alivyotaabika kuuangusha mbuyu.
“Shaka.”
“Mmh!”
“Amka mpenzi wangu.”
Shaka aliamka akipiga miayo na kujinyoosha.
“Vipi Shaka?”
“Mmh! Nipo hoi tamu lakini wee acha tu.”
“Utazoea tu, huu ni mwanzo.”
“Mmh! Nikizoea mbona nitafaidi.”
“Mi ndiyo nitafaidi zaidi, hujazoea lakini raha unazonipa sikutegemea kuzipata kumbe, ningemfukuza nyuki na kuupoteza utamu bure. Shaka wewe sasa hivi ni nyuki wangu naufaidi utamu bila kikomo.”
“Kumbe naweza?” Shaka hakuamini kauli ya Betty.
“Unaweza sana Shaka.”
Walikwenda kuoga tena na kupata mchemsho wa kuku kisha Betty alimpa Shaka Red Bull ambayo ilimchangamsha na yeye kunywa whisky kuuchangamsha mwili wake.
Siku ile walishinda mpaka usiku ndipo Shaka aliporudi kwao kulala kwa vile siku ya pili alitakiwa kwenda shule. Kabla ya kuondoka Betty alimpa laki mbili ya kununua nguo na viatu ili aendane naye.
“Shaka ukitoka shule kafanye shopping nataka uendane na mimi si unaniona nilivyo?”
“Ndiyo mpenzi.”
“Basi nataka tukiongozana tofauti yetu ibakie kwenye umri tu.”
“Sawa mpenzi nimekuelewa.”
“Basi nikutakie usiku mwema, yaani isingekuwa shule ningekuhamishia hapa.”
“Namaliza muda si mrefu, je akija shemeji?”
“Kazi hiyo niachie mimi, sawa?”
“Sawa mpenzi.”
Shaka aliagana na Betty na kwenda kwao kulala huku mwili ukiwa umechoka sana. Alipofika nyumbani alipanda kitandani kulala na usingizi ulimchukua.
                             ***
Penzi la Betty na Shaka lilishamiri huku mwanafunzi akishika mafunzo yote aliyopewa kiasi cha kumfanya Betty atamani kuachana na mpenzi wake kutokana na kila alipokutana naye alimuona akimpaka shombo mpaka alipomvuta Shaka kwenye akili ndipo alipofika safari yake.
Tatizo likabakia kwa Shaka, hakuwa na kitu zaidi ya kutumia nguvu zake kama mtaji na kuzingatia mafunzo aliyopewa na kuyafuata kwa ufasaha kitu kilichozidi kumchanganya Betty na kufikiria kutafuta fedha ili aachane na mpenzi wake ammiliki Shaka peke yake.
                               ***
Shaka naye alikuwa na madiliko makubwa shuleni kwani alianza kuvaa pamba kali na viatu vya nguvu. Wasichana wengi waligundua kumbe Shaka alikuwa mvulana mzuri pale shuleni tofauti na zamani walivyokuwa wakimuona. Waliamini kama angetafutwa mwanaume mzuri shuleni basi Shaka angeshika nafasi ya kwanza.
Kila msichana mzuri alijikuta akijutia nafasi aliyopewa zamani ya kutongozwa na Shaka na kumtolea nje, wengi walijikuta wakitafuta njia ya kumrudisha mikononi mwao.
Stella, mtoto wa tajiri, mmoja wa wasichana wakali pale shuleni aliyekuwa akijisikia sana, alijikuta akiingia kwenye mateso ya kumtaka Shaka, mvulana ambaye mwanzo hakutaka hata salamu yake.
Siku moja alijificha darasani na kumchunguza Shaka dirishani aliyekuwa amesimama nje ya darasa bila kujua kuna mtu anampiga chabo. Stella aligundua Shaka alikuwa bonge la handsome.
Wakati akiyapa macho yake nafasi ya kumsanifu Shaka, alitokea shoga yake kipenzi, Diana ambaye alipofika nje ya darasa alimkuta Shaka amesimama kama anasubiri kitu.
“Aah! Shaka.”
“Sema.”
“Shaka mambo?”
“Poa,” Shaka alimjibu kwa mkato na kuendelea na mambo yake.
“Shaka mbona nazungumza na wewe huoneshi ushirikiano?”
“Diana unataka ushirikiano upi?”
“Mmh! Makubwa, siku hizi umekuwa hivyo?”
“Diana mi si saizi yako, nitakupaka shombo la kikwapa tu.”
“Jamani Shaka bado unayo ya zamani, yale yalishapita.”
“Sasa tatizo nini?”
“Nakupenda Shaka,” kauli ile ilimchefua sana Stella aliyekuwa akijipanga kwa ajili ya kumvaa Shaka. Alitamani kusema yeye ndiye mpenzi wa Shaka lakini alihofia kuonekana malaya.
“Asante,” Shaka alimjibu Diana bila ya kumtazama.
“Basi naomba jioni tuonane.”
“Mmh! Kwa leo itakuwa vigumu.”
“Lini?”
“Nitakwambia.”
“Basi Shaka usiniangushe.”
“Poa.”
Baada ya kuzungumza na Shaka, Diana aliingia darasani. Alipofika tu Stella alimvaa juujuu.
“Diana ndiyo nini?”
“Kuhusu nini tena shoga?”
“Kwa nini kila ninapotoa mguu na wewe lazima ukanyage.”
“Sijakuelewa unamaanisha nini?”
“Utajilengeshaje kwa Shaka wakati unajua ni mpenzi wangu?”
“Stella ningejuaje kama Shaka ni mpenzi wako?”
“Si ungeuliza?”
“Niulize nini, kwanza wewe ndiye uliyesema Shaka ananuka kama dume la mbuzi.”
“Mbona unanisema mimi, wewe je?”
“Tuache utani sasa hivi Shaka anakimbiza shule nzima,” Diana alimsifia Shaka.
“Yaani hapa nilikuwa namuibia kwa chati, Shaka mzuri atakayejichanganya  anga zangu nitamfanyia kitu mbaya.”
“Stellaaa! Lakini uhusiano na Shaka umeuanza lini?”
“Wiki sasa.” "Mmh! Stella muongo.”
“Kama mi muongo muulize.”
“Mbona alikubali tuonane?”
“Si ameamua kukuyeyusha.”
“Mmh! Tutaona.”
Stella alibakia na siri yake na kupanga jioni ya siku ile ahakikishe anatengeneza mazingira ya kuwa karibu na Shaka kabla shoga yake hajagundua kitu.
                                       ***
Muda wa kutoka shuleni, Shaka alielekea kituo cha daladala kupanda gari japokuwa Betty alimpa fedha ya bodaboda kila siku. Alipokaribia kituoni alisikia akiitwa nyuma na mmoja wa wanafunzi wa kiume wa kidato cha chini.
“Shaks,” aligeuka bila kuitikia.
“Ha, Jay! Vipi mwana?” alimuuliza baada ya kukuta ni mwanafunzi anayemfahamu.
“Nina ujumbe wako.”
“Ujumbe! Upi?” Shaka alishtuka.
“Kutoka kwa Stella.”
“Stella! Yupi?”
“Unayesoma naye.”
“Ooh! Anasemaje?”
“Amenipa bahasha hii.”
Shaka aliipokea na kuiweka kwenye begi la shule na kuelekea kwenye daladala na kuwahi zake nyumbani. Alipofika nyumbani hakukaa sana, alibadili nguo na kwenda kwa mpenzi wake, Betty.
Alipomuona alijawa na furaha.
“Jamani mpenzi wangu za shule?”
“Nzuri mamito.”
ITAENDELEA SIKU YA KESHOOO

No comments

Powered by Blogger.